Maisha ya Kenani Kihongosi ni somo; hii ndiyo safari yake Kiongozi

Huko bila kuropoka utakubalika? Unataka kusema mtu anaweza kukubalika kwenye kundi la matapeli bila kuwa tapeli?
Ndege wafananao huruka pamoja na kwa tabia yake huyu kweli kalelewa Ki-CCM na hapo kafika nyumbani. UDC ulimpwaya! Katika waliokomaa kwa unafiki na kufuzu, huyu kweli ni zao la UVCCM! Sifa zote anazo!
 

Kuna kabila (...) Kihongosi maana yake ni Kiongozi kwahiyo juhudi zake zimeumbwa na jina lake amini usiamini majina huumba
 
Nani kakwambia ulete CV yake huku? Hakuna interview huku.
 
Inaonekana ukiwa mtu wa Chama sana ni lazima ukose akili na ushahidi ni huyu jamaa.
 
Hawa rafili zangu wa Akina Mutwa nawaamini sana kwa uzalendo na uongozi. Akamilishe degree zote kwanza ndio tumjadili.
 
Huyu asubirie uteuzi tu ila akubaliki kwenye ballot paper
 
Usikate tamaa, kuwa muadilifu, kuwa mzalendo, penda kujitolea na ishi kwa kuheshimu wengine. Wakati wa Mungu ukifika utainuka. Kazi iendelee
Mkuu, umefanya vyema kwa taarifa ya huyu kijana, lakini haya mambo ndani ya CCM ndiyo yanayotupa matatizo siku hizi.
Vijana wanalelewa na kuandaliwa kuwa walaji na siyo watumikia wananchi.

Taarifa muhimu kwa kiongozi mtarajiwa kama huyu ingejikita zaidi katika kutujulisha matendo yake, maneno yake na matamanio yake katika nafasi zote alizowahi kutumikia.
Hii habari ya kutueleza maisha yake ndani ya CCM pekee, tena yanayoonekana kulenga katika matayarisho ya ulaji akiwa ndani ya chama hicho, hayatusaidii sisi kumfahamu huyu mtu akipewa nafasi kubwa anawatakia nini waTanzania na nchi yake Tanzania.

Alisha sema au kufanya chochote kinachohusiana na vijana wenzake ambao wapo kwenye vyama vya upinzani?
Tueleze hayo, yatatusaidia na sisi kumpamba kama ulivyofanya wewe.
Mwisho ngoja nikuulize, kwa sababu siku hizi mambo haya ndio mtindo wenyewe: Je, nawe unajipanga kuwa CHAWA wa mkuu Kenani kKihongola?
Tumekwisha waona akina Lucas Mashamba hapa, kwa hiyo hatuwezi kushangaa nawe ukiwa tayari kwenye mazoezi.

Kama ni kijana mwenye kulipenda taifa hili, na watu wake. Nampongeza kwa mafanikio yake hayo.
 
C V ya G4N inatia moyo sana.
* Darasa la kwanza tu alipigwa suspension.
*. Darasa 6 akafukuzwa shule.
* Akawa mvuvi lake Rukwa.
" Akawa msaidizi wa mama ntilie (mji siutaji).
  • Akawa fundi msaidizi.
  • Akachukuwa boda ya mkataba.
  • Hivi Sasa ana boda yake.
*Mwaka huu navuta fomu ya kugombea uenyekiti serikali za mitaa
 
Nami niongezee haya
1.Alishateuliwa na Chama Chakavu kuwa Katibu Mkuu wa Jumuia ya Vijana Taifa

2.Nae ni mnufaika wa hela za Halmashauri ya Jiji Arusha zilizokwapuliwaga na aliyekuwa Mkurugenzi , ndugu Pima hadi akanunua gari aina ya Range
 
Tuna akili za kichawa chawa na kipigaji pigaji. Hko kote alikopita hutasikia kama aliwahi kusema kwa mdomo tu jambo la heri kwa nchi yetu. Utakuta alikuwa anasifia na kujipendekeza. Watu wa aina hii ndiyo wanairudisha Tanzania nyuma.
 
Ndege wafananao huruka pamoja na kwa tabia yake huyu kweli kalelewa Ki-CCM na hapo kafika nyumbani. UDC ulimpwaya! Katika waliokomaa kwa unafiki na kufuzu, huyu kweli ni zao la UVCCM! Sifa zote anazo!
Mleta mada hakumtendea haki, '' CV' ya huyo bwana imekosa mstari muhimu
''Mwaka 2019? akiwa Iringa katika mkutano wa UVCCM aishauri Wapinzania wapigwe risasi''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…