Maisha ya Dar vs Maisha ya mikoani

Sisi tunaongelea pesa/ mshiko wapi nirahisi kuunyaka we unasemelea mambo ya mandhali sijui hewa....kuhusu hewa hata panya buku anapumua chini ya ardhi

Mshiko
Pesa
Hela [emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ukiweza kuishi DSM vizuri, basi unaweza kuishi popote pale nchini bila tatizo ikiwemo huko mikoani
Ujaishi lindi mkuu, ukiishi lindi nadhani utaishi popote hii nchi
 
Ujaishi lindi mkuu, ukiishi lindi nadhani utaishi popote hii nchi
EX wangu alikuwa huko na ndo kwao mi nilimjua baada ya kuja Dar kwa bimkubwa wake baada ya kuishi Dar kwa miaka kama 6 hivi akaamua kurudi kwao baada ya kuona huku Dar ramani hazisomi.ameishi kule takribani miaka miwili akawa analalamika kila tunapowasiliana anadai maisha huko ni magumu mno kiasi hata kula muda mwingine inakuwa shida mpk wakalime kwenye mashamba ya watu vibarua ndo wapate malipo tena ni kidogo mno kiasi kwamba anafanya tu kuokoa uhai,nikamwambia afanye awezavyo arudi Dar maana ugumu wa maisha ya kijijini na Dar hauwezi kuwa sawa Dar kuna fulsa nyingi sababu ya wingi wa watu,nikamwambia huku unaweza kupata mume au mwenzako mkatoka wote kila mmoja njia yake mkirudi usiku hamuwezi kukosa chochote kitu.kweli alifanya mpango akaja Dar alikaamiaka miwili tu akampata mwenzake wakafunga ndoa na saiv wanaishi maisha ya kawaida tu sio kama ya kule alipotoka.Dar haiwezi kufanana na mkoa wowote kwa fulsa na sababu kuu ni POPULATION.
 
Ina dar mina hot slama gyal 2times mi jus flot ,Mi lov A city weda si don wi mi bway stackin tugeda ina consat mi gi dem fleva.
 
Umemaliza mkuu
 
Apo kwenye population ndio umegusa kwenyewe Mkuu, lindi population ndogo ata mzunguko wa biashara mdogo

Na bado kuna umimi sana mtu yuko radhi atumie gharama kubwa kununua bidhaa umbaki mrefu akuache ulie karibu kisa tu sio mwezao
 
Kuna nn cha ajabu huko lindi, enhe vp korosho Bei gani sku hz?
Korosho ililipa miaka ya nyuma tusubiri bei ya mwaka huu, maana ata ufuta mwaka jana bei ilikuwa ya ajabu ila mwaka huu imeanza 2600

Mbali na kuwa na korosho hali ni tete sana hakuna maendeleo yoyote ukienda ukirudi kuko vilevile kama pamelaaniwa ivi[emoji3]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lindi wanapenda sana vigoma. Lakn korosho mm nmeuliza tu bei ya saiz n sh ngapi hata kama ipo chn
 
Dada yangu alipofika dar na ndoa ikavunjika

Maisha magumu
 
dar kuna hela ila maisha magumu, mikoa mingine kun amaisha mepesi ila hakuna hela
 
Dar kuna umri ukifika ukiona mambo hayaeleweki toka haraka sana kaangalie maisha sehemu zingine mikoani opportunities zipo nyingi tu,hapo dar watu wengi sana wanapoteza tu muda bila kujijua kisa wako dar,..mtu akipanga upande,friji,anapata hela ya kula na bia anaona kamaliza miaka inapota maisha hayohayo hujui kesho yako itakuwa vipi!....Huna akiba,Huna nyumba ukifiwa tu kurudi msibani mkoani ni shida,kama una kagari ndo hela unazopata zote zinaishia kwenye mafuta,ukifukuzwa kazi tu mwezi hauishi unaanza kuuza vitu ukoanza na gari ukihisi uko kwenye hayo maisha toka haraka nenda mkoani kuna fursa kibao kama wewe ni mjanja kweli utaingia tu kwenye mfumo utaona dar ulikuwa unajichelewesha!...na dar utakuwa unaenda tu kupumzika na kula raha na washikaji naongea kwa experience tulivuruga sana hapo dar sema nilishtuka mapema!...halafu maisha yanabadirika sasa hv maisha siyo lazima uishi dar kila sehemu kuna kila kitu sasa wewe vimba tu eti mimi naishi dar kisa dalali wa magari sijui wenzako watatafuta fursa zingine mikoani wana make bingo wakuja dar wanakukuta vilevile unashinda lumumba,kkoo au samora,...acheni ufala mmebanana sana hapo tanueni uwanja sehemu zingine mjipate
 
How old are you!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…