MAISHA MTAANI NI MAGUMU

MAISHA MTAANI NI MAGUMU

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Bro, Maisha mtaani ni magumu.
Ukisikia ni magumu unaelewa, moja haikai mbili haisimami. Mbele hauendi, nyuma hakurudiki. Hauoni future.!
Ni kama matumaini nayo yamekata tamaa.

Unajaribu namna zote za kujikwamua ambazo zinatajwa na kijana wa karne ya 21 lakini wapi.... Unabeti mikeka inachanika,
Degree yako haikusaidii kitu ni sawa na muhuni mmoja tu ambaye hajui hata shuleni huwa kunafundishwa nini.

Unamuona muhuni katoboa anaishi vizuri, ukimkaribia vizuri unaona ni kama ana "kete" flani hivi anauza,
"Oya nipe huo mchongo mwanangu", unajaribu na wewe kuuza ngada.

Siku ya kwanza unajaribu, ndio arobaini yako, mapongo wanawafuma, unaswekwa lumande.
Dhamana yako ni mkopo aliouchukua Bi.Mkubwa kwa kuweka rehani ki-biashara chake cha genge.

Mwamba aliyewakopesha ameshakudhamini mara kadhaa kwenye mikopo ya riba ya "Kausha Damu" mtaani kwenu ulipokosa hela ya kumtoa wife hospital mlipopata first born wenu.

Sio janga hilo tu...
Kila duka la mangi pale mtaani kwenu ni madeni ambayo hayana uhakika wa kulipwa, hakuna hata mwenye hamu ya kukukopesha kibaba cha unga.

Mwezi wa tatu sasa unakimbizana na maafisa wa OYA ulipochukua mkopo kufanya mtaji wa Forex, baada ya kuwa umepoteza hela nyingi kwenye Crypto currency.

Ma-bro wako kadhaa uliowashawishi mjichange mfanye trading ya crypto na mkaishia "kupigwa" na mentor wenu aliyewachomesha kwa broker feki, wanakuona wewe ndo chanzo cha kuliwa hela zao wanataka uzirudishe.

Wahuni mtaani wanakuwinda kwa bisibisi, ni ama urudishe hela zao au upoteze maisha. Kausha damu, Finca, Vicoba, mchezo wa hisa na kwa mwenye nyumba, kote unadaiwa.

Alafu huu mchezo wa kuchukua mkopo kulipa mkopo mwingine sio unyama wala nini...

Ukijaribu kujumlisha jumla ya mikopo yote mikubwa ni kama milioni 30 ambazo hata ulichofanyia hakionekani, hachana na madeni madogo madogo ya kukopa bumunda kwa mangi mwanao mdogo asife njaa.

Baby mama wako anakuona hauna future yeyote kwa sababu hata zawadi ya kibangili kwenye birthday ya mtoto wenu hauwezi kuilipia, anakupiga chini.

Unabaki na mama yako mzazi tu ambaye anakulisha kwa biashara yake ya genge nalo mtaji umeisha kwa kukudhamini unapodaiwa na kila anayekuona.

Huna hili wala lile, hauna mbele, hauna nyuma.
Unadokoa hata vijisenti vya Bi.Mkubwa wako unasukia mikeka ambayo hata muhindi hacheki na wowote.
Hata ukiotea mkeka muhuni anakupora.!
Ni kama Dunia nzima iko kinyume na wewe.!

Katika njia panda unapotarajia walau kifo ndo kiwe rafiki yako wa pekee, anakuja mhuni mwingine kukuharibia kabisa siku, ikiwezekana hata kaburini nako usipumzike.

Jamaa hujawahi kumuona kabisa, lakini yeye ana taarifa zako zote, hata ambazo unahisi ni siri yako peke yako...

Mwana yuko smart, suti kali, kiatu cha bei mbaya, mkoba wake umejaa mpunga usiotambulika idadi mpaka kwa msaada wa vikokotozi.
Huyu ni nani sasa.!?

Kabla hata hujamuuliza anakwambia vile alivyokuona una masononeko, ni kama vile hauna hela ya kula au mishe haziendi, hauelewi maelekezo.!
Alafu ni kweli.!

Anakupanga...
"Sasa sikia mwanangu, hapa Duniani hakuna hela ya bure, mimi nataka nikupe hela ya kula ila lazima uifanyie kazi, unasemaje.!?"

Kwa bashasha kabisa unakubali
"Oya hizi ndo vitu zangu, nimekuwa nikitafuta kazi kwa muda sasa sijapata, nipe hilo dili mwanangu"
Ni kama umepata mkombozi.

Dili ni simple tu...
Tunacheza mchezo– wowote hata wa kurusha shilingi, unachagua kichwa au mnyama– ukishinda nakupa 5000, nikishinda mimi nakupiga kibao kimoja shavuni.

Yaani kibao kimoja kwa buku 5.!? Hii hainishindi mzee hata tukienda round 20 sikosi kula hata round 5, twende kazi.

Mnacheza mchezo, unashinda round kadhaa na yeye anakutandika vibao round ulizoshindwa, baada ya kupata kama buku 30 hivi anakwambia kwa leo inatosha, hiyo itakusogeza siku mbili tatu.

Mnakubaliana poa sio mbaya, lakini unapenda mjuane zaidi kwa ajili ya mchezo mwingine kama atakuwa na muda siku nyingine.
Kabla hajakupa dili la mchezo kwa siku nyingine...

Anaanza kukutajia kila deni ulilonalo, kila kosa la jinai na lisilo la jinai ambalo uliwahi kulifanya, anajua umefukuzwa kazi, anaijua familia yako– mke aliyekubwaga na mtoto wenu mdogo uliyekosa zawadi ya kumpa siku ya kuzaliwa kwake. Mama yako na baadhi ya watu wengine wanaokujua na kukudai.

"Wewe ni yupi asee.!?"
"Tulia, ukitaka kunijua nitakwambia, na ninakuhakikishia kukusaidia kulipa madeni yako yote uwe huru Duniani kama wengine, uachane na maisha ya kutangatanga kama hivi"

Kwa kuwa bro amekuja na taarifa zako zote ni kama vile anakujua miaka 10 iliyopita, mmecheza mchezo rahisi wa kuchapwa vibao na umepata hela ya kukusogeza wiki nzima, unamuamini mazima.

Sharti la kukulipia madeni yote ni kucheza mchezo ambao utashinda hela nyingi sana za kuweza kulipa madeni yako yote na kiasi kingine kikabaki cha kumwaga.

Sasa rasmi unamuomba mawasiliano ya kukutana siku nyingine ikiwezekana ukacheze mchezo wa kukufutia madeni yako yote na kupata kipato cha kukuweka huru kwenye hii Dunia ambayo umeikatia tamaa.

Mchezo wenyewe ni SQUID GAME, huko unakwenda kukutana na ma-bro, mabinti, makamo, na wazee waliojikatia tamaa na maisha, wenye madeni hata kuliko wewe...

Wote mnacheza kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, wengine hofu ya kifo wameshaizika tangu walipozika watu wao wa karibu, hawana cha kupoteza kwenye maisha.

Kwa hiyo mnacheza kutafuta hela, kwa sababu mtaani mambo hayako upande wenu.
Lakini nyuma ya pazia ya huu mchezo ni nini.!?
Hakuna anayejua.

Embu anzeni kucheza mengine mtayajua huko mbele kwa mbele. Mchezo ni SQUID GAME.

Season 1 ina vipande 9 imetoka 2021,
Season 2 ina vipande 7 imetoka 2024,
Enjoy, mimi ni Magical power
1736497654614.jpg
 
Mkuu uhalisia wa Squid game tunapitia vijana wengi wa kiafrika sio Tanzania pekee wala Nigeria. Wengi tunajaribu kupitia njia za panya kikubwa tutoboe tu

Kikubwa ni kukaza maisha mazuri hayaji kama ndoto
Kabisa mkuu 👏🏽
 
Mkuu uhalisia wa Squid game tunapitia vijana wengi wa kiafrika sio Tanzania pekee wala Nigeria. Wengi tunajaribu kupitia njia za panya kikubwa tutoboe tu

Kikubwa ni kukaza maisha mazuri hayaji kama ndoto
Pongezi kwa Mama amesababisha sasa hivi vijana wote wamepata ajira na ile mikopo ya Halmashauri vijana wote wamepata, pongezi sana kwa Mama
 
Kabisa mkuu 👏🏽
Sasa hivi Mama anaupiga mwingi hakuna kijana asiekua na ajira wote vijana wote wameajiriwa na wale wanaohitaji mikopo kwenye Halmashauri masharti ni nafuu kwa sasa kwaa hio vijana wengi wamepata mikopo ya Halmashauri, makofi mengi kwa Mama
 
Sasa hivi Mama anaupiga mwingi hakuna kijana asiekua na ajira wote vijana wote wameajiriwa na wale wanaohitaji mikopo kwenye Halmashauri masharti ni nafuu kwa sasa kwaa hio vijana wengi wamepata mikopo ya Halmashauri, makofi mengi kwa Mama
Usitake kunigombanisha Siri Kali yangu mkuu 😂😂
 
Sasa hivi Mama anaupiga mwingi hakuna kijana asiekua na ajira wote vijana wote wameajiriwa na wale wanaohitaji mikopo kwenye Halmashauri masharti ni nafuu kwa sasa kwaa hio vijana wengi wamepata mikopo ya Halmashauri, makofi mengi kwa Mama
Kuwa specific mkuu makofi yapi? Maana unatuchanganya 🤣🤣.
Makofi haya haya aliyopigwa mwanetu au yale ya " clap hands for..."
 
Back
Top Bottom