Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Mithali 18:7 )(
Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, kusingewezekana kuwapo na mpumbavu popote.

Ukishaona kuna uwezekano wa mtu kuwa mpumbavu, hilo ni ushahidi Mungu huyo hayupo.

Mtu kuwa mpumbavu katika ulimwengu ambao una Mungu ni mambo mawili yaliyo mutually exclusive.

Ama una mtu mpumbavu katika ulimwengu ambao hauna Mungu.

Au una ulimwengu ambao una Mungu na hauna mtu mpumbavu.

Haiwezekani ulimwengu ambao una Mungu uweze kuwa na mtu mpumbavu.
 
Sitaki habari za kuamini, nataka kujua.

Thibitisha Mungu yupo.
Udhibitisho upi unautaka!Kwani upepo ulishawahi kuona umbo lake au rangi yake?lakini ukivuma mbona unasema huu ni upepo,tunaamini uwepo wa Mungu kwa matukio tunayoyaona hapa duniani.(
Yohana 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
 
Hujathibitisha Mungu yupo, unahubiri.

Upepo unapimwa na vifaa kama anemometers, wind vanes, windsocks, and wind alarms.

Mungu unahakikishaje yupo kweli?

Thibitisha Mungu yupo, hata kimantiki tu.
 
You are just throwing tantrums.

Unataka nikubaliane na uongo wako?

Thibitisha uwepo wa ulimwengu wa roho.

Sio kuleta stori zako uchwara za vilabuni huko.
Soma hii habari, Ikiwezekana nenda channel ya Wasafi then urudi tujadili jambo
 
Attachments

  • Screenshot_20240807-002121.png
    436.1 KB · Views: 6
Soma hii habari, Ikiwezekana nenda channel ya Wasafi then urudi tujadili jambo
Wazee hao wana maarifa, ujuzi na utaalamu wao ambao mtu wa kawaida huna hayo maarifa.

Kwa hiyo lazima uombe ruhusa za wazee wenye maarifa na ardhi yao.

Hakuna uchawi wala ulimwengu wa roho hapo.
 
Kwa Mungu hakuna lisilowezekana
 
Kuna uwezekano mkubwa Yeshua (Yesu) na Muhammad (Mudi) walikuwa matapeli.

Mmoja alidai yeye ni mtoto wa Yahweh (Mungu). Mwingine alidai yeye ni nabii na mjumbe wa Allah (Mungu).
 
Hili halina ubishi dini inatumika kwa malengo zaidi ya moja ( multipurpose) pale itakapobidi.

Hata michezo hasa soccer inatumika kutimiza malengo mengine inapobidi hususani hapa bongo.

Sasa imani yako wewe iko ipo kwa Mungu au kwa Dini...!? Ya kaisali mpeni kaisali na ya Mungu mpeni Mungu...

Msimchanganye Mungu na dini ninaamini Mungu hana uhusiono na dini ila dini ndio zinauhusiono na MUNGU.

Kuna mahali huko duniani dini hazijafika na baraka wanaipata kama kawaida kama wanastaili.
 
Kuna uwezekano mkubwa Yeshua (Yesu) na Muhammad (Mudi) walikuwa matapeli.

Mmoja alidai yeye ni mtoto wa Yahweh (Mungu). Mwingine alidai yeye ni nabii na mjumbe wa Allah (Mungu).
Kama unahekima ya kutosha unaweza ukawa-classify kwa vigezo ukapata majibu(mbivu na mbichi).

Mambo mengine kufahamu unahitaji roho matakatifu... kwa upeo huu wa ulimwengu wa mwili sio rahisi kujua na kuamini.
 
Umeanza kujitambua.
Hongera sana
 
Mtu kama wewe unatakiwa upelekwe Mtwara ama Tanga ama Kigoma Sasa ukishapata KUJUA kuwa kuna ulimwengu halisi kabisakabisa wa roho, hapohapo unapata KUJUA kuwa MUNGU yupo...
Mbona mi kwetu ni Tanga (nimeenda mara nyingi sana kumsalimu bibi yangu wakato alipokuwa hai)na sijawahi kuuona huo ulimwengu halisi wa kiroho?
 
Hili halina ubishi dini inatumika kwa malengo zaidi ya moja ( multipurpose) pale itakapobidi.

Hata michezo hasa soccer inatumika kutimiza malengo mengine inapobidi hususani hapa bongo.

Sasa imani yako wewe iko ipo kwa Mungu au kwa Dini...!? Ya kaisali mpeni kaisali na ya Mungu mpeni Mungu...
Mimi sina imani ya aina yeyote ile.

Mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani.
Msimchanganye Mungu na dini ninaamini Mungu hana uhusiono na dini ila dini ndio zinauhusiono na MUNGU.
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Mimi sihitaji kuamini, Nataka kujua kwa uthibitisho, ushahidi na uhakika.

Mungu ni dhana ya kufikirika tu, Mungu hayupo katika uhalisia bali katika mawazo ya kufikirika tu, mnayoita imani.

Ndio maana hamuwezi kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu akaonekana yeye kama yeye.

Mungu huyo hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
Kuna mahali huko duniani dini hazijafika na baraka wanaipata kama kawaida kama wanastaili.
Hakuna kitu kinaitwa Baraka.

Baraka ni dhana ya kufikirika tu, iliyotungwa na wanadamu tu.

Baraka ni imaginations just an illusion.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…