Surya
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 8,774
- 13,566
Soma kwa Makini uhusiano huu..hadi mwisho.
*******************
Yohana 1:1-5
[1]Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
[3]Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
NENO
Maneno yalitumika Kuumba ulimwengu,
MUNGU NI NENO, PIA MUNGU NI ROHO.
(NENO +ROHO)
Kilichoumbwa kwa mfano wa Mungu kwetu sisi wanadamu ni Roho zetu,
Mwanadamu akitamka neno kinywani au ndani kimoyo moyo (rohoni) maneno yake huweza kuumba yanakua na Nguvu na ndio maana Tunatakiwa kusali,
Unaposali unaruhusu Ule uungu au mfano ambao Mungu kakupa uweze kuachilia Nguvu ya kiroho ya kwenda kukamilisha unacho kiomba na iwe kwa imani.
Hata katika uchawi hutumika 'MANENO' ni lazima ili kwenda kuipiga roho ya mtu mwingine.
Nguvu ya roho ya mwanadamu inaweza kutumika kuumba kitu kizuri au kibaya yani ikatumiwa na Mungu au shetani ama tamaa zetu wenyewe.
Note: Kitu cha Pili 👇
Tangu katika bustani ya eden ilionekana kwamba, ili Mwanadamu aweze kujitakasa makosa yake au kutakasa kitu chochote kile kama Ardhi, ilihitajika Damu ya mnyama ili kutakasa dhambi.
Mwanzo 3:21
[21]BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Ngozi hiyo ilitoka wapi..
Inamaana kuna mnyama alichinjwa na damu kutumika
Kutoka 24:6
[6]Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu.
Musa pia alitakasa madhabahu kwa kutumua Damu 👆
Abramu pia alichinja ili kuweka Agano na Mungu
Torati Ya Musa imeeleza dhambi ilifutwa na Damu za Wanyama (mafahari) 👇
Mambo ya Walawi 4:2-3
2]..Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo;
[3]kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.
Wana wa Israeli walitolewa utumwani baada ya kuchinja kondoo aitwae Pasaka.
******************
Tuendelee na Maisha ya Mwanadamu
Katika familia kuna Baba ambae ni kiongozi wa familia, Mwanaume kapewa hisia za kumpenda mkewe na kutokukubali kabisa kushare mke wake na Mwanaume mwingine yeyote,
Mwanaume kapewa jukumu la kuwapenda wake zake na kweli Mwanaume ana hisia na upendo kwa mkewe.
Mwanaume hawezi kukubali mkewe apigiwe na mtu mwingine akitizama.
Katika familia kuna watoto ambao hupatikana wanapokutana Mwanamume na mkewe.
Ni hivyo hivyo hata kwa Mungu aliyetuumba ni Kama Baba haimaanishi kuwa Mungu ni Jinsia ya kiume, hapana..
Mungu ni Roho + Neno
Mungu anatuita sisi ni watoto wake ni mfano wa kuonesha umiliki wake kuwa anatumiliki;
Tunatakiwa kumsikiliza zaidi ya Baba zetu wa kimwili
Yesu Kristo ni mfano wa Mzaliwa wa kwanza, Hata kwenye Familia kuna mzaliwa wa kwanza, Mnaojua Upekee wa kuwa Mzaliwa wa kwanza kwenye familia mtanielewa.
Mwanadamu ni kuhani ila Yesu ni Kuhani mkuu.
Mwanadamu ni mtoto wa Mungu, ila Yesu aliye mfano wa mzaliwa wa kwanza ambaye ni lango la baraka zetu anaitwa mtoto wa Pekee.
Yesu kama mzaliwa wa kwanza wa Adamu 👇
Mathayo 9:6
[6]Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Mtoto huyu wa Kwanza ana mamlaka makubwa sana.
Wakolosai 1:15
[15]naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Like father like son, ukitaka kujua uwezo na tabia ya baba unaweza mtizama mtoto wake wa pekee.
Pia hata katika familia zetu makosa ya watoto wadogo anaweza kuulizwa Kaka au Dada mkubwa..
Tutapewa urithi -
Warumi 8:16-17
[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo Yesu
NOTE: Habari hizi hazimaanishi kwamba Mungu ana mke na kampa mimba hadi sie kuzaliwa.
Bali sisi tu watoto Kiroho, roho zetu alizoziumba kwa Mfano wake, baba yako wa duniani ni baba wa mwili lakini Mungu wetu ni baba wa Roho zetu.
Damu Ya Mzaliwa wa Kwanza inakwenda kutumika kutakasa Dhambi za Wanadamu na ulimwengu wote.
👉👉👉itaendelea
najitahidi kuweka mifano michache nisiwachoshe wasomaji.