Maisha kabla ya Uhuru yalikuweje?

Shida hapo ni hili zimwi tawala...

Na Mwalimu alikosea kidogo kuwafukuza kabisa wazungu... Angewaacha kwa masharti.. ..tungekuwa mbali!

Maana kwa uzalendo wake alijuwa tutaweza ..akasahau kwamba kuna vipanga ! Vinangoja aondoke tu...

Tuna rasilmali nyingi lakini kazi Ni kukopa tu kila uchao!
 
Bora mkoloni mwingereza nchi ilikua na focus kuliko mkoloni mweusi asie na dira yoyote ya maendeleo zaidi ya kuwaza kujilimbikizia mali.
Nani amekuambia mwingereza alikuwa na focus na maisha ya waafrika, ni kipindi baada ya nyerere viongozi wa juu kabisa wamekuwa utopolo
 
Kumtegemea mzungu katika maendeleo yaki ni kujiaminisha kuwa kichwa chako hakiwezi kupambana kulets maendeleo haya kenya inawazungu ipo wapi hali za waafrika huko kenya zipoje, zimbambwe na afrika kusini hali za waafrika zipoje
 
Wewe usijibu kwa kukariri hadithi. Sema kwa Tanganyika, nini tofauti bora na hasi zilizopo kati ya maisha baada ya uhuru na wakati wa mkoloni.
Kitu gani kimebadilika kuwa chanya na kwa nani?
Sina muda huo wa kuanza kuelezea hiyo historia tulipotoka na tulipo sasa. Hata tu kwa akili ndogo sana ya binadamu unawezaje kusema kwamba wakti wa ukoloni ni bora kuliko sasa? Mtu nakuwa na kahoja kake kamoja tena hakana mashiko basi ndio anashikilia hako tu bila kuangalia nyanja zingine za maisha. Mambo yaliyofanyika baada ya miaka 60 ya uhuru ni mengi na mazuri kuliko yaliyofanyika kwa miaka 80 ya wakati wa ukoloni. NARUDIA KUSEMA NI UPUNGUANI NA UKOSEFU WA LISHE YA AKILI KUDAI KWAMBA WAKOLONI WALIKUWA BORA ZAIDI KULIKO SISI TUNAVYOJITAWALA.
 
Huo uwekezaji unaousema wa wakaloni ndio ulikuwa unafaidisha waafrika? Wasomi wakti huo walikuwa wangapi kulinganisha na population ya watu wakati huo na je hizo ajira zilikuwa ni za namna gani?, Maofisa wa mashirika au serikali ya kikoloni au Manyampala, manamba, vibarua, kuli? Let go with statistics tuache longolongo za vijiweni. Unajua kwamba wakati Tanganyika inapata uhuru population ya watu ilikuwa around milion 9 na madaktari wa kiafrika hata kumi wlikuwa hawafiki, ma-engineer hata kumi walikuwa hawafiki achilia mbali fani nyingine kama wanasheria n.k hali ndiyo ilikuwa mbaya zaidi. Idadi ya shule za serikali za kikoloni hata kumi zilikuwa hazifiki (ukitoa za mission). Kwenye sekta ya afya tulikuwa na madktari wangapi na hospitali, vituo vya afya na zahanati ngapi? Mikoa mingapi ilikuwa na umeme na kwa kiasi gani, hali ya usafiri ilikuwaje? fuatilia takwimu ndizo zitakufanya utoe judgement ya kweli.
 
Hata kama maisha yamekuwa magumu kiasi gani tusianze kutamani maisha ya ukoloni.
Ni bora turudi tu mkuu, wenda itatustua zaidi kuliko kua na ukoloni mamboleo.
Direct colonialolism inahitajika
 
acha kufananisha wazungu na mambo ya kipuuzi, CCM ni wanyama waliokusu utu kabisa. miaka 60 wanatawala mpaka leo hata maji kuwapa wananchi wanashindwa halafu kuna watu humu wanaleta hoja za kuwakingia kifua.
 
Mwalimu aliwahi sana kuleta uhuru.

Pengine nchi ingekuwa na maendeleo zaidi. Angengoja hao wakoloni waongeze barabara, shule, hospital nk, sijaona kipya sana sana ni ada na bili kila mahali.

Endelea kupumzika huko Mbinguni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 
Ni kweli wakoloni walifanya mambo wa uchache ila kwa ubora mkubwa. ni kheri ufanye jambo kwa ubora likamilike kuliko kufanya mengi yakiwa na upungufu mkubwa, sisi hatujali quality bali tunajali quantity.
Weee!! mzee funguka!! wao wanataka Waafrica muamini kuwa wao wazungu walikuwa/na still ni bora!!.... kwa hiyo mtu km wewe ndo wanakutaka! tena wanakupa na uraia kwao kabisaaa!!

Sisi Africans ni bora, tuna kitu usicho kijua ndo maana walitununua kwa karne nne mfululizo! Tangu enzi za Pharaos' wa Misri!!... mengi wametoa kwetu! ila hawataki ujue ulivo bora? wala kuona tuna panda!! wameweka mikakati ya kutudunisha! kwa njia ya nini cha kutupatia, wapi! lini, kwa nini! yote ni ili tusiwe juu tena!

km Rais wa kiafrica ukijifanya mjanja hutaki kujikomba kwao!! basi jua kabisa zako zinahesabika! wanakuua kwa vyovyote vile! mifano ni mingi ya viongozi wenye msimamo walio uawa! kwa kukataa, kujikomba kwao! Lumumba, jiwe, nkrumah, kwa uchache!

Well!! unataka kujenga miundo mbinu! Utaalamu wa Ramani, Malighafi, vifaa,nk, ukanunue kwa adui yako/ mkoloni? Gabachori?! ili uendelee kuliko yeye! akijua kabisa weye ndo uliye mpa hizo nguvu?? unadhani watakupa ili uwe bora? hujiulizi swali dogo hili???

Hata ukijifanya eti kutengeneza vya kwako ndo utaona moto wa blue!!...........na masimango meengi mara huna hati miliki, hii ume copy tulipe hutaki tunakuja kukuchapa!! mfano Gadafi aliuawa sababu ya kuimarisha maisha bora tu, ya walibya. hili pia huoni???????

Kumbuka ule ubora unaodhani walifanya ni kwa faida zao!! na watu wao!! hizo reli zilienda hadi mashamba ya mikonge ndani huko!!! ajili ya Kuboresha maisha ya watu wa Ulaya........ hatawalipo waachia walijua zitakufa!....wazee wetu wamejitahidi miundo mbinu hiyo ipo mpaka leo!

Jambo hili la kudumisha mabaki yao,mpakaleo yanatumika kwa ubora japo choka mbaya wenzako limewaacha midomo wazi, wazungu mpaka kesho..... mfano, Mv victoria, liemba, LOPISO ni Meli ya karne ya kumi na saba mto kongo inapiga kazi mpaka kesho!

Ikulu yetu, Bomani zetu, Maghala ya kikoloni, Musoma Hotel, Tabora Hotel nzuriiii! vimetunzwa mpaka kesho yana kula mzigo mpka kesho hayo hapo...........Tizama inavyo pendeza....

Wao sasa Ikulu ya Pharaoh kule Misri, Mijengo ya mfalme suleiman, Hekalu la Jerusalem, Golgotha!!. tumbuktu, Gomba zomba state house nk... wao walivo na mkono wa uharibifu waliharibu vyote dakika sifuri!! mpaka leo yamebaki magofu!!

Siri waliyo nayo ni hivi leo wanatamani kujifunza kutoka kwa Africans!!! kuhusu utunzaji wa Mali, ili zidumu, ila hujui tu!!

Mie huwaga nasema hivi!! Miafrica mmerogwa saaaaana hamjielewi!! na bila wewe mwenyewe kujitibu hkn dawa!...... utajitibuje sasa hapoooo ndo kazi ilipo........
 
Na Mwalimu alikosea kidogo kuwafukuza kabisa wazungu... Angewaacha kwa masharti.. ..tungekuwa mbali!
Mwalimu alikuwa sahihi kabisa! kuwafukuza wazungu sababu alijua bado wanatuhitaji watakuja tu!.......aNgalia leo ni miaka 60 tu tangu tupate uhuru!! Tuna Mijengo ya serikali mikali ya kufa mtu km twin tower! NIC,

Mavyuo vikuu ya sirikali mangapi? mengi tu, angalia viwanja vya ndege vya kimataifa, tunavuna tu, isingekuwa vita ya kagera na kusaidia ndugu zetu wa kusini tungekuwa mbali mno!


Barabara kila mkoa tumeunganisha kwa Lami ya kisasa! reli zipo zilezile hazijafa! Viwanda vingi tulivuna !! but vilikufa kibudu kwa ujinga tu wa mtu mweusi! wenye akili km zako eti aliwawaisha kuondoka! NHC nchi nzima mlipata kwa bei Rahisi sana mpaka leo mnaishi!

unataka nini?? sema tu Mungu ukoo wenu kawapiga kofi!! unamlalamikia Nyerere!! wao hao wazungu miaka 200 waliishi humu wamefanya nini km sisi weusi??? acha izo bana!!!

wewe kwanza muongo sana hujui Nyerere hakuwafukuza wazungu wote wengi tu walibaki aliowafukuza ni wale hatari kwa nchi ikiwa ni pamoja na Rais!! wao wakatangazia Dunia wamefukuzwa wote! na wewe ukakariri ivo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…