Maisha ya Kijiji cha kiboriani ni ya ajabu, huduma zote muhimu ni changamoto kupatikana

Maisha ya Kijiji cha kiboriani ni ya ajabu, huduma zote muhimu ni changamoto kupatikana

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
kiboriani.png
Kijiji cha Kibodiani kilichopo Wilayani Mpwapwa, Dodoma ni mfano wa Jamii nyingi zinazokabiliwa na changamoto kubwa za kijamii.

Wakazi wa kijiji hiki wanapitia matatizo mengi yanayohusiana na ukosefu wa huduma za msingi kama Elimu, afya, umeme na maji safi na salama. Hali hii inawaathiri kwa njia nyingi, huku ikihatarisha maisha yao na ustawi wa Jamii kwa jumla.

Ukosefu wa Huduma za Afya

Wakazi wake wanakabiliwa na ukosefu wa Zahanati, hali inayosababisha wanatembea umbali mrefu wa kushuka na kupanda mlima mrefu kwa zaidi ya Kilometa tatu (3), ili kufikia huduma za matibabu katika Hospitali ya Mpwapwa Mjini na wakati mwingine wanashindwa kabisa kupata msaada wa matibabu wanapohitaji.

Hali hii inasababisha kuenea kwa magonjwa yasiyo na udhibiti, huku watoto na wazee wakiwa kwenye hatari zaidi. Wakati wa milipuko ya magonjwa kama malaria au homa, familia nyingi zinakosa usaidizi wa haraka, na hii huleta huzuni na hasara kwa jamii.
Kijiji cha Kibodiani kinachokadiliwa kuwa na Wakazi 3,000, idadi kubwa ya Wananchi wake wamezaliwa nyumbani kutokana na ukosefu wa huduma za afya, wakinamama wajawazito kijijini hapo, ili wajifungue salama wanalazimika kuhamia Mpwapwa Mjini kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu ya mwisho ili kutohatarisha maisha yao pindi wanapotaka kujifungua.

Pamoja na hali hii kujifungulia nyumbani kutokana na mazingira kinamama wa Kibodiani wakifika hospitali bado wanatozwa faini kwa kosa la kujifungua nyumbani.

Ukosefu wa Umeme
Umeme ni msingi wa maendeleo ya kisasa, lakini katika Kibodiani, hakuna kabisa huduma za umeme. Hali hii inawafanya wanakijiji kukosa fursa za kujifunza na kujenga ujuzi.
Shule moja iliyopo aina umeme, hivyo Wanafunzi wanashindwa kujisomea wakati wa usiku au kutumia vifaa vya kisasa vya kujifunzia.
Aidha, ukosefu wa umeme unawazuia wakazi kufaidika na teknolojia na huduma nyingine muhimu kama redio na runinga, ambazo zinaweza kusaidia katika kupata taarifa muhimu za kijamii na kiuchumi.

Ukosefu wa Maji safi na salama
Maji ni maisha, lakini katika Kibodiani, wakazi wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama. Wengi wanategemea vyanzo vya maji ambavyo si salama, hivyo kupelekea kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.
Wanakijiji wanapata maji kwa kutembea umbali mrefu, wakati wa kiangazi, upatikanaji wa maji unakuwa mgumu zaidi. Hali hii inawaathiri kwa kiasi kikubwa, kwani ukosefu wa maji safi unachangia katika matatizo ya afya na ustawi wa Jamii.
Kukabiliana na changamoto hizi, wanakijiji wa Kibodiani wameamua kujitafutia suluhisho. Wameanza kuunda vikundi vya kujitolea ili kuhamasisha jamii katika kutafuta msaada kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali. Wanajitahidi kuanzisha ujenzi wa majengo ya zahanati kwa nguvu zao wenyewe.
Changamoto za Elimu
Kibodiani inakabiliwa na tatizo kubwa la elimu, ambalo linaathiri maendeleo ya watoto na jamii kwa ujumla.
Uchafu na ubovu miundombinu ya majengo ya shule na ukosefu wa walimu wenye ujuzi ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayowakabili Wanafunzi. Hali hii inachangia idadi kubwa ya Wakazi na Watoto katika Kijiji hicho kutokujua kusoma na kuandika.

Ubovu wa Majengo ya Shule
Majengo ya Shule ya Msingi Kibodiani yamechakaa na hayana mazingira mazuri ya kujifunzia. Wengi wa Wanafunzi wanajikuta wakisoma katika madarasa ambayo hayana viti na meza huku wengi wakikosa mahitaji ya vifaa vya msingi kama vitabu na madaftari.
Hali hii inawakatisha tamaa wanafunzi na kuwafanya wasijisikie hamu ya kujifunza.
Aidha, mazingira magumu ya kujifunzia yanachangia katika kushuka kwa kiwango cha elimu katika kijiji.

Tatizo jingine kubwa ni ukosefu wa Walimu wenye ujuzi na uelewa wa kutosha. Shule ya Msingi haina walimu wa kutosha na wale waliopo mara nyingi wanahama kila wanapopangiwa na Serikali. Hii inasababisha Wanafunzi kukosa uelewa wa msingi katika masomo yao, hasa katika lugha, hisabati na sayansi.

Ukosefu wa walimu wenye motisha pia unachangia katika kushuka kwa kiwango cha elimu, kwani wanafunzi wanahitaji mwongozo mzuri ili kuweza kujifunza kwa ufanisi.

Harakati za Kuboresha Elimu
Wanakijiji wamejaribu kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kupata msaada wa vifaa vya shule na kuhamasisha walimu kuja katika kijiji hicho.
Kijiji cha Kibodiani kipo katika changamoto kubwa katika sekta ya elimu, lakini jitihada za wanakijiji kuimarisha hali hiyo ni za kupongezwa. Ni muhimu kwa Serikali na Wadau wengine wa maendeleo kuwasaidia ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza idadi ya Walimu wenye ujuzi.
Kijiji cha Kiboroani kinaonyesha nguvu na uvumilivu wa watu ambao wanakabiliwa na changamoto nyingi. Ingawa wana matatizo makubwa yanayohitaji ufumbuzi wa haraka, jitihada zao za pamoja zinaonyesha matumaini ya kuboresha maisha yao.
Ni muhimu kwa Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuwasaidia ili kuweza kufikia malengo yao ya kupata huduma za msingi na kuimarisha maisha yao. Kwa kushirikiana, Kibodiani inaweza kuwa mfano wa mafanikio katika kukabiliana na changamoto za kijamii na maendeleo.
 

Attachments

  • kiboriani.png
    kiboriani.png
    1.1 MB · Views: 8
Ni ngumu sana kueleweka kwenye uongozi wa Rais anaechagua matukio ya ku trend ndio anayapa kipaumbele (goli la mama, matamasha ya wasanii nk.) vitu muhimu kama hivi havimuhusu
 
utashangaa na kusikia kipindi cha uchaguzi wimbo unapigwa CCM ni ile ileeee oooh ni ileeee wanapita na kanga zao walizopewa uchaguzi ukiisha vilio vinaanza tena, wanasahau Chorus ya CMM ni ile ile
 
Huu ndio mtaji wa CCM.
Mbunge wao anaitwa nani? Utackia mnajichelewesha kuchagua upinzani hapo nina uwakika ni mbunge wa CCM.
All the best
 
Penye unafuu kidogo wa maisha kwa Mkoa wa Dodoma ni pale mjini tu. Ukitoka nje ya pale, kukutana na hali kama hiyo ya Kiboriani ni jambo la kawaida sana.
 
Back
Top Bottom