Maisha ya mwanamuziki nguli Muhidin Maalim Gurumo 1940 - 2014

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
WanaJF,

Mimi ni mshabiki sana wa muziki wa Tanzania na hasa muziki ule uliokuwa ukipigwa kuanzia miaka ya 60 mpaka mwishoni mwa miaka ya 90.

Kuna huyu mwanamuziki "nguli" ambaye kwa sasa yuko na bendi ya OTTU Jazz kwa jina Muhidini Gurumo ambaye alianza kazi ya muziki miaka ya 1960.

Amepitia bendi mbali mbali kama vile Afrikan Stars ya wakati huo (sio twanga pepeta), Kilimanjaro Chacha, Nuta Jazz, DDC Mlimani Park "Sikinde", Safari Sound "OSS" wana ndekule.

Licha ya umri mkubwa bado nyimbo anazotunga a mirindimo ya sauti yake ina radha ile ile. Kwa mtazamao wangu nadhani ni mwanamuziki wa kuigwa na hasa na hawa waimbaji wetu wa sasa ambao anaibuka muda mchache na baadae kimyaaa jumla!!

Big up mzee Gurumo.

=============

 
Last edited by a moderator:
Wakati wa ujana wangu mimi baba yenuuuu,
Shati dukani shilingi sita unapata,
Lakini sasa shilingi sita,
Hata mkate hupatiiiiii!

Kwa hiyo wanaangu muishi kulingana na wakati *2

Jiepusheni na anasa,
fanyeni kazi kwa bidii,
Kama kuna mkorofi,
Kati yenu aache mara mojaaaaa!

Dah! Kweli Gurumo anahitaji SENKSI za kufa mtu!
 
twende kazi mazee!.........................
 


....Ngurumo ni mmoja na wanamuziki wachache waliojaliwa sauti nzito na nzuri ya kuvutia nchini. Ni mwanamuziki wa kupigiwa mfano katika kuipenda na kuitumikia fani yake isipokuwa kwa kitu kimoja tu kibaya nilichokisikia mitaani (kama ni kweli)-inasemekana yule mzee anavuta bangi kwa kwenda mbele....ili kufanikisha kazi yake, na kwamba inamsaidia kweli kweli!😕
 
Xpin na wakuu wengine kama mnakumbuka line up ya Sikinde mwaka 1978. Gurumo, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Suleiman Mwanyiro, Michael "King" Enock, Juma Town, Hamis Juma "Maalim Kinyasi", Cosmas Thobias Chidumule.
 
 
twende kazi mazee!.........................

Nilipokwenda kwa mjomba,
Nilikutana na binamu yangu,
Na kwa kweli tulipendana,
Wazazi wangu walinikatalia tusioane,
Eti kwa sababu
Yeye ni mtoto wa mjomba,
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoaaa

Wazaziiiiii ninasema (WASEMAAAA)
nasononeka
Kwa vileeeeee msichana,
Nilimpenda.......

Utapata wako mwingine, naye utampenda,
Mtoto wa mjomba kufunga ndoa si vizuriiii!

Laligeni nahitaji na Senksi nyingine hapa kwa hii yuziful post! Hahaha!
 

twende sasaaaaaaaaaaaaaaaa.....................

utakula senksi 24/7
 
 

Tuache uoga bangi ni mitishamba ambayo kama inatibu maradhi yako ina ubaya gani? Sio kila kilichopigwa marufuku na serikali hakiwasaidii watu acha watu watumie mitishamba kwa ajili ya afya zao! Serikali hiyo hiyo inasema haiamini mambo ya uchawi lakini nyakati za uchaguzi kama tutakavyoona mwaka huu, magari kibao ya serikali yatakuwa yanakwenda Bagamoyo kunani?
 
Xpin na wakuu wengine kama mnakumbuka line up ya Sikinde mwaka 1978. Gurumo, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Suleiman Mwanyiro, Michael "King" Enock, Juma Town, Hamis Juma "Maalim Kinyasi", Cosmas Thobias Chidumule.
Safi kabisa mkuu, ila umemsahau Hassan Rehani Bitchuka "sterio".
 
twende sasaaaaaaaaaaaaaaaa.....................

utakula senksi 24/7

Ukiwa ulionipata mkubwa,
baada ya kufariki wazazi wangu,
Alinichukua mjomba,
Kaka yake mama yangu,
Alinilea mpaka nimekua,
Alinisomesha mpaka nikamaliza,
Alinifanyia mpango nami ili niishi vizuri,

Lakini ndugu zake babaaa....... Wananipakaziaaaa!
 

Serikali kupiga marufuku matumizi ya bhangi si kwamba inawaonea wivu au kwa sababu nyingine yoyote...,ni kutokana na madhara ambayo yamethibitishwa kisayansi kwamba bhangi ni kama madawa ya kulevya mengine- Heroin, Mandrax, etc, hata kama in the short-run yanaweza kuonekana kama yanakusaidia..in the long-run yana athari kwenye ubongo wako.

Kuhusu hilo la uchawi ni swala lingine tofauti kabisa ambalo nawaachia wengine wachangie...
 


Mkuu Crispin, hapa kidogo umechanganya somo. Hili Goma la 'Mtoto wa Mjomba' la miaka ya mwishoni ya Sabini lilipigwa na Urafiki Jazz Band wana Chakachua Ngoma wakiongozwa na 'Ngulimba wa Ngulimba' Mrisho huku mwimbaji mmojawapo kama sijakosea sana akiwa Cosmas Chidumule.
 
Labda nikupoze kidogo kwa hili kipande cha 1982 cha Gurumo na wana Sikinde 🙂:

'mapenzi hayana kificho,
yaingiapo Moyoni mwangu,
mwenye mapenzi haonii ingawa macho aanayo,

Mtu chake apendacho,
hakina ila machoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani,
 

Hivi Gurumo hakuwepo humo? Kuna jisauti lake hapo, hebu vuta memori kiaina!
 
Hivi Gurumo hakuwepo humo? Kuna jisauti lake hapo, hebu vuta memori kiaina!

ha ha haa, hakuwemo mkuu na hakupata kuimbia Urafiki Jazz! Kipindi hicho Gurumo alikuwa Juwata akitamba na Super Sterio Bitchuka na na vitu kama:


'kijana una umbo la kupendeza,
mrefu mnene, na mwanya wa wastani,
hakika uzuri si shani,
utu wa mtu ni tabia njema...



Inakukumbusha mbali eh?
 

Saafi sana kwa kumkumbuka Ngulimba wa Ngulimba Juma Mrisho na Chaka Chua (Urafiki Jazz)
 
Lwikunulo: Bangi ni kitu cha kawaida sana ili mradi usiinuizie kwa mabaya. Wengi waliofanikiwa katika dunia hii wamevuta majani, mfano: George na Laura bush, Barak na Michel Obama, Bill Clinton, n.k. Ufisadi ni mmbaya zaidi kuliko bangi hasa ule unaofanywa na watu wakiwa macho makavu kama RA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…