Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Hakuna Mungu anayetoa Uzima wala nguvu kwa kiumbe chochote.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe ajidhihirishe na kujiongelea mwenyewe yeye kama yeye.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea Mungu ambaye hajawahi kuwepo wala hayupo kujiongelea na kujidhihirisha mwenyewe.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Huo utafiti uliufanya lini na ulitumia methodology gani
 
Mkuu Nimesoma Mada yako.Wewe una Muabudu Mungu katika ROHO na KWELI. Tuko wengi ambao Tunamuabudu MUNGU katika ROHO na KWELI ambao tunajidai kusema hatumuamini MUNGU ili kiuhalisia sisi tuna imani kuliko WAFIA DINI.

KARIBU sana Katika KUKUA kwa KIROHO.Endelea Kumuabudu MUNGU katika ROHO na KWELI na kamwe hatokuacha UAIBIKE
 
Ulimwengu ulivyo perfect iv unasemaje hakuna mwanzilishi....yani unataka kusema utam wa chungwa ulijitokezea tu ki bahat bahat , au ule utam ukiwa una ngonoka unahisi ulikuja kuja tu ,
 
Kwa hyo ww ni science believer si ndio
Science ni proven facts tu! Ni mjinga pekee ndiyo anaweza asiamini Science. Bila Science binadamu tusingeweza ku-survive kwenye uso wa Dunia.

Science inaendelea kurekebisha makosa aliyofanya Mungu mnayedai yupo. Mimi nilizaliwa na tatizo la macho (myopia) bila Science leo hii ningekuwa siwezi kuona mbali.

Science ndiyo uti wa mgongo kwenye maisha ya binadamu na itaendelea kubaki hivyo.
 
Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.
"Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema." Zaburi 53:1
 
Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Na iwe kama ulivyonena mkuu... ila ikiwa kuna maisha baada ya kifo rufaa iko wazi. Na kwa muktadha huu jehanamu na habari za moto wa milele havikuhusu.
 
Science ni proven facts tu! Ni mjinga pekee ndiyo anaweza asiamini Science. Bila Science binadamu tusingeweza ku-survive kwenye uso wa Dunia.

Science inaendelea kurekebisha makosa aliyofanya Mungu mnayedai yupo. Mimi nilizaliwa na tatizo la macho (myopia) bila Science leo hii ningekuwa siwezi kuona mbali.

Science ndiyo uti wa mgongo kwenye maisha ya binadamu na itaendelea kubaki hivyo.
What about unproven theories kama bing bang theory unaniamin au huamini chochote kuhusu origin of life?
 
Science ni proven facts tu! Ni mjinga pekee ndiyo anaweza asiamini Science. Bila Science binadamu tusingeweza ku-survive kwenye uso wa Dunia.

Science inaendelea kurekebisha makosa aliyofanya Mungu mnayedai yupo. Mimi nilizaliwa na tatizo la macho (myopia) bila Science leo hii ningekuwa siwezi kuona mbali.

Science ndiyo uti wa mgongo kwenye maisha ya binadamu na itaendelea kubaki hivyo.
Mkuu BILA MUNGU hakuna sayansi kama unabisha tafuta maana ya sayansi afu tafakari wanasayansi wanatoa wapi hizo tafiti na vumbuzi zao.

Kwa fikra hizo za kuamini katika sayansi unakua hauna tofauti na na mtu anayeokota pesa ndani ya nyumba ya mtu arafu bila shaka anasema ni yake.
 
Ww tuelezee unafaham nn kuhusu origin of life?
Jibu sahihi kwa swali la jinsi maisha yalivyotokea, ulimwengu ulitoka wapi ni "sijui".

Kama binadamu labda hatujui bado, lakini kuna jibu. Nina furaha kukubali ambapo ujuzi wangu unaishia.

Kwa hivyo; kama mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu, sijui jibu la swali hilo, na sidhani kama kuna mtu yeyote anayejua pia.

Kwa maana hiyo hakuna kitu kinachopaswa kudaiwa au kuaminiwa bila ushahidi kuwa ndiyo chanzo cha maisha na ulimwengu.
 
Kama kuna maelezo yapo aliyowahi kutamka moja kwa moja kuwa HAAMINI ni vyema ukaleta hapa chief
Yan kusema hivyo tu inatosha kuonyeaha kwamba hana uhakika, na inafikirisha kweli. Juz nimetoka kuona mzungu mmoja anahoji kwamba wanasema Mungu yupo na anatupenda sana ila huyu Mungu anaetupenda sana kaumba pepo na moto na ana sheria zake kumi ( ten commandments ) ambazo anazitumia kama reference usipofuata kuna moto kakuandalia atakuchoma vibaya uungue milele, yeye ndie alieumba shetani ila hawez kuliangamiza na ndio yeye anajua litakalokutokea kesho ila hawez kulikontrol baya lisikutokee, mkuu huoni kama this is illogical ? Hatujapigwa kweli hapo na kitu kizito ? Alafu akasema ukianza kuhoji vitu kama hivyo unaletewa reference ya maneno ambayo yapo kwenye maandish ambayo yamepewa vifungu na mistari au aya ambayo watu wanasema yalishuka kutoka mbinguni.
Mimi sisemi Mungu hayupo ila wazungu waongo sana aisee walitudanganya na kama hizi dini zina watu basi ni wa middle east sio huku sababu zote zimeanzia huko. Wazungu wamedanganya mambo mengi sana ukianza kuyalogic unaletewa vifungu vya maneno ya kwenye kitabu ambacho hata wewe unaweza kuandika
 
Ukija kuzeeka utakuwa lizee moja jinga sana! Nakumbuka babu yake mama alikuwa hana dini yeye alikuwa tu wa imani za kimila. Haki ya nani nyumbani kwake kulikuwa kama jehanamu. Simulizi tulizozikuta wanafamilia walikuwa wanapata suruba siyo kidogo!
😂😂😂😂😂 nimecheka daaah 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom