Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Ukija kuzeeka utakuwa lizee moja jinga sana! Nakumbuka babu yake mama alikuwa hana dini yeye alikuwa tu wa imani za kimila. Haki ya nani nyumbani kwake kulikuwa kama jehanamu. Simulizi tulizozikuta wanafamilia walikuwa wanapata suruba siyo kidogo!
 
Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Na katika dunia hii hata kama huna dini lakini kuna mungu unaemwabudu pasipo ww kujua ndugu (Mungu wa kweli akutokee ili umwamini)
 
Ulimwengu wa ROHO upo 100%

Is kidding to believe that ur a body creature and not a spiritual creature.

God exist
Believing God exists means you also believe in the afterlife: consciousness and memories ought to vanish with physical death, there's scientific proof that our brains stop working after death; so, how does a soul keep hold of all our memories after death?
 
Mkuu Mimi nilikuwa Kama wewe Ila tukibishana tutakesha Endelea kuamini katika njia yako uliochagua.
 
Sehemu hizo ulizotaja zipo kwenye ulimwengu huu huu unao onekana.

Hakuna ulimwengu mwingine zaidi ya huu.
Mkuu kwani vimelea-bacteria wa typhoid wanakuwaga nje ya mwili wako unapoumwa?

Lakini inahitaji vipimo kuthibitisha.

Unajua Hawa watu wasioamini MUNGU yupo, ndio wanaharibu mambo Kwa kusema kwani watu wakiwa na maadili mabaya kuna tatizo Gani, waache watu waishi watakavyo.
 
Kuamini ni tofauti na kujua.

Unahakikishaje mistari hiyo ipo kweli?
Je unajua ipo kweli au unapingana na hayo?
Na unajuaje kama hayapo?

Ili uweze kupinga uwepo wa kitu unatakiwa uwe na ushahidi wa kuthibitisha sasa tupe ushahidi unaothibitisha MUNGU hayupo

Tofauti na hapo ni unaamini hayupo sio kwamba unajua hayupo
Nb; ushahidi uwe researchable
 
Hayo mambo yote yapo kwenye ulimwengu huu huu.

Kwenye ulimwengu huu huu kuna mambo na vitu vingi sana ambavyo sisi binadamu hatuvijui bado.

Hatuwezi kujua tusivyo vijua ila tunaendelea kupunguza tusivyo vijua kwa utafiti, uchunguzi na udadisi zaidi.

Kwa hiyo ulimwengu ni huu huu mmoja ambao bado tuna endelea ku uchunguza na kuujua vizuri.

Hakuna ulimwengu mwingine unaoitwa wa roho tofauti na huu huu.
Enhe hilo umelijuaje kwamba hakuna ulimwengu zaidi ya huu?
 
Back
Top Bottom