wewe uliamua hutashiriki 'other people's show'
ulishiriki your own show
na sasa huna regrets
thanks The Boss kwa hii makitu umedrop kha! unamkuta mtu alifundishwa na wazazi kuwa ukiolewa NO divorce, ukiachika tu ni laana na mikosi na maisha yatavurugika! mtu anavumiliaaa weeee anapigwa, ananyanyaswa kwa namna moja au nyingine , yaani its full inhuman acts in her/his life but yupo tu just bcoz of the word CURSE! but nimeona wengi walijitoa kwenye mikono hiyo dhalimu na kuja kuwa mifano kwa x's wao popote wawaonapo.
ndivyo tunavyotakiwa kuifanyia hii nchi, ni muda sasa tuseme basi na CCM, itupe talaka yetu na tutafute MUME/CHAMA kingine kitakachotukomboa. hii dhana ya kikija chama kikingine kutatokea matatizo ife, AND LET IT BEGGIN WITH US! life is not how it is from stories and other pipos aspects, but it is how u take it with your DOTS.........! in short MAISHA YAMEJAA KUCHAGUA NA MUDA ALWAYS HAUTUSUBIRI!!
mkuu The Boss,ninachojua mimi maisha ni sinema,we are actors katika a big show ambayo mwanzo na mwisho wake hatujui,uwe Bill Gates,uwe matonya,uwe Obama ,uwe Kikwete,uwe invisible uwe bishanga, duniani humu wote tunacheza makida tu.................anyway death is the greatest equaliser.
Nakubaliana na wewe kiasi lakini hebu tusifikirie kizungu sana lets think kwa kujiweka kwenye position ya watanzania wengi..hasa ukizingatia nchi yetu nayo inacheza show za nchi zingine(developed countries)..watu wengi waliopo vijijini ni maskini kuliko mijini kwa sababu wengi hawajacheza show za wenzao(hawana elimu,kazi) na wenye elimu wengi wamekimbilia mijini kucheza show za watu na zimekua msingi wa mafanikio yao!kwa maisha ya kitanzania ni ngumu sana(japo inawezekana) kustand on your own bila kua na msingi(fedha,elimu) labda kama una special talent!
Hivi bila kua na resources( elimu, fedha au special talent) unawezaje kucheza show za maisha ya kitanzania on your own??
exactly my point
hata wazazi wanaweza kukufanya uwe 'victim' of their show
hawakupi uhuru wa kuchaagua na kufanya mistakes zako mwenyewe..
mfano wapo wanaochaguliwa nini wasome...mfano baba dokta analazimisha mtoto awe dokta
tena hili la wazazi kukupangia cha kusoma lilikuwa linanikera sana.
Nililzimishwa kwenda PCM wakati nachukia kemia kama nini, uzuri nilikuwa mbishi na kukataa.
Na chuo nako nikachaguliwa kozi lol
haikufanikiwa maana nilikataa
hapo ndo unakuta mtu anashindwa shule kumbe anasoma kitu ambacho hapendi au hana uwezo nacho.
she is a housewife now
Na kwa mujibu wa hii 'theory' yako na yeye yuko kwen 'top three' ya BSS sio....LOL
nimeipenda hii mada ila sina mchango nahisi ni kwa watu wenye akili tu,mie niliyebakiza za kuvukia barabara hapa ni parefu....:loco::loco: