Maisha ya Babu wa Loliondo(Ambilikile Mwasapile) kwa sasa

Maisha ya Babu wa Loliondo(Ambilikile Mwasapile) kwa sasa

afu wanasema eti sijui ukifika miaka 50 kama hujaukwaa utajiri usahau...kumbe timing zako tu..
Babu kapiga pesa kimasihara tu, Magu ,Lowasa wamekunywa hicho kikombe,kuna ndugu huku alisafiri safari ndefu kwenda huko loliondo ,ila yuko poa labda kilimsaidia
 
The late mwendazake!
tapatalk_1567993480702.jpg
 
Babu wa Loliondo a.k.a kikombe cha uzima aliweza kutikisha karibu Afrika nzima kwa madai ya kuwa yeye anaweza kupona ugonjwa wowote kupitia dozi moja ya dawa wa maji pekee.


Wengi walitekwa na jambo hili na kufanya matajiri, maskini, wazee, vijana kumiminika katika kibanda chake cha kuuza hio dawa.

Sasa mzee huyu yuko wapi?

Babu wa Loliondo kwa sasa ameacha kazi ya utabibu baada ya kupata mikwanja ya kutosha. Jamaa huyu alipogunduliwa kuwa dawa yake ilikuwa haifanyi kazi ilimbidi kuingia mafichoni ili kuikwepa laana na mikono ya wengi...bila shaka wengi waliumia kwa kumsikiliza tabibu huyu.

Maisha ya zamani ya babu wa Loliondo
Babu sahizi ni mtu wa kulengwa kwa manati coz anamiliki nyumba, ana gari aina ya land rover na anaishi maisha ya kistarehe kuliko ya wengi wanayoishi majirani zake.

Picha tulizozipata katika blog yetu ya bkuHABARI zinamuonyesha babu wa Loliondo akipiga pozi kando ya Land Cruiser yake na pia sebuleni kwake. Cheki photo hapo chini.


Sebuleni kwake...hebu chunguza kule ndani

Akila pozi nje ya jumba lake

Akipiga pozi kando ya gari lake

Chanzo: bkuHABARI
Instincts zangu mimi hadi leo huwa zinaniambia kuwa huyu babu alitumiwa na watu wenye akili kubwa waliokuwa wanahitaji kupiga hela ndefu kwa ulaini. Hapa ni akili ndefu tu ilitumika na inayomilikiwa na watu wachache sana hapa duniani.

Walikaa chini wakapiga mahesabu wakasema tukifanikiwa kupata angalau asilimia 10 ya watanzania ambayo ni takriban watu million 6

6,000,000x500=300,000,000/= (million mia tatu)!
 
Huyu Babu ni Muuaji.....watu walitoka mbali sana, nchini na ngambo kuja kunywa kikombe..........hata nafikiri alikua akikojolea hayo maji!

Vibaya zaidi, watu waliacha kutumia dawa za kisasa, kwani alionya usitumie hicho kikombe na dawa zinginezo.........kwanza waarthiriwa wa UKIMWI ndio wengi aliwamaliza!

Kama ni nchi zilizoondelea angekuwa jela maisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom