Mimi nimekaa Marekani mji wa Washington. Ubaya wa Marekani hakuna undugu kila mtu kivyake kiutafutaji. Maisha ya Marekani ni magumu sana kwa kiingereza tunaita hand to mouth. Kwa gharama ya $600 kwa mwezi naona mtu huyo anapata mateso makubwa. Kama alivyosema kuwa anaweka akiba ya $4500 kwa mwezi. Kwa Afrika ukiwa unajishughulisha hicho kiasi ni kidogo kwa mfanyabiashara wa Afrika. Kinachotuharibu hapa Afrika hatuna utaratibu mzuri wa maisha. Familia tegemezi za afrika huwezi linganisha na familia ya America ya mtu mmoja, mkewe na mtoto. Nawashauri hapa kwetu Afrika kuna fursa nyingi sana kuliko America ambapo hata usingizi hupati kwa kudandia kazi za kuhama hama kwa siku.