Mshuza2
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 11,261
- 17,202
Jamani huko mliko nyie wenzangu vipi? Huku naona kama kipa katoka, ngoma ngumu sana! Ile milo mitatu kwa siku imekua kwa mbinde sana, hebu fikiria yale mahitaji muhimu ya mwanadamu bado kwetu ni tatizo.
Hatuli vizuri, hatuvai vizuri, na mbaya zaidi hatulali pazuri. Kuna kundi kubwa la watu wanarudisha mpira kwa kipa (wanarudi kijijini), mijini hakukaliki, kila siku afadhali ya jana!
Biashara haziendi, mikopo hailipiki madeni kila kona, stress tupu. Hivi kwa hali hii nguvu za kiume zinatoka wapi? Usiku usingizi hauji ni kuwaza tu, hata hamu ya kula Chakula cha usiku" utaitoa wapi? Barabarani unapishana na mtu anaongea peke yake.
Hebu tupeane mbinu wakuu, wale wanaokesha kitambaa cheupe na kule bandarini kila siku meli zinaleta magari wanafanyaje? Yaani kama adhabu kumbe ndio maisha yenyewe.