SoC02 Maisha ni mfumo

Stories of Change - 2022 Competition

Sekela peter

New Member
Joined
Sep 22, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Kila kitu kimewekwa katika jamii yetu kwaajili ya kitu Fulani. Unatembea barabarani, unatupa chupa, muda huo huo Kuna mtu Kama wewe anategemea chupa iyo iyo unayoangusha kwa kudhamiria au kwa kutokudhamiria ili aweze kupata ridhiki ata kupata hela kidogo ili aweze kujikimu.

Jalajala ambalo Mimi naogopa kupita karibu nalo Kuna mtu Kama Mimi ambae anatafuta ridhiki kupitia sehemu hio, je hili halipo kwenye jamii? Lipo na bado linaendelea kuwepo kwa jinsi maisha yanavyoenda.

Ukiangusha hela yako,ambayo labda ulikuwa umejitahidi Sana kuitunza na huwezi kuwa nayo Tena,ishapotea utajilaumu Sana kwanini imepotea na wewe utapataje pesa nyingine lakini muda huo huo mtu mwingine ameweza kuiokota iyo na ikamsaidia katika baadhi shida alizokuwa nazo au ukimpata msamaria mwema atakupa pesa yako,ndo jinsi ilivyo,ndo maisha yalivyo.

Na kila tunapopita, tunaweza tukakutana na tusishirikiane kwa chochote na imekuwa vigumu Sana kwa jamii kushirikiana katika matukio mbalimbali kwa sababu ya jinsi maisha yalivyo Ila atakama kila mtu anajali shughuli zake tu na tupo na Hali tofauti, je, hatuwezi kushirikiana kuweza kutoa ata michango midogo midogo ili kuweza kusaidia wale wenye uhitaji, kila mtu ana uwezekano wa kukusaidia mtu mwingine kwa namna moja au nyingine Ila tu huwa tunangoja kundi fulani la watu ambao hujitolea kila siku waweze kufanya hilo wakati linaweza kufanyika na makundi mengi kutoa msaada au hata ushauri lakini kwa mfumo wa maisha unavyoendelea inakuwa vigumu Sana kwa sisi Kama wanajamii kusaidiana,je tutaweza kusaidia wengine?

Elimu, Tunaona kuwa elimu ni neno dogo Sana lakini linaweza kuzaa matunda na kumpa mtu uelewa wa kuweza kujua na kutambua Kama akifanya hichi atafikwa na hili, Ivo Kama akiamua kufanya kitu ambacho kitamuathiri apo itakuwa tayari ni maamuzi ya mtu baada ya kupata iyo elimu. Hatakama kila mtu anapambania maisha yake Ni muhimu pia kuweza kuwasaidia ata wale ambao hawapati elimu yoyote kuweza kuwasaidia kwasababu sio kila mtu ana huo uwezo.

Maendeleo ya sisi na jamii yetu pamoja na vizazi vijavyo mbele yetu inatutegemea sisi tuliopo muda huu ili kuweza kuweka njia kwa ajili ya wale wanaokuja baada yetu au ya wale wanaotutegemea, je, adi Sasa unatarajia kizazi chako kitakuwa katika hali gani? Au je, una mwanga juu ya maisha yako au wale wanaokuzunguka?

Wewe ukaamua ushiriki katika Mambo ya kujiendeleza au kuendeleza jamii lazima Kuna watu watanufaika kutoka kwako, kutoka kwangu.

Usisite kuomba msaada wa kimawazo au hata kimahitaji na wewe pia usiogope kusaidia wengine

MAISHA NI MFUMO, tuishi.
 
Upvote 0
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…