mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Huenda Ibilisi pamoja na malaika wengine waovu kabla ya kushindwa vita huko mbinguni waliishi katika sayari ya Mars. Ni lazima nikiri ukweli ya kwamba hakuna nyaraka zilizopo ambazo zinaweza kubainisha jambo hili moja kwa moja, isipokuwa tunaweza kupata picha ya jambo hili kupitia maandiko matakatifu.
Kwa kuwa maandiko matakatifu yanaweza kujitetea yenyewe pasipo msaada wa nyaraka nyingine, basi uwezekano wa jambo hili unaweza kuwekwa wazi kupitia vifungu vya mbalimbali aya zilizopo ndani yake. Aya hizi zikiweza kuangaliwa vyema vitalithibitisha jambo hili.
Ni ukweli ya kuwa kulitokea vita ya uasi mbinguni, ambapo malaika mkuu Mikaeli pamoja na malaika wengine waaminifu kwa Mungu, walipambana na Ibilisi pamoja na malaika wengine waovu. Matokeo ya vita hivyo ni kwamba malaika waovu walishindwa na kufurumushwa mbinguni.
Malaika hao walitupwa katika sayari ya dunia na kuwekwa vifungoni. Sehemu hii iitwayo kuzimu ilikuwa ni chini ya sura nchi ambayo ilikuwa imezungukwa juu yake na giza nene pamoja na vilindi vya maji mengi.
Ukweli huu tunaupata kupitia nukuu ya historia ya kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu kama vile ifuatavyo;
Mwanzo 1
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Aidha, tukirejea katika maandiko, inatudhihirishia kuwa Ibilisi kabla ya vita huko mbinguni hakuwa akiishi huko mbinguni. Bali alipanda kwenda mbinguni makao ya Mungu ili akafanye uasi ili naye aweze kuinua kiti chake cha enzi cha kifalme na aweze kufanana na Muumba wake.
Nukuu kuhusu ukweli huu tunaweza kuipata kama vile ifuatavyo;
Isaya 14
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Kuna kila dalili uwanja wa mapambano haukuwa mbinguni katika makao ya Mungu aliye hai, bali walifurumushwa na hatimaye mapambano makali yalifanyika katika makao yao, yaani sayari hii ya Mars. Licha ya vita hii kufanyika huko, tunaupata ukweli huu kwa kuwa kwa mwanadamu eneo lote la juu ya nchi huitwa mbingu kama vile ambapo tunapata nukuu kutoka katika maandiko;
Mwanzo 1
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga hilo. Ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita anga “Mbingu.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya pili"
Mungu ndiye asili ya vyote, kwa Yeye ndiye Muumbaji wa vitu vyote na anamiliki vyote. Aliitambua nia ya Ibilisi na asingiweza kamwe aweze kufikia sehemu aishiyo ili apate kufanya vita dhidi yake. Bali ni kweli vita vya kiroho vilitokea kupitia nukuu ifuatavyo ya maandiko;
Ufunuo wa Yohana 12
7 Kisha, kukazuka vita mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalo likawashambulia pamoja na malaika wake.
8 Lakini joka hilo na malaika wake walishindwa, na hatimaye hapakuwa tena na nafasi mbinguni kwa ajili yao.
9 Basi, joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyoka wa kale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani ambaye huudanganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.
Ukizichumguza picha za sura ya sayari kutoka kwa vyombo vya "rovers" vya USA na China vilivyopo huko hivi sasa. Ama chombo cha anga kilichopelekwa na India katika "orbit" ya Mars utaona mahame yaliyopo ndani yake. Utauona mfanano wa mahame na ya zile picha za Sodoma na Gomora zilizoteketezwa na moto wa Mungu kupitia kwa malaika wake.
Sura ya sayari ya Mars inaonyesha kuna kila dalili za uwepo wa maisha na maji hapo zamani za kale. Na huu ni ukweli ambao hata Ibilisi mwenyewe anautambua na hapingani nao.
Ibilisi anatambua ukweli ndiyo maana anafanya kila awezalo ili aweze kurudi huko. Yeye ana asili ya mwili wa kiroho ulioumbwa nao kwa asili, nao uliumbwa kwa upepo na miali ya moto, hivyo hawezi kwenda huko bila ya msaada wa mwanadamu ambaye ana mwili ambao umeumbwa kwa udongo.
Waebrania 1
7 Anapozungumza juu ya malaika anasema: “Anawafanya malaika wake kuwa upepo, watumishi wake kuwa ndimi za moto.”
Napenda kuhitimisha mada yangu kwa kusema, huenda Ibilisi aliishi kabla ya uwepo wa mwanadamu katika sayari ya Mars. Makao yake katika sayari hii pengine yaliangamizwa kutokana uasi wake dhidi ya usasi kwa Mungu na Muumbaji wake.