Maisha nikutu gani hasa?

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,903
Reaction score
1,979
Heshima mbele wakuu wangu.

Nimekuwa nikijiuliza swali hili mara nyingi bila kupata majibu. Nini hasa maana ya maisha? Tunapo sema binadamu "UHAI" umemtoka na hana maisha tunamaanisha nini hasa?

"MAISHA" ninini?

Naomba kuwasilisha.

CC Rutashubanyuma Nyani Ngabu Kiranga JingalaFalsafa gfsonwin Roulette AshaDii na wengine wote.
Karibuni kwa mjadala wana Jf wote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Kima Mchanga, hii mambo ni tata sana kwa kila mtu! Hivyo ni wazi kila mtu anaweza kutoa tafsiri yake vile alivyoguswa na dhana nzima ya Maisha, na zote zikawa sahihi ama laa! Wapo watakaotafsiri kwa kuangalia chimbuko/asili, wengine experiences na wengine matokeo yake! Na wote utakuta wanazo hoja za msingi!
Binafsi ninaamini hivi... Zao la kuishi kwangu ndio kitwacho maisha, zao la uhai wangu ndio maisha. Hivyo asili ya maisha ni uwepo wa binadamu na anayofungamana nayo! Sasa katika kuishi kwake mwanadamu kuna mambo mawili, aidha AFURAHIE au AUMIE. Matokeo ya mimi kuishi ni mawili, aidha NIPATE FURAHA ama NIPATE MAUMIVU. Chochote afanyacho binadamu, kina matokeo makuu hayo mawili. FURAHA ndiyo faida ambayo kila mtu anaitaka, lakini MAUMIVU ni hasara ambayo kila mtu anaikwepa! Yule anayefurahia, maisha kwake ni furaha, lakini yule anayeumia ni wazi kwake maisha ni janga/nonesense/upuuzi. Hivyo kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni kuwa "MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO NI UPUUZI" Hata hivyo kwa vile kuishi kwangu kunategemea sana kuishi kwako wewe, ni wazi kuwa Furaha ama maumivu yangu, yatachangiwa nawe, hivyo siwezi kuwa na Furaha yangu binafsi, ila yetu mimi nawe maana TUNAFUNGAMANA! Hivyo basi, "Maisha ni Furha, kama haipo ni Upuuzi. Na hakuna Furaha ya Mtu, bali WATU" Kama kweli tunataka kufurahia kweli matokeo ya kuishi kwetu ni lazima mimi nawe TUSIKINZANE, TUELEWANE/TUFIKIRIANE. Kama hatuwezi, basi ni maumivu tu! Kilicho leo, ni Upuuzi kwa sababu kuna Furaha ya mtu na si Watu, ni BATILI/IMEKUFA.
Maisha ni Furaha, Furaha ya kweli ni Kuishi Upendo(kupendana), na huo(upendo) ndio Ukweli mkuu kuliko wote ule chini ya jua, Ukweli ni MANTIKI yaani UUWIANO SAHIHI, mtu mweusi anaita UTU, nao ndio KUFIKIRIANA, yaani KUPENDANA (upendo), ndio FURAHA hiyo na hayo ndio MAISHA. Ni kama duara kwangu, MAISHA => Furaha => Upendo => Ukweli => Mantiki => Utu => Upendo => Furaha =>> MAISHA.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Ahsante mkuu JingalaFalsafa.
Umegusia sehemu muhimu sana ya maisha: Furaha,amani,upendo n.k.
1/Sasa mkuu JingalaFalsafa,ina maana,kwa defn hii,watu walio in deep sorrow na matatizo makubwa Wamekufa ingawa wana exist?
2/"Zao la Uhai ndio maisha"
Ina maana mtu anaweza akawa na UHAI lakini akakosa maisha?
Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Ingawa mtoa mada amebainisha watu anaotaka wachangie, naomba na mimi niwaingilie kwenye mjadala wenu kwa kuchangia kile ninachofahamu kuhusu maisha ni nini

Ninachofahamu mimi maisha ni kile kinachokufanya uendelee kuwepo hapa duniani ikiwa ni pamoja na shughuli zako, matamanio yako, matarajio yako ya baadae, jinsi unavyoingiliana na mazingira yako na jamii inayo kuzunguka pamoja na imani yako.

Haya yote yanafanyika kwa jinsi unavyotunza afya yako, unavyofanya kazi ili kukupatia ridhiki, mipango yako ya sasa na ya baadae ambayo ni matamanio yako ya nini unataka kufanya ukiwa hapa duniani, ni jinsi gani unayatumia mazingira yako iii kukupatia fursa na jinsi unavyoingiliana (interact with) na jamii inayokuzunguka hapa ndio utahitaji upendo, furaha au chuki kutokana na wewe mwenyewe unavyoishi na hiyo jamii.

Matokeo ya mambo yaliyotajwa hapo juu, yanafanya 'historia' ambayo hutusaidia kuboresha maisha ya sasa aidha kwa kupunguza au kuongeza kutokana na uzuri au ubaya wa jambo husika.....

Nipo kwenye gari nitarudi baadae!
 
Ahsante Mshua's.
N.B:
Ku tag au ku mention baadhi ya members haimaanishi hao ndio wachangie mjadala,
ni utaratibu wa kawaida sana hapa jamvini.
Ahsante tena mkuu Mshua's kwa mchango wako maridhawa.
Ninathamini!
 
Last edited by a moderator:

Hapana Mkuu, sijasema hivyo. Nilichosema ni kwamba, Maisha ni Matokeo ya kuishi kwa binadamu! Matokeo hayo yako ya pande mbili, yaani FURAHA ama UPUUZI/MAUMIVU. So si kweli kwamba yule aliye kwenye deep sorrow basi hana maisha, anayo lakini tafsiri yake kwake ni Upuuzi, wakati kuna wengine ni Furaha. Ndio maana nimesema, Maisha ni Upuuzi, kama haupo ni Furaha. Ila hakuna Furaha ya mtu bali WATU!
Binafsi kuishi sio matokeo ya Uhai tu, unaweza kuwa mfu na bado ukaendelea kuishi. Maana kwangu kuishi ni Kuathiri yale yanayokuzunguka (nyakati na mazingira yaliyopo), ndio maana naamini kuna kuishi hata ya kutoka kwa uhai/kufa. Ila tu inategemea uliishi nini! MANTIKI au HULKA ZAKO? Uhai ni just Uwezo kwa binadamu, ni just uwezo wa mwili wake(viungo vyake) kufanya kazi! Na vinapofanya hivyo ndio vinaathiri mazingira na nyakati fulani, yaani KUISHI.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Kwa upeo wangu mdogo, maisha ni process zote anazozipitia binadamu toka kuzaliwa mpaka kufa.
Lakini kinachoyapa mashiko haya mapito ya binadamu ni UTASHI, ambao ndio ESSENCE ya uwepo wake, na ndio unaomtofautisha binadamu na viumbe wengine, utashi.

Sasa kwa sababu binadamu ana utashi, tunategemea kuuona huo utashi katika maisha yake au kwa lugha nyingine maisha yanatakiwa yaongozwe na utashi.

Utashi umuongoze binadamu kujua maana ya maisha, na je katika kuyaishi haya maisha kuna wajibu maalum ambao anawajibika kuutekeleza? Je kuna principles maalum za maisha? Kama zipo ni zipi? Kuna athari yoyote ya kuzipuuzia hizo principles?

Lakini pia Binadamu amezaliwa na karama/ abilities, lakini kwa sababu ya ujinga unatufanya tusizijue, lakini kama binadamu atajifunza toka akiwa mdogo nini maana ya maisha, umuhimu wa yeye kujitambua na kujielewa vizuri pamoja na karama alizonazo kutamfanya ayatakase maisha yake, ya binadamu wenzake, viumbe wengine na mazingira yake.

Socrates alisema kuwa maovu ni matokeo ya ujinga na "unexamined life is not worthy living"
Kwa maana hiyo, ili kuishi maisha yaliyokusudiwa kwa binadamu, kiumbe mwenye utashi, kuna haja na ulazima kwanza kujua ni nini maana ya maisha, kwa nini unaishi, na kujitambua kwa karama tulizonazo ili kuyatakasa haya maisha.

Kama binadamu tungejua maana ya maisha ingetusaidia kujua maana ya UTU, UPENDO, HAKI na FURAHA. dunia ingekua bora zaidi ya ilivyo, maovu yangepungua sana.

Ndio maana wachache walioishi/wanaoishi wakijua maana ya maisha na wajibu wao wakifa hufa kimwili, akina Nyerere, Socrates, Gandhi, Che Guavara et al, hawa wote bado wanaishi nafsini mwetu, kwenye fikara zetu na wengine tunaweza tukafa na tukawaacha hawa wakiendelea kuishi vizazi na vizazi.
 
Hili swali ni pana sana na ningependa kwanza unambie unataka tujibu tokana na uelewa wetu au tokana na dini zetu? SOMETIMES imani zetu kidini na uelewa wetu binafsi vinaweza kua tofauti (that's my case) na kabla sijaanza kupaa naomba unifafanulie hapo juu.
 

Madam Roulette,ningefurahi ungejimwaga kutokana na UELEWA wako.
Karibu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa uelewa wangu na katika maana rahisi Maisha ni kipindi (years of one's life) ambacho mtu huwa hai hapa duniani. Kama kiumbe hupitia mengi katika kuhakikisha unaendelea kuwepo (surviving to fulfill biological role) na kuendeleza kizazi chako.

Ikiwa kuna maisha baada ya kutoka uhali ni suala la kiimani zaidi ambalo wengi wetu huamini kwa misingi ya kidni katika life after death ambayo ipo katika nafsi (spirit) na sio kimwili. Mara nyingine mimi hufikiria hivi pumzi itabitoka lini siku za karibuni au miaka kadhaa ijayo au itakuwaje lakini naona sio kazi yangu kuogopa kuhusu hilo...My chapter will be closed then....
 
Madam Roulette,ningefurahi ungejimwaga kutokana na UELEWA wako.
Karibu.
Kwangu mimi kuna tofauti kati ya maisha (life, tena THIS LIFE) na existence. This life is the period between the moment we are conceived (not born) and the moment we die. But our existence is well beyond that. In this life we aquire a consciousness ouf our own, through our souls, but in existence this consciousness is collective. we are still in touch with the collective consciousness through our spirit, and we are interacting at the physical level through our body, which is the sanctuary of our soul. take it this way:
1. Spirit: the divine dimention in us, which is common to all human beings and connected to a greater Spirit
2. Soul: the dimention that is unic to us, but unseen. that's what makes me be me.
3. The body, hapa sitii neno.
This life is the process where the spirit is in a body, and where the soul exists. when I die, the spirit goes back to where it was (with its achievements) and the soul disapears (or it doesn't?). the body decomposes and its energy fuels life on earth. Mfano mzuri ni hii picha:



When the drop is up, it's a single drop, but when gravity pulls it down it will become part of the ocean again. Life is that moment when the drop is detached from the ocean.
that, Kima Mchanga, is my understanding of life.
 
Last edited by a moderator:
Thank you madam Roulette for that great explanation.
Your comment brings me to further questions:
1:What is Soul?
Where is it located?
2:What is spirit?
Where is its location?
Is there any life after this life on Earth(Where the spirit and its achievements have returned)?
Karibuni.
 
Last edited by a moderator:
Nikiendelea kujibu kwa uelewa wangu:

1. the spirit is the divine entity in us. It is what is refered to as Nefesh in Hebrew and Nafs in arabic (or Nafsi in Kiswahili). This is eternal, and is can be illustrated by the ocean in the picture. to me it is the most important dimention of a human being. This dimention is perfect. Ndio pumzi ya Mungu.

2. The soul, also invisible is the entity that results from the interaction between our spirit and our human existence. It is referred to as Rouah in Hebrew or Roho in Kiswahili. It is not perfect as mtu anaweza kua na roho mbaya au nzuri tokana na his life, his mind, his experience, circumstances etc. It is this dimension that fades away (progressively) as the spirit leaving the body goes back to the ocean. The soul can be mislead into believing that it is the most important dimension of a human being and start behaving as if there is no ocean, and that when it dies it is the end of everything. The soul can only have an interaction with this world for as long as it inhabits a body.

3. The body is the temple, the sanctuary that welcomes the spirit and the soul. Once the spirit leaves it, the body starts a decomposition process to give its energy back to the earth. Some people don't go beyond believing in what their five senses tells them (sight, noise, taste, touch and smell). they are trapped in their body, they are trapped by the five organs of sense: eye, ear, tongue, skin and noze.
 
Maisha,maisha,maisha!!!!
'
Wacha niseme kama nifuatavyo kwa mujibu wangu
'
Ili kuwe na maisha ni lazima kuwe na uhai pamoja na mahitaji ya kuufanya huo uhai uendelee kuwepo
'
Nikija kwenye maisha,maisha ni kile unachokifanya kila siku,yaani kuamka,kula,kulala,kufanya kazi n.k
'
Maisha nadhani yanaelezeka hivyo,labda useme unataka kujua nini kilichoko kwenye maisha,maana kinachoyafanya maisha yawe maisha ni zaidi ya kimoja!
 

Mkuu Eiyer,nilitamani kupata ufahamu juu ya nini hasa maana ya maisha(naona wana baiolojia hawajatokeza hapa kuelezea life at cellular level),
ila nilitaka kujua maana hasa ya maisha,
nini kinafanya "maisha " yaonekane ya maana na kama je,baada ya maisha ya hapa duniani,yapo mengine?
What happens at death?
E.t.c.
Tiririka tu mkuu Eiyer kwenye field uliyo na ufaham nayo.
 
Last edited by a moderator:
Simple and clear maisha starts when born ends when dead
 
paulss mkuu,hayo "maisha" ninini sasa?
is everything since you born

ukizaliwa na kukaa dakika moja kisha ukafa maisha yako ndio hiyo dakika moja tu
kitendo cha wewe kuwa hai ndio maisha bila kujali unafanyanini

kwa maana nyingine maisha ni kila kitu unachopitia kuanzia unapozaliwa(some say since mimba inatungwa) hadi siku unakufa. haya ndio maisha
 
Watu watazungumza maisha kwa mitazamo ya "Kula Maisha au Raha"! Lakini Msingi Mkuu wa MAISHA NI UHAI mengine yanajengwa kutoka humo. Maisha ni uhai wa kuimbe wakati kina ishi, haijalishi kama kama ni virus, bacteria, fungus, mmea, mdudu, mnyama, Binadamu, jini, shetani, malaika au roho! Kiumbe au roho yoyote ikifa inakuwa haina uhai na maisha yake yanakomea hapo!
 
acha na mm niseme kile ninachojua ,,maisha hasa,,ni mwenendo mzima uliofungamana na ww mwenyeo kihali na kimali,unaanzia kuzaliwa hadi kufa kwako,,ndio maana,,tunapata kusema,,hakuish maisha marefu,,kwakua mantiki ya maisha ndio kama hivyo nilivyojaribu kuichambua,ahsante sana,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…