Maisha siyo maisha bila maarifa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Tunahitajika kujiondoa katika dhoruba za maisha ambazo zipo ndani ya uwezo wetu,na kimsingi kinacho tutese kwa sehemu kubwa ni kilichopo ndani ya uwezo wetu, hatuhitaji kujifunza,tunavua vazi la asili la kiuanafunzi, utunukiwaji wa vyeti hutufanya kuona kuwa tumemaliza kujifunza

Lakini tunahitaji maarifa kila wakati, tunahitaji kuchuja aina ya maarifa tunayo yaingiza ndani ya akili zetu, lazima kila siku tukusanye au kuongeza ujuzi, tunahitaji maarifa ili kuweza kutupa marekebisho katika nyanja tofauti tofauti za maisha yetu, bila maarifa maisha hayawi maisha katika kuishi

Sasa ulimwengu umekuwa rahisi kufikika hivyo ni rahisi sana kupata maarifa.Funguo ya kuufungua ulimwengu ipo katika maarifa hivyo tafuta ujuzi ili uunde njia bora ya kuishi, katika kutafuta maarifa ni muhimu sana kufahamu yakuwa utakutana na maarifa danganyifu

Ukuaji hupatikana katika maarifa hivyo weka wakati wa kujifunza,kuna changamoto katika kujifunza kuna wakati utakutana na maarifa danganyifu , unahitaji umakini wa akili kupenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…