Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,587
Anasema wafungwa ambao wanasubiri kunyongwa kwa siku hupewa dakika 15 tu za kutoka nje na muda mwingi hubaki ndani.
“Kwa kuwa wanakuwa wengi gerezani, basi kuna baadhi wanaweza kukaa muda mrefu bila kuona hata jua na baadhi wamefikia hatua ya kuchanganyikiwa kutokana na msongo wa mawazo,” anaeleza.
Kwa mujibu wa Moringe, kila anapokumbuka matukio hayo, hupatwa huzuni hasa anaposikia mtu amefanya mauaji dhidi ya mwingine kwa sababu yoyote ile ikiwamo wivu wa mapenzi.
“Kama utashuhudia maisha ya gerezani kwa watuhumiwa wa mauaji, sidhani kama utathubutu kuua mtu, kwani damu ya mtu haiwezi kupotea bure ni lazima utajutia tu.
“Ukiwa kule mwisho wa kukaa macho usiku ni saa tatu hivyo unapaswa kuwa kimya na kulala japo unalala katika kipande cha blanketi moja umetandika chini na jingine unajifunika.
“Nakumbuka kutokana na upweke na kuchanganyikiwa, kuna wakati ulitokea ugomvi, mfungwa mmoja kudai wenzake wanamloga hivyo, kuanza kupigana hadi viongozi wa magereza wakajitokeza na kutoa adhabu,” anasema.