Maisha: Ni mitihani gani au changamoto zipi ulizokumbana nazo maishani mwako na kuzikubali na kuamua uishi nazo ili maisha yaendelee?

Maisha: Ni mitihani gani au changamoto zipi ulizokumbana nazo maishani mwako na kuzikubali na kuamua uishi nazo ili maisha yaendelee?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za asubuhi waungwana wa humu jamvini......

Hakika maisha ni safari ndefu sana na wakati mwingine kwenye maisha tunakumbana na changamoto na mitihani mbali mbali.......

Kuna baadhi ya changamoto na mitihani tunazikabili na kuzipatia ufumbuzi na kuendelea na maisha na kuna zingine kwa bahati mbaya zinatushinda na kukosa ufumbuzi wake na kubakia fumbo maishani mwetu........

Wakati mwingine maisha hayakupi unachotaka na mambo hayaendi kama ulivyotarajia hivyo kupelekea mambo kwenda mrama na misongo ya mawazo inayogonga vichwa vyetu.......

Najua kuwa kila mmoja wetu mwenye utimamu wa akili kwenye harakati za kupambania maisha kwa namna moja au nyingine ameshakumbana na mambo mbali naengine katika amekubali kushindwa na kumuachi Mungu huku akiendelea na maisha.......

Hivyo basi nawakaribisha jukwaani Wana jamvi ili kuweza kushare nasi baadhi ya matukio au mambo ili kupeana matunzo , kutiana moyo na matumaini kwenye mioyo iliyokufa ingali inaishi kwenye dunia iliyojaa fujo......

Nawasilisha......
 
Niliwahi kupata mtihani wa kidonda ndugu miaka kadhaa nyuma......

Kile kidonda kilichagua kukaa kwenye kalio la kushoto kwa chini na kilichimbika hasa ambapo kilikuja mfano wa jipu.....

Nilipambana na hali hiyo kwa miaka mitatu bila mafanikio ya kudumu huku uchumi wangu ukididimia maana nililazimika kulazwa mara kadhaa na mimi ndio mpambanaji ninayetegemewa......

Nilivyoona nimepata nafuu ya kuniwezesha kufanya shughuli zangu nikaachana na matibabu huku kidonda kikiendelea kutoa maji maji..... hivyo kulazimika kubandika nguo au pampasi kubwa ili kujistiri......niliishi kwa miaka mitatu mpaka nilipofanikiwa kupata tiba ya kudumu mpaka leo.......

Lakini tiba ilikuja kwa kubahatisha baada ya mimi kuikubali hali kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa na mimi Hali yangu duni
 
Changamoto tunazo na tunaishi nazo,,, zangu na familia yangu sizisemi siku zikinikaba naenda kwenye makaburi ya wazazi wangu wamezikwa pamoja wapendanao nalia nagalagala hapo huku nikishushia Kili zangu nikitoka hapo naenda kwa mume wangu maisha yanaendelea .
 
Maisha ni kitu cha ajabu sana. Kwenye maisha kuna mengi mengi munooooo. Wakati wengine wanalia na kuumia kwa uchungu wengine wanafurahi na kuchekelea kuishi.Unaamka asubuhi unapatwa na msiba mzitoooo wa kuuma sana, unaona kama kesho haitafika... lakini maisha yataendelea tu.. kikubwa kubali hali. Unajikuta una gonjwa la kukutesaaa... jikaze kubali ni maisha. Unazaliwa kilema.. unajiona hukustahili kuishi..NO. jikubali. Unasoma na kuwa kinara darasani... ukija uraiani unakosa ajira halafu yule mbumbumbu anapata ajira tamu sana inaumaaa sio wivu... hayo ndiyo maisha. Kumbuka kadri unavyoongeza siku za kuishi ndivyo changamoto na raha zinavyoongezeka kwako!
Kikubwa songa mbele, pambana na usikate tamaa. ISHI
 
Changamoto tunazo na tunaishi nazo,,, zangu na familia yangu sizisemi siku zikinikaba naenda kwenye makaburi ya wazazi wangu wamezikwa pamoja wapendanao nalia nagalagala hapo huku nikishushia Kili zangu nikitoka hapo naenda kwa mume wangu maisha yanaendelea .
Kwenye kila chumba chenu specially for migegedo na mziki juu 😜
 
Kuwa domo zege nankuwa na kibamia...imebidi nikubaliane nanhali halisi aisee
 
Back
Top Bottom