Leo nimepokea kwa masikitiko habari za kufulia kwa mkaka niliyewahi kuwa nae kwenye uhusiano kwa mda wa miaka 3. Nasikia amefulia ameuza kila alichokua nacho amebaki na komwe lake tu. Huyu kaka lininyanyasa sana kipindi ana vijipesa mi nikiwa kajamba nani. Alininyanyasa kisaikolojia kuna baadhi ya vitu nikikumbuka hadi leo nakua mnyonge.
Kuna siku nilimnunulia zawadi akaniuliza bei ya zawadi nilivyomwambia bei yake akanijibu i dont use cheap things keep it for yourself 🥲
Siku anaachana na mimi akaniambia relationship yetu illkuwa just for fun nothing was serious and it wasnt even a relationship it was a situationship 🥲 kumbuka hapo wakati anaongea haya tulikuwa pamoja kwa miaka 3. Halafu akaongeza nimekua nakuonesha signs zote za kutotaka kuendelea kuwa nawe lakini bado ukaendelea kuniganda. Naomba kuanzia leo usinitafute kwa namna yoyote ile its over!!
Katika maisha yangu yote hakuna kipindi moyo uliniuma kama siku ambayo alinitamkia maneno haya. Mungu si asumani sasa ivi amepigika maisha yanamnyoosha tu. Licha ya mambo yote aliyonifanyia nimesikitika sana. Mwanga wa Mungu umuangazie arudi katika hali yake ya zamani. Tuweni humble jamani maisha ndo haya haya tuache kudharau watu katika maisha haijalishi ni maisha ya kimapenzi au kikazi , hakuna mtu anayeijua kesho yake.
NB: Roby nitafute nikupe mchongo mi sina roho mbaya kama yako!