Maisha ya Instagram ni ya uongo kinoma

Maisha ya Instagram ni ya uongo kinoma

Mkuu sio insta tu hata JF siku hizi maisha ya hapa noma sana.

Kila mtu ni dingoo ana kimango chakutosha, kila mtu hapa JF anamilikia dinga kali kali.

Wengi hapa JF ni diaspora wako mambele huko wanafanya maisha hata ya kubeba boksi.
 
Mimi nilikuwa simfahamu demu mmoja wa Kenya anaitwa Huddah..

Sasa nikiwa naperuzi inst nikaona picha za demu mkali anapost, nikamfollow nikacheck picha zake aisee demu yupo bomba kichizi, nika m dm akajibu fresh kwa kuwa alikua alikuwa demu mkali akaniambia nipo wapi nikafake ili nimpate nikamjibu nipe State, akaniuliza wapi huko ni mkoa gani, dah nikasema mbona demu kama mkali halafu mjanja hajui State ni wapi, nikamwambia nipo Unyamwezi akaniambia kumbe wewe upo Tabora, akaniambia nisimsumbue tena, dah nikamwambia hapana nipo Unitee State Of America (Marekani) akajichekesha akaniambia utarudi lini nikamjibu kesho kutwa akaniambia nikirudi nimletee zawadi ya Iphone 5 nikamwambia poa,

Sasa kuja kudadisi nikaja nikangundua yule pimbi alikuwa anatumia picha za Huddah wa kenya, siku nimemwambia nipo bongo tukutane, akaniambia tukutane cocobeach, nilipo enda kumwona demu mwenye coco dah..
 
Back
Top Bottom