Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Bongo ukiuza vitumbua unatusua??!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mkuu hassle zako UA nazielewa najifunza Vitu Vingi,..hongera San mkuu,..but nasikia Guangzhou na London wabongo wanapata tabu sana

Mkuu umenikumbusha kuna siku (2014/15) napita Gordon Square (London) nasafari zangu kuelekea Guilford Street, mvua imeanza kunyesha na nilikuwa nimebeba mwamvuli. Kuna dada alikuwa jirani, kwa vile alikuwa na ngozi yenye rangi kama yangu sikuogopa, nikaunyanyua zaidi mwamvuli umfunike na yeye. Baada ya kushukuru, tukaulizana tunapoelekea, tukajikuta sote tulikuwa na njia moja (isipokuwa yeye safari yake ilikuwa inaishia jirani-Russell Square Underground Station). Na pia hapo tukatambua kuwa sote tulikuwa tunatoka nchi moja (Tanzania). Kwa kumuangalia tu, yule dada alikuwa amechoka (nguo zimechoka, ongea yake na hata sura vyote vilikuwa ni vya kinyonge). Kwa muda mfupi tuliotembea nilimueleza ninachofanya hapo London, na yeye akanisimulia anapoishi na alivyofika huko. Roho iliniuma, nilitamani nikutane na kila mwenye ndoto za kwenda nje ya nchi bila ya kuwa na mpango uliokuwa thabiti nimueleze asifanye hilo kosa.
Yule dada aliniambia alimaliza kidato cha sita miaka ya mwanzoni mwa 90, na alipata daraja la pili (sikumbuki vizuri mchepuo, lakini ni kati ya PCM au PCB). Kwa miaka hiyo, huo niliuona ni ufaulu mzuri saaana. Akaniambia yupo mtu alikuwa jirani yao, anakaa sana Uingereza, akamshauri waende wote Uingereza. Anadai hakujiuliza mara mbili akakubali, na hakwenda chuo, na huko Uingereza hakuwahi kupata nafasi ya kusoma na anafanya vibarua vya siku (akibahatika) ambavyo mara nyingi ni vya "minimum wage". Aliniumiza zaidi, alinitajia classmates wake wa A'level, kidogo nitoe chozi (mmoja ni kwa kipindi hicho alikuwa Katibu Mkuu Wizara fulani). Alichojutia na ambacho pia ni funzo kwa watu wanakwenda nje ni kuwa "unapoona maisha hayaeleweki ukiwa nje, hima rudi nyumbani". Kadri unavyochelewa kurudi nyumbani, ndivyo unavyopata "pressure" kuwa wenzako (cohort) watakuwa wamepiga hatua, na wewe utakuwa kituko. Hii nilielewa kwa jinsi nilivyokuwa natafsiri mazungumzo yake. Na nikaja pia kukutana na hali hiyo kwa dada mwingine ambaye hakuwa anatamani kabisa kurudi kutokana na hiyo "pressure" (ingawa huyu wa pili alikuwa Mkenya)
 
 
Huyu hakuwa mpambanaji bali msomi anayetegemea karatasi ili kuishi. Ila mpambanaji lazima atoke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha KUOKOTEZA HABARI ZA VIJIWENI ,,,,usidanganye WATU..,kama kweli ulikuwa unasoma kule tuwekee RESDENT PARMIT HAPO....MAISHA NI POPOTE.,,huo UHALIFU UNAOSEMA wasouth WENYEWE NA WAZIMBABWE NDY NAMBA MOJA.....UHALIFU ni kila sehem DUNIANI,,,usiwadhalilishe WAISHIO SOUTH AFRICA....kama wewe MAISHA YAKO YA KUUZA GENGE TANZANIA yanakwenda Basi USIDANGANYE WENZIO....MABAHARIA MSIOGOPE....MAISHA POPOTE...hyo mwongo tu..hana ANACHOKIJUWA...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandende katika ubora wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi yule jamaa aliyekua anakalipiana na mhudumu wa hotel kwa kushindwa kulipia hotel ukagundua kua ni mTanzania, haiwezekani ugenini ghafla atokee mbongo mwenzio na akaweka mazingira ya mpaka weww utoke nje,hiyo ni walikujua kitambo yamkini toka unaingia nchini humo,matapeli wana mnyororo mrefu sana,hapo ulikua unalengwa na kama hawakufanya chochote basi waligundua wewe hujaenda kusotea ya kwamba yamkini una shilingi mbili tatu watakazo weza kukukwapua kwa kukupiga kiswahili,pia watakua waliona una mishe zako zinazoeleweka na pesa iko bank hawawezi ichukua,so wakaamua kuachana nawe.
 
Mie nko Milton Keynes naona watanzania wa uku wengi wanafanya kazi na wako vizuri na wanasaidiana sana. Changamoto kubwa ya Watanzania hatusaidiani kabisa yani tofauti na Wanigeria. Yani hawa wanigeria wanasaidiana sana na wamejaa mno uku akija ata kusoma lazma abebe na familia yake.
 
Maisha yapo Bongo maana watu bado wamelala Sana na fursa kibao. Tofauti na ughaibuni. Elimu (recognized worldwide) bado nafuu Sana ukilinganisha na Ughaibuni. Eg. Fikiria Mangi anakuja town anaanza kupiga Rangi viatu baadae kibanda, Mara kiosk mwishowe Duka, yard na anatoboa. Ndo uone fursa bongo bado fursa kibao "virgin" kila sekta. La muhimu usione aibu kuanzia chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…