Maisha ya Babu wa Loliondo(Ambilikile Mwasapile) kwa sasa

Maisha ya Babu wa Loliondo(Ambilikile Mwasapile) kwa sasa

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Babu wa Loliondo a.k.a kikombe cha uzima aliweza kutikisha karibu Afrika nzima kwa madai ya kuwa yeye anaweza kupona ugonjwa wowote kupitia dozi moja ya dawa wa maji pekee.

Wengi walitekwa na jambo hili na kufanya matajiri, maskini, wazee, vijana kumiminika katika kibanda chake cha kuuza hio dawa.

Sasa mzee huyu yuko wapi?

Babu wa Loliondo kwa sasa ameacha kazi ya utabibu baada ya kupata mikwanja ya kutosha. Jamaa huyu alipogunduliwa kuwa dawa yake ilikuwa haifanyi kazi ilimbidi kuingia mafichoni ili kuikwepa laana na mikono ya wengi...bila shaka wengi waliumia kwa kumsikiliza tabibu huyu.

Maisha ya zamani ya babu wa Loliondo

Babu sahizi ni mtu wa kulengwa kwa manati coz anamiliki nyumba, ana gari aina ya land rover na anaishi maisha ya kistarehe kuliko ya wengi wanayoishi majirani zake.

Picha tulizozipata katika blog yetu ya bkuHABARI zinamuonyesha babu wa Loliondo akipiga pozi kando ya Land Cruiser yake na pia sebuleni kwake. Cheki photo hapo chini.


Sebuleni kwake...hebu chunguza kule ndani

Akila pozi nje ya jumba lake

Akipiga pozi kando ya gari lake

Chanzo: bkuHABARI
 
Babu hapo anajuta na kusikitika kwa nini hii "akili" hakuipata mapema akiwa kwenye twenties.

Alafu mbona wale wenzake wa DESI wamezenguliwa na kukoseshwa amani wakati babu yeye anatesa tu na walichofanya hakuna tofauti ?
 
Dah babu tapeli katoka kimaisha hivi hivi duh akili ni nywele asee
 
Nimejifunza vitu vingi toka kwa babu wa loliondo.
1.usikate tamaa utajiri upo kwa umri wowote.
2.namna ya kuwa mbunifu kwenye biashara.
3.kutumia fursa vizuri.
4.namna ya kupiga deal kubwa za kulala masikini kuamka tajiri.
5.kila jambo linawezekana.
6.kuwaandaa wateja kisaikolojia na maneno mazuri kwa wateja
7 etc.

Kwa kweli babu ana akili sana sasa ni kusmile all da way to da bank.
 
Hapo alipitisha mchango wa jero tu,ni vipi kama angelipitisha mchango wa elfu 50 ambayo kimsingi watu wasingeona tabu kulipa?
 
Kwa vile alipitia mlango wa kanisa alifagiliwa sana.thubutu angepitia mlango wa msikiti,angekiona cha moto.
 
Back
Top Bottom