Mkuu wangu
Kima Mchanga, hii mambo ni tata sana kwa kila mtu! Hivyo ni wazi kila mtu anaweza kutoa tafsiri yake vile alivyoguswa na dhana nzima ya Maisha, na zote zikawa sahihi ama laa! Wapo watakaotafsiri kwa kuangalia chimbuko/asili, wengine experiences na wengine matokeo yake! Na wote utakuta wanazo hoja za msingi!
Binafsi ninaamini hivi... Zao la kuishi kwangu ndio kitwacho maisha, zao la uhai wangu ndio maisha. Hivyo asili ya maisha ni uwepo wa binadamu na anayofungamana nayo! Sasa katika kuishi kwake mwanadamu kuna mambo mawili, aidha AFURAHIE au AUMIE. Matokeo ya mimi kuishi ni mawili, aidha NIPATE FURAHA ama NIPATE MAUMIVU. Chochote afanyacho binadamu, kina matokeo makuu hayo mawili. FURAHA ndiyo faida ambayo kila mtu anaitaka, lakini MAUMIVU ni hasara ambayo kila mtu anaikwepa! Yule anayefurahia, maisha kwake ni furaha, lakini yule anayeumia ni wazi kwake maisha ni janga/nonesense/upuuzi. Hivyo kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni kuwa "MAISHA NI FURAHA, KAMA HAIPO NI UPUUZI" Hata hivyo kwa vile kuishi kwangu kunategemea sana kuishi kwako wewe, ni wazi kuwa Furaha ama maumivu yangu, yatachangiwa nawe, hivyo siwezi kuwa na Furaha yangu binafsi, ila yetu mimi nawe maana TUNAFUNGAMANA! Hivyo basi, "Maisha ni Furha, kama haipo ni Upuuzi. Na hakuna Furaha ya Mtu, bali WATU" Kama kweli tunataka kufurahia kweli matokeo ya kuishi kwetu ni lazima mimi nawe TUSIKINZANE, TUELEWANE/TUFIKIRIANE. Kama hatuwezi, basi ni maumivu tu! Kilicho leo, ni Upuuzi kwa sababu kuna Furaha ya mtu na si Watu, ni BATILI/IMEKUFA.
Maisha ni Furaha, Furaha ya kweli ni Kuishi Upendo(kupendana), na huo(upendo) ndio Ukweli mkuu kuliko wote ule chini ya jua, Ukweli ni MANTIKI yaani UUWIANO SAHIHI, mtu mweusi anaita UTU, nao ndio KUFIKIRIANA, yaani KUPENDANA (upendo), ndio FURAHA hiyo na hayo ndio MAISHA. Ni kama duara kwangu, MAISHA => Furaha => Upendo => Ukweli => Mantiki => Utu => Upendo => Furaha =>> MAISHA.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!