Msaga_sumu
JF-Expert Member
- Aug 31, 2022
- 289
- 291
Kumekuwa na msemo mmoja mali utaipata shambani,, siju moja nilikua katika safari ya kikazi japo ni kazi ya muda hapo mkoani geita,, wale wenyeji wa geita mnaelewa unakuta kikosta (daladala) kina makonda zaidi ya sita wapiga debe 6 kuna mzee akasema mnatupotezea mda shida vijana wamejazana hapa uvivu wa kwenda shamba kulima,, nikajiuliza huenda kilimo kina tija kuliko kuvizia 1000 1000 za abiria mijini,,, mimi ni muhitimu chuo kikuu shahada ya uhasibu na IT, ninandugu wengi sana wenye hela na maconnection kibao lakn kama unavojua wabongo connection bila magoti ni kujitekenya na kucheka wazazi wangu wanamaisha ya kawaida tu huko vijijini mkoa wa kagera,,, nimekaa mjini nikihustle hapa na pale ndio nilipata kazi kwenye microfinance na badae auditing firm niliopo mpaka sasa shida ni malupulupu aseh maboss wengi wanakuajili ili kesho uendelee fanya kazi mapato hayaendani kabisa na mahitaji pesa unalipia kodi, chakula na mahitaji madogo inabaki kadhaa ya kucheza vikoba imekwisha,,, wakuu najua mnauzoefu na mitaa nimewaza nitimkie zangu kijijini nikaanze kilimo ufugaji na biashara ndogondogo kama miamala, consultations mbalimbali na electronic services, uuzaji wa nguo za mitumba, na kuuza vifaa vya umeme na simu kwa order, ila nipo na saloon kule na kiglossery cha bia moja mbili pia,,, vinaendeshwa mdogomdogo nataka nikashike mwenyewe,, najiuliza kama litakua chaguo bora kwangu kwani sioni manufaa ya kubaki mjini na kuendelea tumikia utajiri wa maboss wa jiji,,,,, pia mama yangu amekua akinishawishi kuacha kazi hizi mjini na kwenda kupambana na fursa za kijijini,,,,,, maeneo yapo frame zipo pia na mtaji wa kufanya yote haya yapo ila bado natafakari,,, nahitaji ushauri wenu wakuu katika machaguo hayo....