Maisha na Chuki

Hii hali ipo, ila watu kamwe hawawezi kukupa uthibitisho watakuona unajikweza so jua tu kuna kitu ndani yako kinachofanya wakuchukie. Na itakua hivyo maisha yako yote
 
Mara nyingi sana riziki huwa ndio mwanzo wa chuki. Wala isikupe shida hali hii. Kitu cha msingi wewe ni kutenda HAKI na kuishi vile inavyopaswa siyo vile ambavyo watu wanataka.

Aidha, binadamu yoyote yule aliyekamilika sawa sawa kabisa ni LAZIMA awe na maadui pamoja na marafiki.

But all in all, kukataliwa na Waovu au mashetani kwangu Mimi binafsi naona ni FAIDA, kwa sababu naepushwa na Mabalaa. Waovu yao ni mabalaa!
 
Unakuta wapuuzi wanamvimbia mtu ukiwauilza kakufanya nini Jibu lake utaskia jamaa hasilimii watu yule, Sasa wewe usiposalimiwa unapungukiwa na nini? Dume zima kabisa linaongea maneno kama hayo
 
Neno chuki/hate ni baya sana. Unakaaje unamchukia mtu hata uwe na sababu nini kinakufanya umchukie? Je unakua na amani umchukiapo mtu? Binafsi naona wanaume wengi hatuna hiyo roho ya kuchukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…