mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,307
- 12,410
Habari za muda huu jf.
Tuanze moja kwa moja,tutatumia bibilia as reference pindi itakapohitajika Kama msingi kwakuwa ndio kitabu nikisomacho.
Nabii Musa ni Nani?
Maisha yake yanaelezewa kwenye kitabu Cha kutoka katika bibilia Kama mtoto aliezaliwa na wazazi waebrania lakini alilelewa katika kasri la ufalme wa misri.
Baadae anageuka kuwa mwanaharakati wa kutetea waebrania hadi anajikuta kaingia kwenye matatizo yaliyopelekea kukimbia nchi Kama vile tundu Lissu anavyofanya saivi (kutoka 2:15)
Alivyorudi toka uhamishoni midiani akawa mwanaharakati zaidi hata ya Bobby wine ama Samora machielle wa Mozambique hadi kufikia hatua ya kumega idadi kubwa ya watu katika kile kinachoitwa "kutoka misri kwenda nchi ya ahadi"
Baada ya miaka 40 ya huku na huku jangwani ,Siku ya kifo Cha Musa ilifika na aliarifiwa akafanya mchakato wakumpata mrithi wake na kumkabidhi madaraka (demokrasia), akapanda hadi mlima nebo.
Utata unaanzia hapa
Alipanda hadi mlima nebo akafa akiwa mwili wake hujapungua Nguvu(kumbuk 34:7)
Akazikwa na bwana na hakuna anaejua kaburi lake (34:5-6)
Je kwanini mungu alimtenga Musa na watu wake kabla ya kifo chake? alitaka wasione Nini?
Wengine wanaamini Musa hakufa bali alipazwa kwenda mbinguni kwa kuwa Yesu aliwahi kutokewa na Musa na eliya ambapo tunatambua Eliya hakufa hivyo wanasema Musa nae hakufa ndio maana alimtokea yesu (Marko 9:4).
Wengine wanaamini alikufa Ila mwili wake ulilindwa Sana na mungu (yuda 1:9).
Maswali yangu kwenu wanajamvi.
Je kaburi la Musa liko wapi?
Je Kuna jitihada zozote za kulitafuta?
Je kwanin Mungu alilificha hilo kaburi?
Nyongeza :hatujui lilipo kaburi la Gadafi Wala Osama bin laden.
2.kutokuaminika kwa chanzo Cha vifo vya viongozi wa Afrika Kama Jiwe na Nkurunziza je Kuna uhusiano na kisa hiki Cha Musa?
Asanteni karibu kwenye mjadala.