Until_The_End
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 1,456
- 2,202
Kama nimepotosha, ni haki yako kusahihisha. Kukosoa bila kusahihisha haina afya katika kujifunzaWewe umechukua mistari baadhi, na kwa sababu hiyo umepotosha wazo zima la andiko lenyewe: andiko au ujumbe unawahusu akina nani.
Ungeanza kusoma kuanzia Rum 8: 31-39.
Uko sahihi kwamba Mungu anakaa kwenye Moyo ulio safi.Mungu anawapenda watu wote:wema na waovu.
Lakini Mungu ni mwema, mkamilifu na msafi wa hali ya juu wa akili; kwa hiyo hachangamani na uchafu.
Yesu alizungumza Heri, katika heri hizo alisema, "...Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu".
Mungu ni kweli anakaa ndani yetu, lakini anakaa ndani ya wale tu wenye usafi; usafi wa moyo na akili.
Mungu akai kwa watu wachafu, hatahivyo, anatupenda watu wote. Ukweli huu ni muhimu kuuelewa, ili tufanye bidii tuwe na usafi wa moyo.
Hakuna mtu ambaye hawajibiki au hatawajibika. Yesu hakuja duniani au hakufa msalabani, ili kuondoka hilo.Kutambua kuwa kwa matendo yako utapata uzima ni kujikweza na kufanya msalaba wa Yesu ukose maana. Hebu jiulize kama kwa matendo yetu tunaweza kuokoka na kuwa na uzima basi yeye alikufa ili iweje?
Jibu hilo swali...Hakuna mtu ambaye hawajibiki au hatawajibika. Yesu hakuja duniani au hakufa msalabani, ili kuondoka hilo.
Kwa hiyo, kifo cha Yesu msalabani, hakimuondolei mtu uwajibikaji. Kila mtu atawajibika kadiri ya matendo yake.
Yesu Kristo, kwa kuja kwake duniani, mafundisho yake, matendo yake, mateso, na kifo chake msalabani, amemrejeshea mtu haki yake ya asili (origin justice) aliyoipoteza kwa dhambi.
Kifo cha Yesu msalabani hakiondoi wajibu.
Ndio. NinawezaJe unaweza kufaulu kuwa na moyo safi kama Mungu akiangalia shughuli na juhudi za maisha yako?
Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.Ndio. Ninaweza