hahahaaaaaaaaa.... yaani wengine tumegeuza magurudumu yetu yamekua kama embe au hata mstatiliDuh..gurudumu langu haliendeshi hata mkokoteni...needs big tym fixing!
Thanks Mbu...leo umetoa tiba badala ya maradhi!
Yule miss J ndoa ndio dawa yake mana pale hakuna mjanja inaonekana anaingia katika ile ndoa akiamini 1+1=2 kumbe hakuna hio kule jibu ni 11.
Ataijua sawa sawa.
Ila huyu Mbu bana naona kakosea kujiita Mbu
Haya mapost anayoweka hapa JF hayafanani kabisa na jina lake
Yaani akianzisha mada, akachangia M'JamiiOne utafikiri ni mtu na mke wake.
Nampa wazo afikirie kulibadilisha if posibo.
I am a failure when it comes to balancing my time..... All blames to TBL/SBL. Why on earth are they brewing this kind of drinking liquid? ...When I get out of my office the only thing in my addicted mind is Beer......... and only Beer!
Ataijua sawa sawa.
Ila huyu Mbu bana naona kakosea kujiita Mbu
Haya mapost anayoweka hapa JF hayafanani kabisa na jina lake
Yaani akianzisha mada, akachangia M'JamiiOne utafikiri ni mtu na mke wake.
Nampa wazo afikirie kulibadilisha if posibo.
"You can have anything you really want but you cannot have everything you want."
The wheel of life is a valuable tool to help you evaluate whatΒs working and whatΒs not working in your life.
...ni kawaida kusikia mtu anakujia na excuse ya,."..sikuwa na muda!"...lakini je? huwa unajipangia mambo yako kwa mujibu wa muda, au ndio umejikubalisha muda utawale sehemu kubwa ya maisha yako?
Evaluate maisha yako kisha ujiulize;
Badala ya kulaumu hali ngumu, jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kujipangia yaliyo na umuhimu katika maisha yako. Kila siku iendayo hairudi Nyuma. Usilolifanya leo na kuliweka kiporo kwa kisingizio utalifanya kesho jua umeshaharibu mtiririko wa mpangilio wa maisha yako. Jiepushe kulimbikiza shughuli.
- una muda wa kutosha kukaa na kubadilishana mawazo na familia yako? Unawasaidia watoto homeworks zao, kujua maendeleo yao kimaisha? ...vipi kutembelea ndugu, jamaa na marafiki?
- una muda wa kutosha na mpenzi/mke/mume wako, ...mwenza wako halalamiki hutulii nyumbani?
- umejiwekea muda wa kutosha kujiburudisha akili, hii ni recreational activities hata kama ni kwa kibustani cha mboga..., michezo etc? , una muda wa kutosha kufanya ibada?
- una muda wa kutosha kujiangalia afya yako, kufanya mazoezi, regular check ups? au mpaka uumwe ndio unakwenda hospitali?
- Una muda wa kutosha kufanya kazi zako bila kuelemewa na kurudi nazo nyumbani? Wengine 'hushikika' hata kula wanasahau. Nawe ni mmoja wao?
"You can have anything you really want but you cannot have everything you want."
"To know yourself is the first and most important step to pursuing your dreams and goals." Β Stedman Graham
Liwezekanalo kufanyika leo, usilisubirishe. Ni wangapi kufumba na kufumbua wamejishtukia tayari retirement age ishawafikia ilhali hawakukumbuka kuwekeza?
Fainali uzeeni!....tusisubiri kukurupushwa ilhali kushakucha!...Hakuna awezaye kukupangia mkaisha yako ila wewe mwenyewe. Tuanze kujipangia maisha yetu kuanzia sasa kisha mtaona uwiano mzuri wa maisha, furaha, amani na mapenzi yanavyorudi tena majumbani mwetu. Otherwise,
kwanini unaamini hauna muda wa kutosha (ku balance maisha yako?)
Jamani tusifikirie kila ndoa mbaya.. Pengine Miss Judy kapata mtu aliye compatible naye.. Hebu msameheni jamani.Yule miss J ndoa ndio dawa yake mana pale hakuna mjanja inaonekana anaingia katika ile ndoa akiamini 1+1=2 kumbe hakuna hio kule jibu ni 11.
Mie ndio maana nikiona maji ya shingo nabeba mwanangu na mdada wake naenda nao safari hukohuko kwenye kaziLol maisha yetu wengine mwenzangu mh......unapanga weekend uende beach na mtoto mara wapigiwa simu ijumaa jioni unatakiwa kusafiri Ntwaraaaaaaaaa........... miezi miwili!! Ukirudi wakuta meza inakusubiria na mkoloni ndo kasimama tititi!! kutahamaki miezi miwili hujaonana na rafiki wala kukaa na familia!
Actually Mbu najialumu sana mwenyewe kwa kuweka mbele career and finance ambavyo vimekula kabisa spiritual, personal growth, health
relationship na family navyo nisipokua makini vitanitupa mkono
I am going to try something to reverse this... the only challenge ni kazi/career success na pesa... they are more addictive than anything i have ever experienced
shem, what can i say??
....this is a very good reminder about our life purpose, the only challenge niionayo ni ile definition ya success kwa community zetu, including those we love most... what if i balance all of them and end up with less income and stunted career path, my love may never give me the same respect
its a challenge really, especially now you find in many couples wote wanakua career people
Hii hali inawapata watu wengi sana wenye kazi/majukumu yenye kuwategemea sana hasa middle and senior cadre of workers/experts. Ndio maana taasisi nyingi zenye malipo makubwa kitu kikubwa kinachowafanya wawe "waajiri wabaya" ni ile work-life balance.They scored very poorly hadi wanatafuta hadi mikakati ya kuimprove na inashindikana maana ule mzunguko wa kazi uko palepale!
Tukiacha mchango wa waajiri katika kukosekana balance, kuna upande mwingine pia ambao unachangiwa na familia zenyewe. Huwa nasema wazee wetu waliostaafu ambao walitulea kwa kipato chao walichokipata kwenye mishahara na ambao hawakujisikia kusukumwa kuongeza kipato, walifanya vizuri kuliko siye wa zama hizi za kukimbiza shilingi isiyokamatika!
Mwanao MTM leo anataka "toys" ambazo siyo toys bali ni "hi-tech gadgets" zinazouzwa mamilion ya shilingi, umlipie ada ya mamilioni, atoke kutembea na kuburudika kwa gharama kubwa, akifunga shule aende holiday,avae mavazi yaendanayo na world trends.... the list is long!
Mamaa naye anataka aishi maisha mazuri, mjenge au mpangishe nyumba ya kiwango, usafiri wa binafsi, maisha bora kwa kifupi.Je usipochacharika unadhani familia itakuwa na amani na wewe? Je unadhani utajivunia heshima kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kutokuhangaika... nikimaanisha urudhike na kipato cha kijungu-jiko kisichokuweka kwenye level ya wewe kujiskia confident kujichanganya nao?
Ukija kwenye kujijali afya, ukiwa huna pesa ( unayoitafuta kwa kujinyima muda wako na kuuwekeza kwenye kazi) utamudu AAR na bima nyingine za afya assuming haulipiwi na muajiri.
Nina mengi ya kuchangia kwenye hili kuonyesha its becoming almost impossible kuligawanya hilo gudumu alilotuwekea MBU na kutoa nafasi sawa.
Ninapoandika huu mchango wangu, nimekumbuka video moja tulionyeshwa miaka ya nyuma kuhusu management and leadership kwa kifupi ikionyesha baba aliyejitesa sana kutafuta ili aipe familia yake maisha mazuri.Katika kimbizana hiyo akaja kupata heart attack akafa! Alipokufa akaenda mbele ya Muumba, na akaulizwa jitetee kwanini upate paradiso na siyo jahanamu.Utetezi wake ulikuwa kwamba alihangaikia sana familia yake hadi akajikuta umauti unamfika!
Cha ajabu na kilichonishtua ( miaka ile) ni kwamba Muumba alimuuliza tena " je una uhakika familia yako ilifurahia hali hiyo?" Akajibu ' nina uhakika maana hawakukosa chochote walichohitaji".
Muumba akamwambia " subiri tuthibitishe kama kweli familia yako ilirIdhika". Ikaonyeshwa Re-play ya maisha ya yule bwana na familia yake...jamaa alishtuka kuona jinsi mkewe alivyokuwa ananung'unika kwa vile muda mwingi hayuko nyumbani hata pale alipokuwa na watoto wadogo, watoto walipoumwa, mke alipoumwa, yalipotokea matatizo mbalimbali kwenye familia etc. Kisha akaonyeshwa jinsi hakuwepo kuona wanae wakikuwa kwa haraka, wakianza shule, wakifanya homework na kushiriki michezo mbalimbali.Watoto walihudhunika baba hakuwepo kuwapa support nk.
In short jamani hakuna jema.Haya maisha ya sasa ni ubatili mtupu!
Mimi mwenyewe ninajiangalia na kujiuliza itakuwaje kama naulizwa maswali aliyoulizwa huyo bwana hapo juu. Je na nyie wengine majibu yenu yatakuwa vipi?
Je mtastahili paradiso?
Pole kusoma kitu kirefu lakini ni vema kushirikishana.
Yaani unapanga kwenda kwenye ibada (kujaribu kurejesha uhusiano wako na Muumba wako)....ukiwa njiani unapigiwa simu....njoo hapa baa mpya, nipo na A, B na Y....
Ratiba inabadilika....unasahau njia ya kwenda nyumba ya ibada....
Damn...I surely need a life mechanic.....
Ni kweli lakini Mbu ukiangalia kiundani zaidi ni wazi kuwa kila kitu kiko mikononi mwetu!! If we strictly stick to our job description (kwa walioajiriwa) ni wazi kuwa utawezajipangia na kuweka limit ya ufanyaji wako wa kazi but kwangu mimi (Sijui wengine) najikuta kwenye dilema kwa kuwa kuna kale kamstari kasemako......and any other work assigned by my employer...yaani hii inanifunga hata akinambia unatakiwa kuja jumamosi au uunganishe safari juu kwa juu hata miezi miwili nashindwa kumwambia siwezi.......nilisign mwenyewe ule mkataba ujue!!
But I think there is a need to reflect some aspects!
But kitu kingine ni how do we get satisfied?? especially ukiwa na kazi ambazo yaani zinalipa? mfano safari zenye per diems nzito na masurufu mengineyo (Posho za kibunge lol) how can we sacrifice that only to spend some quality time with our loved ones?
Mwe!! Mtihani
Mbu we need a 48 hours day π instead of 24 hours only π in order to balance our daily lives
hhaaa hha! BaK wasemaje? twahitaji masaa 48?....
Mimi nakwambia tuanze kwanza kujiuliza haya masaa 24 tuliojaaliwa tunayatumiaje.
Ukishaweza weka hayo masaa kwenye mchanganuo unaoeleweka, wallahi utajikuta wacheka mwenyewe unavyo waste!
Mbu tayari tuna uthibitisho wa kutosha kwamba 24 hours hazitutoshi ili kuweza kuendana sambamba na hilo gurudumu la maisha, hivyo labda saa moja iwe na dakika 120 π badala ya dakika 60 au tupunguze masaa ya kufanya kazi kwa siku badala ya masaa manane iwe ni manne tu tena kwa ujira ule ule wa masaa manane (Waajiri kamwe hawatalikubali hili) labda Wanadamu tutafanikiwa kuweza kuendana na hilo gurudumu la maisha, vinginevyo itabaki kuwa ni ndoto tu.
NB: Nina baadhi ya marafiki ambao wanaupanga muda wao kila siku wakitoka kazini watafanya hili watafanya lile n.k. na kila siku huwa nawauliza katika ile schedule yako ya jana ulikamilisha mangapi? Kila siku jibu linakuwa sikuyamaliza yote kutokana na hili na lile na hawa ni watu ambao wanajitahidi sana katika kupanga mambo yao kila siku iendayo kwa Mungu.