Umewahi kusikia msemo wa kiswahili unaosema “Wema hauozi?”. Inawezekana umesikia lakini inakuwa vigumu kuamini na kubaki kujiulizau maswali mengi kwamba unawezaje wema kutokuoza?. Bila mifano halisi kama huu ambao leo tunakwenda kuutafakari,msemo huo wa wema hauozi inaweza kubaki kuwa nadharia ya kufikirika tu.
Katika matukio ya kusisimua ya hivi karibuni yanayodhihirisha usemi huo kwa vitendo, basi miongoni mwa hayo matukio ni kisa cha kuvutia kilichotokea nchini Zambia hivi karibuni, ambapo Raisi mpya wa nchi hiyo Hakainde Hechilema amemteua bwana Kuyomba Bwalya kuwa mkuumpya wa magereza nchini Zambia.
Karibu tena msomaji wetu katika mtandao wetu wa maishanifursa. Leo tutajikita katika mada ambayo nimeipa kichwa “WEMA WAMPA UKUU WA IDARA YA MAGEREZA” Nakushukuru sana kwa kuendelea kufuatilia kazi zetu uwepo wako ni muhimu sana kwa kazi yetu kwani bila wewe kazi yetu haina maana.
“Kamishina Bwalya ni kijana mdogo ambaye tulikutana katika mazingira ya namna hiyo alikuwa bosi wangu. Katika mazingira magumu tuliyokuwa tunapitia bado alijaribu kwa weledi mkubwa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma na sheria” mwisho wa kunukuu. Hayo ni maneno ya raisi Hakainde Hechilema aliyoyatamka wakati akihutubia kwenye hafla ya kumwapisha Kuyomba Bwalya kuwa mkuu mpya wa magereza nchini humo.
Ilikuwa hivi: mwaka 2017 kiongozi huyo wa zamani wa kambi ya upinzani wa nchini Zambia ambaye ni bilionea aliswekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi 4 kabla ya kesi yake kufutwa na mkurugenzio wa mashtaka nchini Zambia, baada ya upande wa mshtaka kushindwa kutoa ushahidi kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanamkabili Hakainde Hechilema.
Karibu miaka minne baadaye Kuyomba Bwalya Mungu anamlipa kuwa mtu mkuu mwenye jukumu la kusimamia idara muhimu ya magereza nchini Zambia. Hapa kuna somo kubwa sana ambalo binadamu wote tunapaswa kujifunza ili kuitendea haki dunia na jamii tunamoishi.
Katika mazingira yoyote Mungu akikupa nafasi ya kutumika mahali popote tumika kwa weledi,uaminifu na kuzingatia misingi ya usawa. Haijalishi wewe ni kiongozi wa familia,taasisi,idara au kitngo chochote kinachohusiana na masilahi ya watu tenda tema tenda zako tena usingoje shukrani.
Mifano ya namna hii ibo mingi duniani, lakini swali la kujiulizau ni nani alikuwa anajua kuwa mtu ambaye alikuwa chini ya uangalizi wake wakati akiwa mahabusu,leo hii mtu huyo huyo anatumika kumwinua kuwa mkuu wa idara nyeti kama magereza nchi nzima?
Maisha ni fursa binadamu tunalo jukumu la msingi kuhakikisha kila nafasi tunayopata,kila mahali tutakapokuwa,kila watu tutakaokutana nao kuhakikisha tunawetendea jinsi ambavyo na sisi tungetamani watu watutendee katika maisha yetu. Hebu tuishi kwa kuongeza thamani na kugusa maisha ya watu wengine.
Naamini utakuwa umepata kitu kupitia makala hii fupi. Ukiwa na uhitaji wowote au ushauri katika eneo lolote la kuboresha maisha,biashara yako au hata una wazo kuanzish kitu fulani lakini unakwama;usisite kuwasiliana nasi kupitia njia za mawasiliano hapo chini. Aidha kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno, whatsapp kupiga simu au kututumia barua pepe nasi tutarudi kwako mapema iwezekanavyo.Tutashukuru kama watakaotutafuta wakiwa ni wale ambao kweli wanamaanisha.

Upvote
0