Big up!
Another useful contribution from Tulizo! Nimeipenda hiyo.
Naaam, yote uliyosema ndio yanayotokea. Kuna thread nilianzisha
(Couples) kujipendelea muhimu. Wengi walizinduka,...
Hivi tunavyoishi, kidogo kidogo tunaelekea kwenye dysfunctional families.
Baba anakwenda kazini na gari lake, mama anakwenda kazini kwa gari lake.
watoto wanakwenda shuleni kwa school bus. Hapo wote wanategemea kunywa chai on the road/ofisini au
(watoto) shule.
Watoto wanarudi majumbani kumi na moja jioni, house girl ndio anawakaribisha. Wakati huo mama mtu
baada ya kazi anapitia saloon/kikao cha harusi/etc etc almuradi asirudi nyumbani on time. Mume naye hivyo hivyo.
atajichelewesha majiani humo eti anakwepa foleni.
By the time wazazi wote wanakuwa nyumbani, tayari watoto weshalala. Homeworks hazikufanyika.
walishinda wanacheza X-Box games, kuangalia Big Brother etc...Kesho yake mzunguko unaanza tena.
Mbaya zaidi, weekend...mke anakwenda tena saloon kwa kisingizio cha pedicure, sijui manicure, na kusukia weaving...
total time ya yote hayo ni masaa si chini ya sita! Mume nae huyoooo saloon za kiume...shaving, massage bla blah, akitoka hapo Rose Garden, Calabash, Break point etc...
Tunakimbia kabisa majukumu ya kifamilia. Watoto na ndoa zimegeuka mzigo,...kuwajazia ma X-box, na video games nyumbani unaamini ushawapa cha kuwa keep busy. Kumbe mnazalisha taifa la 'coach potatoes'...hakuna physical activities kuanzia baba anayefanya ibada zake pub, mama anayefanya ibada zake kwenye saloon za urembo, na watoto wanaobudu screens... baada ya siku chache baba ana kitambi, mama ana kitambi, watoto wana vitambi...wenyewe mnajiona mmenona kumbe mnalea maginjwa!
Outing kuuubwa ya baba na mama ni harusini, tena kwa mbwembwe mume anabebeshwa handbag ya mkewe kujionyesha ati ni perfect couples.... mnaishi kisanii tu kama mnacheza Egoli!
Uswazi nako ndio aaaaahhhh....
All ina all, nadhani kwa kiwango kikubwa MUME NI KICHWA CHA NYUMBA, usemi huu unatushtaki wanaume kwa kuchangia pakubwa haya ma dysyfunctional families. Sisi wanaume tukishajua thamani ya muda, kidogo kidogo twaweza oanisha principles zetu na za wake zetu majumbani, ili na watoto nao wajifunze maisha ya mpangilio. Tusilaumu mporomoko wa maadili ilhali wenyewe ndio tumeshikilia makali!
Hatuna muda, tuanze sasa kuupangilia.