Mchumiajuone, kumiliki simu janja wewe umeona ni kitu cha ajabu sana kiasi kwamba inaweza kunifanya nisijue napata wapi pesa ya kula mchana?
Simu janja wanamiliki mpaka mateja, sembuse mimi mwenye akili zangu timamu.
Kuunga kifurushi, au kutokuunga kifurushi sio hoja mkuu huwa najiunga kifurushi cha internet tu cha mwezi, unasemaje? Unataka nijiunge cha masaa 24, au unataka kujua hicho kifurushi ni cha Tsh ngapi?
Usiniambie kuwa hujui faida ya kutumia mitandao ya kijamii, ndio maana hata wewe upo humu, na mimi mwenye hali ngumu nipo najichanganya kimawazo na wenzangu, lakini natafuta fursa.
Labda naona wewe mzee ni mboga saba hujui tafsiri ya hali ngumu. Ulitaka mimi nimiliki nini?
Ulitaka nianze kutembeza bakuli kama wale omba omba, bibi na babu zangu wa pale Kariakoo, hapo ndio uamini kuwa nina hali ngumu?
Kijana usipende kutochokoza watu ambao tunapitia machungu ya maisha, ungekuwa karibu yangu ningekuchapa vibao!