Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
MAISHA HAYANA FORMULA LAKINI YANA SIRI NYINGI! ANGALIA HIZI 11, KAMA ZITAWEZA KUKUFAA
1. SIRI YA KWANZA
Tengeneza "connection" na watu usitengeneze urafiki, Iko siku marafiki uliowatengeneza watakugeuza Chakula Cha Kula maana "kikulacho kinguoni kwako!", Siyo rahisi rafiki akakubali upate zaidi yake!
2. SIRI YA PILI
Usimwamini sana rafiki yako, kwa sababu huyo rafiki yako ana rafiki yake ambaye wewe si rafiki yako!, Kama hunielewi subiri siku umseme bosi wako akurekodi halafu amrushie boss wako then boss wako akurushie. Utatamani kufa.
3. SIRI YA TATU
Kuna njia tatu tu za kufanikiwa maishani. Njia hizo ni;
1. Bahati,
2. Kipaji na
3. Bidii yenye akili!,
Jitafute ulipo! Huna bahati, huna kipaji halafu unalala mchana?
4. SIRI YA NNE
Ukiwa na marafiki watano majambazi tegemea kuwa jambazi wa sita; ukiwa na marafiki watano wahuni tegemea kuwa muhuni wa sita, ukiwa na marafiki watano mabilionea tegemea kuwa bilionea wa sita; kasheshe ni pale unapokuwa masikini kumpata rafiki bilionea maana wahenga walisema ndege wanaofanana huruka pamoja.
5. SIRI YA TANO
Ukiona kila mtu anakurushia mawe usijifariji kwamba mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, kuna miti mingine inapigwa mawe kwa sababu ina nyoka!, Kikubwa jitathimini pengine wewe ni Mfalme mwenye mkia, ila hujauona.
6. SIRI YA SITA
Kuwa makini sana na watu wanaosema tuko nyuma yako maana ukigeuka unaweza usiwakute. Kama kivuli chako mwenyewe ikifika usiku kinakukimbia vipi huyo mtu asiyekula kwako?
7. SIRI YA SABA
Ili ufurahie maisha, jifunze kujinyenyekeza na siyo kujikomba!, Unyenyekevu ni kiwango cha juu kabisa cha matumizi ya akili, kujikomba ni kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya akili! Moja ya madhara ya kujikomba ni kuishi maisha ya hovyo!
8. SIRI YA NANE
Kabla hujafanya maamuzi jitahidi kupata ukweli wa jambo kutoka pande zote. Leo hii watoto wengi hawana mahusiano na baba zao kwa sababu ya kusikiliza ufundi wa mama zao katika kusimulia mabaya ya baba zao! Hawayajui ya mama yao kwa sababu baba yao alichagua kuyaficha! Kama unamchukia baba yako hebu muombe msamaha kwanza halafu mwambie akusimulie ya mama yako.
9. SIRI YA TISA
Mlango mmoja ukifungwa usihangaike kuufungua, unaweza ubomoa bure. Pita hata dirishani maana kisicho riziki hakiliki! Asiyekupenda muache aende zake, tena mpe na nauli.
10. SIRI YA KUMI
Hata kama umeishafika mbali kiasi gani, ukijua umepotea njia rudi kuliko kupotea jumla! Kuanza upya si ujinga. Bora uanze upya ufike salama kuliko kuendelea usifike
11. SIRI YA KUMI NA MOJA
Haijalishi umri umekwenda kiasi gani kama una ndoto kichwani amka ukaitekeleze kwa sababu umri ni namba tu na uzee hisia tu. Haijalishi mashavu yamelegea kiasi gani ukitimiza ndoto watayabusu tu.
TUWE NA WAKATI MWEMA NA BARAKA ZA MUNGU ZIKAWE NASI SOTE KWA KADRI YA FADHILA NA NEEMA ZAKE
JUMAPILI NJEMA
Na: Omar bin Labiu