Maisha kabla ya Uhuru yalikuweje?

Ntozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
226
Reaction score
300
Swali fikirishi;maisha kabla ya Uhuru yalikuweje? Kama baada ya Uhuru maisha ndiyo haya yakuhangaikasana,maji shida, ajira shida,umeme ni shida, ajira serikalini ni shida, mahitaji muhimu bei juu, soko la mazao ya mkulima siyo la uhakika,na tuko ndani ya Uhuru uliopiganiwa na mashujaa wazee wetu.sasa kabla ya Uhuru ilikuweje maisha?

Au labda Matunda ya Uhuru wanayapata wachache?Au ilitokea hulka tu kwamba mzungu asiwe kiongozi wa mtu mweusi?Bado najiuliza.
 
Story za maisha ya kipindi cha mkoloni yamejaa story nyingi za uongo uongo kuonesha waafrika tumekandamizwa na kuteswa sana na wakoloni, ila kiuhalisia Tanganyika chini ya ukoloni wa mwingereza maisha yalikua bora sana tofauti kabisa na baada ya uhuru kuanzia huduma za kijamii mpaka miundombinu.
Tungemuacha Muingereza aendelee kutawala mpaka miaka 1990 hakika tungekua mbali zaidi kimaendeleo kuliko maendeleo tuliyonayo sasa hivi miaka 60 baada ya uhuru.
Ukiangalia tu utaratibu wa mipango miji kipindi cha ukoloni unaona wazi kabisa waafrika hatukupaswa kujitawala wenyewe.
 

kuna ka ukweli ndani yake, maana hata ukisema uwaulize waliounda serikali baada ya uhuru ni kitu ambacho wamejenga au kuanziaha kikadumu kwa muda mrefu hakuna, zaidi wataonyesha shule walizoacha waingereza na wao wakapaka rangi tu,

sio shule sio hospitali wala miundombinu ya uchukuzi,

inawezekana maisha kabla ya uhuru yalikuwa na muelekeo mzuri zaidi kuliko haya ya sasa.
 
jamani Mtumwa ni mtumwa tu piga ua garagaza atabaki kuwa mtumwa tu mnatutia aibu!! pamoja na kutubania kwa sananaaa!! mabarabara yoote haya rami tupu! mpaka jikoni! migari ya kumwaga wewe tu!! uza ndizi zako, popote!

jamani mighorofa ya kumwaga! mpaka mkulima diamond anayo, kwa kuimba tu!! viwanda, shule kibao, uhuru wa kujiamlia, midege heee!! miji basi ya kisasa kuelekea mikoani, maweee niseme nini sasa! miji treni ya umeme dada? sijui nini na nini!! mweee!

sema tu watu wengine Mungu amewapiga kofi! wana damu ya kitumwa!! watabaki ivoivo tu!! kwanza kimiundo mbinu kwa miaka 50 tu ya uhuru serikali ya waingereza haitupati hapa tulipo na wamekaa humu miaka takribani 500.

ni sisitumewajengea huko makwao ulaya na america tukiwa watumwa!! kupitia sisi walineemeka ndo maana bado wana tutaka!! tusinge kuwa sisiwangekuwa maskini tu!
 
Story za vijiweni hzi. Mjerumani na Muingereza walitawala hii nchi kwa miaka 80. Mjerumani alitawala miaka 40 na Muingereza pia alitawala miaka 40. Mambo mengi yaliyofanywa na wakoloni kama kujenga shule (chache sana), barabara, reli, kilimo n.k ilikuwa ni kwa faida yao na wala haikuwa kwa ajili ya muafrika.

Ni ujinga na upunguani kudai kwamba maisha wakati wa ukoloni yalikuwa ni mazuri kuliko sasa ambapo nchi yetu ipo huru. Ukitaka kujua kwamba baada ya miaka 60 ya uhuru tumepiga hatua fuatilia kila nyanja ya maisha ya binadamu kabla ya uhuru halafu linganisha na sasa baada ya miaka 60 ndio utajua tumepiga hatua au la. Vinginevyo huu uzi utakuwa ni kijiwe cha kahawa tu.
 
Maelezo mengi katika hoja hii ni siasa sio facts,HATUKUTAWALIWA NA MWINGEREZA ,Tanganyika iliwekwa chini ya UN baada ya kukosa mkoloni!hili ni vema middle class wewe ukalielewa sio kutulisha matango,tunapata uhuru tulikua na miji iliyopimwa na kupangwa vema,services delivery zilikua top class kuanzia elimu,afya hadi uzoaji wa taka mitaani.Kitendo cha serikali ya awamu ya kwanza kwenda China kulivuruga kabisa uelekeo wa nchi yetu na kutufikisha hapa tulipo leo wakati nchi kama Singapore,Norway zimepiga hatua kubwa mno kimaendeleo,leo tunaambiwa uchumi unakua kwa 5%wakati tunaongezeka kwa 3.5%hii ni crazy.
 
Kama tungeruhusu wakoloni watutale hadi miaka ya 1980 basi tungekuwa civilized vya kutosha as a nation na haya mambo ya hovyo hovyo tusingekuwa nayo. miaka 60 ya uhuru huna maji, huna umeme - huo ni uhuru ulikuwa unamaanisha nini basi. Yaani karne hii maji ya kwa wananchi na umeme kwa matumizi yao unategemea vyanzo ambacho msingi wake ni mvua, isiponyesha kwa wakati?
 
Mambo mengi yaliyofanywa na wakoloni kama kujenga shule (chache sana), barabara, reli, kilimo n.k ilikuwa ni kwa faida yao na wala haikuwa kwa ajili ya muafrika.
sisi tumepata uhuru mwaka 1961, tumezaliwa tukakua - lakini kila kitu kizuri tunaambiwa aliacha Mjerumani ama Mwingeleza - zikiwemo shule nzuri za secondary wakati huo za kiitaifa, miundombinu pamoja na majengo ya IKULU pale Dar pamoja na Reli ya Kati ambayo ipo hoi bin taabani kwa sasa.

Ni kweli wakoloni walifanya mambo wa uchache ila kwa ubora mkubwa. ni kheri ufanye jambo kwa ubora likamilike kuliko kufanya mengi yakiwa na upungufu mkubwa, sisi hatujali quality bali tunajali quantity.

Swali je hii miaka 60 imeshapita, kuja jambo kubwa sana la kujivunia kama taifa ambalo tumelitekeleza kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kutembea kifua mbele ukiondoa hii propaganda ya umoja na mshikamano ambao kiuhalisia haupo.
 
Kwa hiyo kama waingereza hawakutawala Tanganyika walikuwa wanafanya nini hapa Tanganyika? Na kwa nini tunaita wakoloni? Unajua maana ya Koloni na maana ya kutawala wewe au unapiga porojo tu. Kwanza Kabisa Tanganyia haijawahi kuwekwa chini ya UN (United Nations) bali Legue of Nations. Ni nchi gani hapa Afrika ambapo wakoloni waliondoka na kuacha maendeleo makubwa ambayo sasa hayapo? TUACHENI KUWA WAJINGA NA KULAUMU BILA SABABU.
 
Nijibie hoja yako sio upumbavu uliouonyesha ,Tanganyika halikua koloni kama wewe unaita koloni hilo siwezi kukuzuia;UN na League of National kweli hapo kuna tofauti,au ni majina tu ndio tofauti hapo?Zimbabwe ni mfano mzuri ambao crocodiles waliiachia nchi hii na walipo kuja Lizards wakavuruga kabisa,tuliipokea nchi hii ikiwa na misingi mizuri including uhuru wa kidemokrasia wa vyama vingi,kilichofanyika ni kuua hii na nchi kupoteza uelekeo bora.
 
Wewe ndiye mpumbavu tena wa kiwango cha juu. Nimeuliza kwenye post zangu huko nyuma kwenye huu uzi kwamba je kabla ya uhuru wa Tanganyika (80 under colonial rule) hali ilikuwaje katika nyanja zote za maisha halafu linaganisha na sasa 60 years after independence hali ikoje. Inaonekana wewe dish limeyumba au ni ubishi tu wa kuzaliwa au hujui hata historia ya nchi yako (kama wewe ni mtanzania).
 
Yan hamna kitu hata ukiangalia shule za maana nyingi ni za mkoloni na za misheni, shule za ccm ndo hizi wanajenga baada ya miaka miwili sakafu ishabomoka.
 
Thinking na reasoning capacity yako ipo chini sana. Kwa hiyo hii nchi inayoitwa Tanganyika ilipopata uhuru uchumi wake ulikuwa sawa na hao waliotutawala hadi uanze kufanya comparison hiyo. Lete comparison ya maendeleo yaliyokuwepo wakati wa ukoloni na maendeleo yaliyopo sasa hapo ndio utakuwa na hoja ya kuilaumu serkali yetu au kuipongeza. SI AJABU NYIE NDIO HUWA MNASEMA HERI KUZALIWA MBWA ULAYA KULIKO KUZALIWA BINADAMU AFRIKA(TANZANIA).
 

Wewe usijibu kwa kukariri hadithi. Sema kwa Tanganyika, nini tofauti bora na hasi zilizopo kati ya maisha baada ya uhuru na wakati wa mkoloni.
Kitu gani kimebadilika kuwa chanya na kwa nani?
 
Wakati wa ukoloni uwekezaji ulikua mkubwa si Tanzania tu bali katika makoloni yote ya Afrika. Kazi zilikua nyingi sana kutokana na elimu na ujuzi wako. Kuanzia Mamlaka ya Bandari, Shirika la reli, Posta na hata mikahawa na mahoteli.

Kazi za ndani kwa ma CEO zililipa ujira wa kima cha chini na uliweza kupata mkopo wa nyumba.
 
Wrwe ni mshamba tuu kama mpaka sasa baada ya uhuru chamoto tunakiona sasa unafikiri ukoloni ungekuwaje
 
Wrwe ni mshamba tuu kama mpaka sasa baada ya uhuru chamoto tunakiona sasa unafikiri ukoloni ungekuwaje
Bora mkoloni mwingereza nchi ilikua na focus kuliko mkoloni mweusi asie na dira yoyote ya maendeleo zaidi ya kuwaza kujilimbikizia mali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…