Maisha hapo awali katika Mars

Maisha hapo awali katika Mars

mbenge

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
4,864
Reaction score
10,483
Huenda Ibilisi pamoja na malaika wengine waovu kabla ya kushindwa vita huko mbinguni waliishi katika sayari ya Mars. Ni lazima nikiri ukweli ya kwamba hakuna nyaraka zilizopo ambazo zinaweza kubainisha jambo hili moja kwa moja, isipokuwa tunaweza kupata picha ya jambo hili kupitia maandiko matakatifu.

Kwa kuwa maandiko matakatifu yanaweza kujitetea yenyewe pasipo msaada wa nyaraka nyingine, basi uwezekano wa jambo hili unaweza kuwekwa wazi kupitia vifungu vya mbalimbali aya zilizopo ndani yake. Aya hizi zikiweza kuangaliwa vyema vitalithibitisha jambo hili.

Ni ukweli ya kuwa kulitokea vita ya uasi mbinguni, ambapo malaika mkuu Mikaeli pamoja na malaika wengine waaminifu kwa Mungu, walipambana na Ibilisi pamoja na malaika wengine waovu. Matokeo ya vita hivyo ni kwamba malaika waovu walishindwa na kufurumushwa mbinguni.

Malaika hao walitupwa katika sayari ya dunia na kuwekwa vifungoni. Sehemu hii iitwayo kuzimu ilikuwa ni chini ya sura nchi ambayo ilikuwa imezungukwa juu yake na giza nene pamoja na vilindi vya maji mengi.

Ukweli huu tunaupata kupitia nukuu ya historia ya kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu kama vile ifuatavyo;

Mwanzo 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Aidha, tukirejea katika maandiko, inatudhihirishia kuwa Ibilisi kabla ya vita huko mbinguni hakuwa akiishi huko mbinguni. Bali alipanda kwenda mbinguni makao ya Mungu ili akafanye uasi ili naye aweze kuinua kiti chake cha enzi cha kifalme na aweze kufanana na Muumba wake.

Nukuu kuhusu ukweli huu tunaweza kuipata kama vile ifuatavyo;

Isaya 14

12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.

Kuna kila dalili uwanja wa mapambano haukuwa mbinguni katika makao ya Mungu aliye hai, bali walifurumushwa na hatimaye mapambano makali yalifanyika katika makao yao, yaani sayari hii ya Mars. Licha ya vita hii kufanyika huko, tunaupata ukweli huu kwa kuwa kwa mwanadamu eneo lote la juu ya nchi huitwa mbingu kama vile ambapo tunapata nukuu kutoka katika maandiko;

Mwanzo 1
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili"

Mungu ndiye asili ya vyote, kwa Yeye ndiye Muumbaji wa vitu vyote na anamiliki vyote. Aliitambua nia ya Ibilisi na asingiweza kamwe aweze kufikia sehemu aishiyo ili apate kufanya vita dhidi yake. Bali ni kweli vita vya kiroho vilitokea kupitia nukuu ifuatavyo ya maandiko;

Ufunuo wa Yohana 12

7 Kisha, kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake.
8 Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.
9 Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani ambaye huudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.

Ukizichumguza picha za sura ya sayari kutoka kwa vyombo vya "rovers" vya USA na China vilivyopo huko hivi sasa. Ama chombo cha anga kilichopelekwa na India katika "orbit" ya Mars utaona mahame yaliyopo ndani yake. Utauona mfanano wa mahame na ya zile picha za Sodoma na Gomora zilizoteketezwa na moto wa Mungu kupitia kwa malaika wake.

Sura ya sayari ya Mars inaonyesha kuna kila dalili za uwepo wa maisha na maji hapo zamani za kale. Na huu ni ukweli ambao hata Ibilisi mwenyewe anautambua na hapingani nao.

Ibilisi anatambua ukweli ndiyo maana anafanya kila awezalo ili aweze kurudi huko. Yeye ana asili ya mwili wa kiroho ulioumbwa nao kwa asili, nao uliumbwa kwa upepo na miali ya moto, hivyo hawezi kwenda huko bila ya msaada wa mwanadamu ambaye ana mwili ambao umeumbwa kwa udongo.

Waebrania 1
7 Anapozungumza juu ya malaika anasema: “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.”

Napenda kuhitimisha mada yangu kwa kusema, huenda Ibilisi aliishi kabla ya uwepo wa mwanadamu katika sayari ya Mars. Makao yake katika sayari hii pengine yaliangamizwa kutokana uasi wake dhidi ya usasi kwa Mungu na Muumbaji wake.
 
Picha za muonekano wa sayari ya Mars
IMG-20211202-WA0042.jpg
IMG-20211209-WA0055.jpg
 
Kwenye bandiko lako umeshindwa kutofautisha Realm na Sayari.
Je kwa mantiki hiyo unataka kutuambia mbinguni au makazi ya Malaika ni sayari ya Mars??
 
Mkuu, pengine hukusoma na kutambua mantiki iliyopo nyuma ya aya ambazo nimezinukuu kutoka katika maandiko. Ufafanuzi ni kwamba maandiko hutuambia kuwa mbingu kwa mwanadamu ni eneo lililopo juu ya nchi, sehemu ambayo anaishi kwa asili.

Kwa hiyo eneo lote ambalo jua, mwezi na hata sayari hii ipo hutambulika kama eneo la mbingu. Lakini pia maandiko yanatuambia Shetani hakuwa akiishi daima mbinguni, bali alikuwa akienda huko kwa 'occasions' fulani fulani hasa za ibada, nukuu iliyopo katika Isaya 14

Labda kwa msaada wa kimaandiko tunaweza pia kusoma katika;

Ayubu 38
18 Je, wewe unafahamu ukubwa wa dunia? Niambie kama unajua haya yote.
19 “Njia ya kufika kwenye makao ya nuru ni ipi? Nako maskani mwa giza ni wapi?
20 Je, unaweza kuvirudisha kwenye makao yake? Unajua njia za kufika maskani mwake?

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Badao naendelea na tafakuri yangu kuhusu vita vya uasi vilivyotokea mbinguni kabla ya mwanadamu kuumbwa na Mungu. Bado ninaamini ya kuwa huenda vita hiyo kubwa katika ulimwengu wa roho havikufanyika katika makao rasmi ya Mungu mbinguni, bali vilifanyika makao ya hao malaika walioasi.

Makao rasmi ni sehemu takatifu sana, na ndipo kilipo kiti chake cha enzi. Mungu kwa vyovyote vile hawezi kurusu dhambi ama udhaifu utokee katika sehemu hii.

Kumbuka katika nyakati hizo, jeshi la malaika watakatifu yalikuwa chini ya malaika wakuu watatu, yaani Mikaeli, Gabrieli na Lucifa. Malaika hawa wakuu kila mmoja wao chini yake alikuwa na safu ya malaika wapatao theluthi moja ya idadi ya malaika wote waliopo mbinguni.

Safu ya jeshi lililokuwa chini ya malaika mkuu Mikaeli ilikuwa na dhamana ya ulinzi na usalama mbinguni, safu ya jeshi lililokuwa chini ya malaika mkuu Gabrieli ilihusika na dhamana ya kusimamia masuala ya logistiki na utawala mbinguni, wakati ile safu ya jeshi lililokuwa chini ya Lucifa ilihusika na kusherehesha kwa nyimbo za sifa na kuabudu kwa Mungu wao mbinguni.

Uasi ulipotokea mbinguni, iliwapasa malaika wote washiriki ili waweze kuamua wenyewe kwa hiari yao juu ya hatma yao, na juu nani hasa wanapaswa kumtii. Theluthi mbili iliweza kusimama upande wa Muumba wao, na theluthi moja iliyokuwa chini ya Ibilisi ikaasi pamoja naye.

Ukiangalia picha ya vita vya Har Magedoni vitakavyokuwa, ni sawa kabisa kabisa na vile vilivyopita. Ibilisi na majeshi ya nchi zote duniani yatajikusanya pamoja na zana za kisasa za kivita, lakini hayawezi kupewa nafasi hata kidogo kumsogelea Muumba wao, bali wataangamizwa pasipo kupiga hata risasi moja. Pengine nukuu hapa chini ya maandiko inaweza kuchagiza hiki ambacho ninakizungumzia;

Ufunuo 19

19 Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake.

20 Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake). Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti.

21 Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.

porojo na hekaya tu hakuna ukweli wowote,hakuna viumbe wanaitwa Shetani,malaika,mungu,mbingu,
Kuzimu,jehanam,akhera!
Na hiyo vita unayoiongelea Hata haipo na haitakuja kuwepo,hakuna Mwisho wa Dunia Wala wa mars hizo ni porojo tu
Dunia itafika Mwisho pale mfumo wetu wa nyota utakapokua supernova tu mengine ni uongo uongo na propaganda,

Povu ruksa!
 
Mtumishi, nyuzi zingine zipo kwa ajili ya mambo ya imani za kiroho. Mada zilizopo ndani yake ni kama upuuzi tu kwa yule asiyeaamini. Kwa hiyo unaweza tu kupita kimya kimya huku moyoni mwako ukizipuuzia.

Jambo pekee ambalo naweza kukushirikisha, ni kuhusu maana ya neno "imani" pale linapotumika ndani ya maandiko matakatifu. Nukuu ya vifungu vifuatavyo vinaweza kutupa tafakari kama vile ifuatavyo;

Waebrania 11

1 Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni uhakika wa mambo tusiyoyaona.

2 Maana ni kwa imani wazee wa kale walipata kibali cha Mungu.

3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vinavyoonekana vilitengenezwa kutokana na vitu visivyoonekana.
 
1 Wakorintho

18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopotea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

19 Maandiko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzikataa akili za wenye akili.”

20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga?

21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa.

[emoji120]
 
Kwanini umechagua sayari ya Mars na si Jupita? au yoyote kuna sehemu Mars imetajwa?
 
Mkuu Einstein, udadisi mkubwa ambao unafanywa hivi sasa katika sayari ya Mars, tukianza na NASA kupitia chombo chao cha "Perseverance" huku kimkakati washirikiana kwa karibu na Elon Musk kupitia SPACE X. Na pia CNSA na chombo chao cha "Zhurong" pamoja na kile kingine cha India yaani "Mangalayaan" vyote kwa pamoja vinachunguza kuhusu uwepo wa uhai ama maji katika sayari.

Udadisi huu kutokana na ukaribu wa sayari hii na dunia, ni kitu ambacho kinaweza kuamsha udadisi wa kwa nini vifanyike katika sayari na wala siyo nyingine. Ile hamu ya watu hawa kutaka kwenda kuishi huko inaonyesha pengine kuna habari ya siri za huko. Gharama kubwa zinazotumika ya kwenda huko, licha ya umbali na baridi kali iliyoko huko inaweza kudhihirisha ukweli huo.

Yapo makundi ya siri ambao hujiita kuwa wao ndiyo wamefunuliwa mambo ya siri na Shetani mwenyewe. Pengine hii ndiyo sababu yenye kuifanya Mars kuwa sayari lengwa kuifanya kuwa koloni jipya na hatimaye kama makazi mapya kwa mwanadamu.

Kama kawaida, nukuu ifuatavyo kutoka katika maandiko matakatifu inaweza kutupa uwepo wa makazi sehemu fulani mbinguni, ambayo huitwa kama mbingu ya tatu. Sehemu ambayo Shetani hajawahi kuifahamu hapo awali.

2 Wakorintho 12

2 Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua.

3 Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua.

4 Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka.
 
Badao naendelea na tafakuri yangu kuhusu vita vya uasi vilivyotokea mbinguni kabla ya mwanadamu kuumbwa na Mungu. Bado ninaamini ya kuwa huenda vita hiyo kubwa katika ulimwengu wa roho havikufanyika katika makao rasmi ya Mungu mbinguni, bali vilifanyika makao ya hao malaika walioasi.

Makao rasmi ni sehemu takatifu sana, na ndipo kilipo kiti chake cha enzi. Mungu kwa vyovyote vile hawezi kurusu dhambi ama udhaifu utokee katika sehemu hii.

Kumbuka katika nyakati hizo, jeshi la malaika watakatifu yalikuwa chini ya malaika wakuu watatu, yaani Mikaeli, Gabrieli na Lucifa. Malaika hawa wakuu kila mmoja wao chini yake alikuwa na safu ya malaika wapatao theluthi moja ya idadi ya malaika wote waliopo mbinguni.

Safu ya jeshi lililokuwa chini ya malaika mkuu Mikaeli ilikuwa na dhamana ya ulinzi na usalama mbinguni, safu ya jeshi lililokuwa chini ya malaika mkuu Gabrieli ilihusika na dhamana ya kusimamia masuala ya logistiki na utawala mbinguni, wakati ile safu ya jeshi lililokuwa chini ya Lucifa ilihusika na kusherehesha kwa nyimbo za sifa na kuabudu kwa Mungu wao mbinguni.

Uasi ulipotokea mbinguni, iliwapasa malaika wote washiriki ili waweze kuamua wenyewe kwa hiari yao juu ya hatma yao, na juu nani hasa wanapaswa kumtii. Theluthi mbili iliweza kusimama upande wa Muumba wao, na theluthi moja iliyokuwa chini ya Ibilisi ikaasi pamoja naye.

Ukiangalia picha ya vita vya Har Magedoni vitakavyokuwa, ni sawa kabisa kabisa na vile vilivyopita. Ibilisi na majeshi ya nchi zote duniani yatajikusanya pamoja na zana za kisasa za kivita, lakini hayawezi kupewa nafasi hata kidogo kumsogelea Muumba wao, bali wataangamizwa pasipo kupiga hata risasi moja. Pengine nukuu hapa chini ya maandiko inaweza kuchagiza hiki ambacho ninakizungumzia;

Ufunuo 19

19 Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake.

20 Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotosha wale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambao walikuwa wameiabudu sanamu yake). Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti.

21 Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Hapo mwanzo hakukua na kitu au watu wengine zaidi ya malaika na Mungu wao sasa hayo majeshi yote yalikua ya kazi gani sehemu takatifu?? Yani walikua wanalinda nini wakati hamna threat yoyote kutoka nje? Je walijua kuwa kuna malaika wataasi au mpaka kukawa na majeshi mbinguni?.
 
Mkuu Wild Sniper, mbinguni katika makao rasmi ya Mungu Mkuu kipo kiti chake cha enzi. Naye huitwa Mungu kwa kuwa daima na milele hutambulika kwa sifa zake za kipekee, yaani ndiye ambaye ni Mwanzo na Mwisho, Muumbaji, Mwokozi, Bwana wa mabwana, na pia ndiye Mfalme wa wafalme.

Maandiko matakatifu hayatoi majibu ya moja kwa moja juu ya kuwapo kwa miungu wengine walio hai kama Yeye. Lakini maandiko haya haya yanakubali kuhusu utawala wake wa kifalme mbinguni huku akihudumiwa na mamilioni ya malaika zake watakatifu.

Kuhusu uwepo wa tishio kwake mpake ikamlazimu kuweka safu ya jeshi lenye dhamana ya ulinzi na usalama ni kitu ambacho kinazungumzika. Pengine nukuu ifuatavyo kutoka katika maandiko hayo hayo inaweza kutupa tafakari zaidi;

Warumi 11

33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachu nguziki!

34 Kwa maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake?

35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe?

36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu kwake. Utukufu ni wake milele.
Amina.
 
Nashukuru mkuu, lakini nadhani biblia inatambua uwepo wa Miungu wengine na hata Mungu pia anatambua ndo mana anasema usiabudu Miungu wengine ila mimi.
Kuhusu jeshi bado sijapata mwanga na maana halisi ya uwepo wake .
 
Ni kweli kabisa, maandiko yanatambua uwepo wa miungu wengine ambao hawapo hai. Nao wametajwa mara nyingi sana katika Neno lake.

Lakini kwa habari za miungu walio hai, hakuna Mungu Mkuu anayetajwa zaidi yake. Ibilisi anatajwa tu kama mungu atendaye uovu na ni wa dunia hii. Pia wanadamu walio na jukumu la kuhukumu wengine hutajwa pia kama sehemu ya miungu.

Maandiko yafuatayo yanaweza kutupa ufahamu zaidi;

2 Wakorintho 4

4 Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.

5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.

6 Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ingʼae gizani,” ameifanya nuru yake ingʼae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.

Na pia kwa nukuu ifuatayo hapa chini tena

Zaburi 82

1 Mungu anasimamia baraza lake; anatoa hukumu katika kusanyiko la miungu:

2 Mpaka lini mtaendelea kuhukumu bila haki na kuwapendelea watu waovu?

3 Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara.

4 Waokoeni wanyonge na maskini, waokoeni makuchani mwa wadhalimu.

5 Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu! Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu! Misingi yote ya haki duniani imetikiswa!

6 Mimi nilisema kuwa nyinyi ni miungu; kwamba nyote ni watoto wa Mungu Mkuu!
 
Back
Top Bottom