Maisha ya Kuigiza: Kajala amiliki simu aina samsung galaxy note 4 ambayo bado haijatoka sokoni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Kupitia mtandao maarufu wa picha wa kijamii, mwanadada Kajala amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuweka picha ya simu aina ya samsung galaxy note 4 kwenye account yake kuwa anamiliki simu hiyo ilihali simu yenyewe ikiwa bado hata haijaanzwa kuuzwa sehemu yoyote duniani.

Kupitia picha hiyo kajala aliambulia maneno kadhaa ya kashfa toka kwa watu mbalimbali wengi wao wakimtaka aache maisha ya kuigiza.



Baadhi ya maoni hayo ni:-


"Hahahaha watu ndo wanatoa pre order october 16 ndo ina launched we umeitoa wap wakat bado haijaanzwa kuuzwa!dah!kwel sasa naanza kumin maisha yako ni ya kuigiza nakufata mkumbo mumy…pole"


"Duh … Simu aijatoka hiyo Pre Order imeanza USA & UK tarehe 19/09 lkn retail stores wanaanza kuuza tarehe 17/10 , hiyo pre order kwa watu ambao awataki kumiss ikitoka wanalipia kabisa ikitoka unaenda kuchukua , sasa hiyo umenunua wapi mwenzetu…"

"KAJALA ACHA UONGO HII CM LABDA MCHINA ORIGINAL HAIJATOKA MPAKA KWA ORDER LOO MWANAMKE MZIMA MPKA LEO UNARINGISHIA CM PAULA NAE AFANYE NINI"


Wewe unaonaje kuhusu jambo hili la mastaa nchini kuishi maisha ya kuigiza kwa ajili ya kuonekana wapo juu kwa mashabiki wao?
 
kama jina la msanii linavyotumika vibaya.......kaamua kuapply usaniii pia
 
Hivi watu wanaona ufahari gani kumiliki simu za gharama zaidi ya 1?ana iPhone 6,ile galaxy yake nadhani ni note 3 hii tena....

Duuu inaelekea unamfuatilia duuu
 
kuwa na akili ndogo ni matatizo sana! yeye hajioni kama anawatangazia biashara
 
Hivi watu wanaona ufahari gani kumiliki simu za gharama zaidi ya 1?ana iPhone 6,ile galaxy yake nadhani ni note 3 hii tena....

Ni sheedaaa simu standard yenye kusupport instagram,whatsapp,opera,email za exchange/pop3,skype front cam inatosha! Kutoa dola 1000 kwa ajili ya kuorder SG N4 halafu simu yenyewe unaweka vocha za jero jero wala si post paid basi ni majanga mengine bora uiuze ufuge kuku kama kala jeremiah alivoshauri.
 
kuwa na akili ndogo ni matatizo sana! yeye hajioni kama anawatangazia biashara

Hapa ndio nimejua hayuko sawa kichwani maana ana watangazia biashara bila kujua! Halafu yeye ndio anaona maendeleo?

Exposure yao ni ndogo sana wenzao wa mamtoni akipost picha kama hiyo basi ujue samsung washamuingizia dolari za kutosha bankwaa ila hawa super mbuluraz wao wanaona ni sifa wamuige Lady JD akipost oirflame product au airtel anaingiza mkwanja,na hata vituo vya luninga wakiona msanii kavaa nembo yeyote ya product ya kibiashara kama hajalipia kuirusha hilo tangazo kwenye tv husika basi editor/producer anaweka blurrrrrr/shades kulificha watu wapo kikazi zaidi.
 

wenye hela zao hawawazi bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…