Hii hali inawapata watu wengi sana wenye kazi/majukumu yenye kuwategemea sana hasa middle and senior cadre of workers/experts. Ndio maana taasisi nyingi zenye malipo makubwa kitu kikubwa kinachowafanya wawe "waajiri wabaya" ni ile work-life balance.They scored very poorly hadi wanatafuta hadi mikakati ya kuimprove na inashindikana maana ule mzunguko wa kazi uko palepale!
Tukiacha mchango wa waajiri katika kukosekana balance, kuna upande mwingine pia ambao unachangiwa na familia zenyewe. Huwa nasema wazee wetu waliostaafu ambao walitulea kwa kipato chao walichokipata kwenye mishahara na ambao hawakujisikia kusukumwa kuongeza kipato, walifanya vizuri kuliko siye wa zama hizi za kukimbiza shilingi isiyokamatika!
Mwanao MTM leo anataka "toys" ambazo siyo toys bali ni "hi-tech gadgets" zinazouzwa mamilion ya shilingi, umlipie ada ya mamilioni, atoke kutembea na kuburudika kwa gharama kubwa, akifunga shule aende holiday,avae mavazi yaendanayo na world trends.... the list is long!
Mamaa naye anataka aishi maisha mazuri, mjenge au mpangishe nyumba ya kiwango, usafiri wa binafsi, maisha bora kwa kifupi.Je usipochacharika unadhani familia itakuwa na amani na wewe? Je unadhani utajivunia heshima kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kutokuhangaika... nikimaanisha urudhike na kipato cha kijungu-jiko kisichokuweka kwenye level ya wewe kujiskia confident kujichanganya nao?
Ukija kwenye kujijali afya, ukiwa huna pesa ( unayoitafuta kwa kujinyima muda wako na kuuwekeza kwenye kazi) utamudu AAR na bima nyingine za afya assuming haulipiwi na muajiri.
Nina mengi ya kuchangia kwenye hili kuonyesha its becoming almost impossible kuligawanya hilo gudumu alilotuwekea MBU na kutoa nafasi sawa.
Ninapoandika huu mchango wangu, nimekumbuka video moja tulionyeshwa miaka ya nyuma kuhusu management and leadership kwa kifupi ikionyesha baba aliyejitesa sana kutafuta ili aipe familia yake maisha mazuri.Katika kimbizana hiyo akaja kupata heart attack akafa! Alipokufa akaenda mbele ya Muumba, na akaulizwa jitetee kwanini upate paradiso na siyo jahanamu.Utetezi wake ulikuwa kwamba alihangaikia sana familia yake hadi akajikuta umauti unamfika!
Cha ajabu na kilichonishtua ( miaka ile) ni kwamba Muumba alimuuliza tena " je una uhakika familia yako ilifurahia hali hiyo?" Akajibu ' nina uhakika maana hawakukosa chochote walichohitaji".
Muumba akamwambia " subiri tuthibitishe kama kweli familia yako ilirIdhika". Ikaonyeshwa Re-play ya maisha ya yule bwana na familia yake...jamaa alishtuka kuona jinsi mkewe alivyokuwa ananung'unika kwa vile muda mwingi hayuko nyumbani hata pale alipokuwa na watoto wadogo, watoto walipoumwa, mke alipoumwa, yalipotokea matatizo mbalimbali kwenye familia etc. Kisha akaonyeshwa jinsi hakuwepo kuona wanae wakikuwa kwa haraka, wakianza shule, wakifanya homework na kushiriki michezo mbalimbali.Watoto walihudhunika baba hakuwepo kuwapa support nk.
In short jamani hakuna jema.Haya maisha ya sasa ni ubatili mtupu!
Mimi mwenyewe ninajiangalia na kujiuliza itakuwaje kama naulizwa maswali aliyoulizwa huyo bwana hapo juu. Je na nyie wengine majibu yenu yatakuwa vipi?
Je mtastahili paradiso?
Pole kusoma kitu kirefu lakini ni vema kushirikishana.