Maisha ya mwanamuziki nguli Muhidin Maalim Gurumo 1940 - 2014

Maisha ya mwanamuziki nguli Muhidin Maalim Gurumo 1940 - 2014

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
WanaJF,

Mimi ni mshabiki sana wa muziki wa Tanzania na hasa muziki ule uliokuwa ukipigwa kuanzia miaka ya 60 mpaka mwishoni mwa miaka ya 90.

Kuna huyu mwanamuziki "nguli" ambaye kwa sasa yuko na bendi ya OTTU Jazz kwa jina Muhidini Gurumo ambaye alianza kazi ya muziki miaka ya 1960.

Amepitia bendi mbali mbali kama vile Afrikan Stars ya wakati huo (sio twanga pepeta), Kilimanjaro Chacha, Nuta Jazz, DDC Mlimani Park "Sikinde", Safari Sound "OSS" wana ndekule.

Licha ya umri mkubwa bado nyimbo anazotunga a mirindimo ya sauti yake ina radha ile ile. Kwa mtazamao wangu nadhani ni mwanamuziki wa kuigwa na hasa na hawa waimbaji wetu wa sasa ambao anaibuka muda mchache na baadae kimyaaa jumla!!

Big up mzee Gurumo.

=============

"Wakati wa ujana wangu mimi baba yenuuu…shati dukani shilingi sita unapata, kwa hivi sasa shilingi sita hata mkate hupatiii…" Kiitikio kikiwa; "Kwa hiyo wanangu tuishi kutokana na nafasi…"

Dar es Salaam. Katika kutambua mchango wa msanii Muhidin Maalim Gurumo kwa jamii na kuuenzi tutakuwa tukiwaletea mfululizo kuhusu nguli huyo, maisha, kazi ya muziki na mikasa kama alivyohojiwa na mwandishi wetu.

"Wakati wa ujana wangu mimi baba yenuuu…shati dukani shilingi sita unapata, kwa hivi sasa shilingi sita hata mkate hupatiii…" Kiitikio kikiwa; "Kwa hiyo wanangu tuishi kutokana na nafasi…"

Hiyo ni sehemu ya mashairi yaliyoimbwa na gwiji la muziki nchini Muhidin Maalim Gurumo zaidi ya miaka 12 iliyopita, akiwa na Bendi ya OTTU Jazz.

Ukweli wa maneno hayo kuhusu ugumu wa maisha unadhihirika hata leo ambapo mamilioni ya Watanzania wana maisha magumu ya kubahatisha kutokana na ufinyu wa kipato.

Hali hiyo inawakumba pia wanaofanya kazi, hata Maalim Gurumo mwenyewe ambaye amefanyakazi akiwa mwanamuziki kwa muda mrefu akisema: "Bado hakuna ninachoweza kujivunia kupitia muziki, hali ya maisha ni ngumu."

Historia ya maisha Gurumo anayefahamika pia kama Kamanda na mashabiki wa muziki ilianzia mwaka 1940 alipozaliwa, katika Kijiji cha Masaki Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.

Anaeleza kuwa baada ya kuzaliwa alipata elimu ya msingi, wakati huo pia akisoma madrasa, chuo cha kufundisha elimu ya Dini ya Kiislamu, lakini alishindwa kuendelea na masomo ya sekondari baada ya baba yake kufariki.

Mjomba chachu ya mafanikio

"Baada ya baba kufariki alinichukua mjomba wangu Selemani Sultani Mikole, wakati huo alikuwa akiishi maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam," anasimulia Gurumo.

Anaongeza: "Ukiacha mambo mengine, mjomba wangu huyo ndiye chachu ya mafanikio yangu katika kila jambo, licha ya awali kunizuia nisifanye mambo tofauti, zaidi ya kuijua dini."

Alipotakiwa kueleza iwapo historia hiyo ya maisha yake inahusiana na wimbo wa Ukiwa alioimba akiwa na Bendi ya Orchestra Safari Sound(OSS) katika mtindo wa Ndekule, Gurumo alisema;

"Ni kweli, wimbo huo una uhusiano moja kwa moja na mjomba wangu na maisha niliyonayo sasa, hata hapa ninapoishi ni yeye alinishawishi ninunue kiwanja hiki. Kwa sasa mjomba wangu ni marehemu, lakini enzi za uhai wake alikuwa akifuatilia mambo yote kuhusu maendeleo ya maisha yangu, namshukuru."

Yapo maelezo ya watu mbalimbali kuwa enzi za ujana wake kuwa Gurumo aliwahi kufanya kazi ya kuuza maji ya kubeba mabegani iliyotambulika enzi hizo kama ‘Mzega mzega.

Wasimuliaji wanaeleza kuwa alifanya biashara hiyo ikiwa ndiyo kazi yake ya kwanza baada ya kufika jijini Dar es Salaam kwa mjomba wake.

Je, nini ukweli wa maelezo hayo, Gurumo mwenyewe atasemaje? Fuatilia Jumamosi ijayo.

Mwandishi wa makala haya alimuuliza Gurumo: "Nasikia ulivyoingia jijini Dar es Salaam kazi yako ya kwanza ilikuwa kuuza maji kwa mtindo wa mzega mzega?

Kabla ya kujibu swali hilo Maalim Gurumo aliangua kicheko akitingisha kichwa na kujibu: " Sikuwahi kufanya biashara kama hiyo. Kama nilibeba maji kwa mzega, basi yalikuwa kwa matumizi ya nyumbani kwa mjomba."

"Hapo ndipo nilipofikia na kuishi kabla ya kuanza maisha ya kujitegemea. Nikiwa kijana wa nyumbani na kwa wakati huo sifa ya kujana ni kusaidia wazazi kutokana na heshima waliyokuwanayo vijana wa wakati huo."

Gurumo anaongeza: "Kazi ni kazi mradi mkono uende kinywaji, wakati huo hata kama ningepata kibarua cha kulima kwa mraba, ningefanya kwa kuwa nilikuwa kijana na nilikuwa natafuta cha kufanya ili aweze kuendesha maisha yangu."

Hata hivyo anasema kuwa umaarufu huambatana na mambo mengi ikiwamo watu wengi kujifanya wanakufahamu na kwamba hilo halimpi shida, cha msingi kwake wanaosema hivyo wakiwa ni mashabiki wake anapata faraja.

Anabainisha kuwa kwa enzi hizo hakukuwa na uhaba wa kazi kwani ajira zilikuwa nyingi na asingeweza kukosa kazi ya kufanya, lakini alichagua kuimba kwa kuwa ndiyo alichokiweza.

Kuingia kwenye muziki kwa siri akiwa na umri wa takriban miak 22.

Akizungumzia mwanzo wake kuwa mwanamuziki Maalim Gurumo anaeleza kuwa wazazi wake walikuwa wanamuziki waliopiga muziki wa kiasili wa Kabila la Kizaramo, hasa mama yake aliyepiga ngoma za aina mbalimbali na kuimba, hivyo yeye amerithi kipaji hicho.

Anasema kuwa alianza kujiingiza katika muziki kwa siri na kuimba akiwa chini ya himaya ya mjomba wake marehemu mzee Selemani Sultani Mikole.

Anaeleza kuwa alianza muziki kwa siri kutokana na ugumu wa kumweleza mjomba wake kuwa yeye ameamua kijikita kwenye muziki, akijua kwamba lingepingwa na mjomba wake, hata familia ambayo wakati huo zilikuwa bado hazijawa na mwamko wa masuala ya muziki kwa vijana wao hasa kwa yeye ambaye alikuwa akisoma Madrasa.

Bendi ya kwanza ya muziki wa dansi

Gurumo anasema kuwa bendi yake ya kwanza ilikuwa ni Rufiji Jazz iliyokuwa na maskani yake maeneo ya Fire (Faya) jijini Dar es Salaam.

Anaeleza kuwa ingawa bendi hiyo haikuwa maarufu, lakini hapo ndipo alipojifunzia muziki, akimwongopea mjomba wake kuwa anakwenda madrasa, huku akienda kwenye mazoezi ya muziki wa dansi.

Anasimulia kuwa katika mazoezi hayo alifanikiwa na kuanza kazi ya uimbaji huku pia akiweza kumshawishi mjomba wake kumwacha afanye kazi hiyo.

"Baada ya kujiunga na bendi hiyo ndiyo nilijua mikoa mingi ya Tanzania kwani tulifanya ziara mikoa mingi ikiwamo Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Tabora na Arusha. Wakati huo hapakuwa na upinzani mkubwa, ilikuwa kama amewasili mwanamuziki wa Zaire au kutoka nje,"alisema na kuongeza.

"Mashabiki walikuwa wakijazana kila tunapopiga licha ya kuwa baadhi ya mikoa ilikuwa na bendi zao, huko ndipo nilipozidi kupata ujuzi wa kuimba zaidi na zaidi."


CHANZO: Maisha ya nguli Muhidin Maalim Gurumo-1 - Habari - mwananchi.co.tz


Kipindi cha Mkasi



 
Last edited by a moderator:
Wakati wa ujana wangu mimi baba yenuuuu,
Shati dukani shilingi sita unapata,
Lakini sasa shilingi sita,
Hata mkate hupatiiiiii!

Kwa hiyo wanaangu muishi kulingana na wakati *2

Jiepusheni na anasa,
fanyeni kazi kwa bidii,
Kama kuna mkorofi,
Kati yenu aache mara mojaaaaa!

Dah! Kweli Gurumo anahitaji SENKSI za kufa mtu!
 
wakati wa ujana wangu mimi baba yenuuuu,
shati dukani shilingi sita unapata,
lakini sasa shilingi sita,
hata mkate hupatiiiiii!

kwa hiyo wanaangu muishi kulingana na wakati *2

jiepusheni na anasa,
fanyeni kazi kwa bidii,
kama kuna mkorofi,
kati yenu aache mara mojaaaaa!

dah! Kweli gurumo anahitaji senksi za kufa mtu!
twende kazi mazee!.........................
 
Wana-jf mimi ni mshabiki sana wa muziki wa Tanzania na hasa muziki ule uliokuwa ukipigwa kuanzia miaka ya 60 mpaka mwishoni mwa miaka ya 90. Kuna huyu mwanamuziki "nguli" ambaye kwa sasa yuko na bendi ya OTTU Jazz kwa jina Muhidini Gurumo ambaye alianza kazi ya muziki miaka ya 1960. amepitia bendi mbali mbali kama vile Afrikan Stars ya wakati huo (sio twanga pepeta), Kilimanjaro Chacha, Nuta Jazz, DDC Mlimani Park "Sikinde", Safari Sound "OSS" wana ndekule. Licha ya umri mkubwa bado nyimbo anazotunga a mirindimo ya sauti yake ina radha ile ile. Kwa mtazamao wangu nadhani ni mwanamuziki wa kuigwa na hasa na hawa waimbaji wetu wa sasa ambao anaibuka muda mchache na baadae kimyaaa jumla!! Big up mzee Gurumo.


....Ngurumo ni mmoja na wanamuziki wachache waliojaliwa sauti nzito na nzuri ya kuvutia nchini. Ni mwanamuziki wa kupigiwa mfano katika kuipenda na kuitumikia fani yake isipokuwa kwa kitu kimoja tu kibaya nilichokisikia mitaani (kama ni kweli)-inasemekana yule mzee anavuta bangi kwa kwenda mbele....ili kufanikisha kazi yake, na kwamba inamsaidia kweli kweli!😕
 
Xpin na wakuu wengine kama mnakumbuka line up ya Sikinde mwaka 1978. Gurumo, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Suleiman Mwanyiro, Michael "King" Enock, Juma Town, Hamis Juma "Maalim Kinyasi", Cosmas Thobias Chidumule.
 
<b><i>....Ngurumo ni mmoja na wanamuziki wachache waliojaliwa sauti nzito na nzuri ya kuvutia nchini. Ni mwanamuziki wa kupigiwa mfano katika kuipenda na kuitumikia fani yake isipokuwa kwa kitu kimoja tu kibaya nilichokisikia mitaani (kama ni kweli)-inasemekana yule mzee anavuta bangi kwa kwenda mbele....ili kufanikisha kazi yake, na kwamba inamsaidia kweli kweli! Ilikuwa zamani ndio alikuwa anavuta lakini kwa sasa Ngurumo ni SWALA TANO atumii ULEVI wa aina yoyote ile
 
twende kazi mazee!.........................

Nilipokwenda kwa mjomba,
Nilikutana na binamu yangu,
Na kwa kweli tulipendana,
Wazazi wangu walinikatalia tusioane,
Eti kwa sababu
Yeye ni mtoto wa mjomba,
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoaaa

Wazaziiiiii ninasema (WASEMAAAA)
nasononeka
Kwa vileeeeee msichana,
Nilimpenda.......

Utapata wako mwingine, naye utampenda,
Mtoto wa mjomba kufunga ndoa si vizuriiii!

Laligeni nahitaji na Senksi nyingine hapa kwa hii yuziful post! Hahaha!
 
Nilipokwenda kwa mjomba,
Nilikutana na binamu yangu,
Na kwa kweli tulipendana,
Wazazi wangu walinikatalia tusioane,
Eti kwa sababu
Yeye ni mtoto wa mjomba,
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoaaa

Wazaziiiiii ninasema (WASEMAAAA)
nasononeka
Kwa vileeeeee msichana,
Nilimpenda.......

Utapata wako mwingine, naye utampenda,
Mtoto wa mjomba kufunga ndoa si vizuriiii!

Laligeni nahitaji na Senksi nyingine hapa kwa hii yuziful post! Hahaha!

twende sasaaaaaaaaaaaaaaaa.....................

utakula senksi 24/7
 
<b><i>....Ngurumo ni mmoja na wanamuziki wachache waliojaliwa sauti nzito na nzuri ya kuvutia nchini. Ni mwanamuziki wa kupigiwa mfano katika kuipenda na kuitumikia fani yake isipokuwa kwa kitu kimoja tu kibaya nilichokisikia mitaani (kama ni kweli)-inasemekana yule mzee anavuta bangi kwa kwenda mbele....ili kufanikisha kazi yake, na kwamba inamsaidia kweli kweli!
Ilikuwa zamani ndio alikuwa anavuta lakini kwa sasa Ngurumo ni SWALA TANO atumii ULEVI wa aina yoyote ile

Konaball, this is good news! Kwa jinsi ninavyompenda mzee huyu ilikua inaniumiza kusikia anapuliza bhangi. Thanks....
 
....Ngurumo ni mmoja na wanamuziki wachache waliojaliwa sauti nzito na nzuri ya kuvutia nchini. Ni mwanamuziki wa kupigiwa mfano katika kuipenda na kuitumikia fani yake isipokuwa kwa kitu kimoja tu kibaya nilichokisikia mitaani (kama ni kweli)-inasemekana yule mzee anavuta bangi kwa kwenda mbele....ili kufanikisha kazi yake, na kwamba inamsaidia kweli kweli!😕

Tuache uoga bangi ni mitishamba ambayo kama inatibu maradhi yako ina ubaya gani? Sio kila kilichopigwa marufuku na serikali hakiwasaidii watu acha watu watumie mitishamba kwa ajili ya afya zao! Serikali hiyo hiyo inasema haiamini mambo ya uchawi lakini nyakati za uchaguzi kama tutakavyoona mwaka huu, magari kibao ya serikali yatakuwa yanakwenda Bagamoyo kunani?
 
Xpin na wakuu wengine kama mnakumbuka line up ya Sikinde mwaka 1978. Gurumo, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Suleiman Mwanyiro, Michael "King" Enock, Juma Town, Hamis Juma "Maalim Kinyasi", Cosmas Thobias Chidumule.
Safi kabisa mkuu, ila umemsahau Hassan Rehani Bitchuka "sterio".
 
twende sasaaaaaaaaaaaaaaaa.....................

utakula senksi 24/7

Ukiwa ulionipata mkubwa,
baada ya kufariki wazazi wangu,
Alinichukua mjomba,
Kaka yake mama yangu,
Alinilea mpaka nimekua,
Alinisomesha mpaka nikamaliza,
Alinifanyia mpango nami ili niishi vizuri,

Lakini ndugu zake babaaa....... Wananipakaziaaaa!
 
Tuache uoga bangi ni mitishamba ambayo kama inatibu maradhi yako ina ubaya gani? Sio kila kilichopigwa marufuku na serikali hakiwasaidii watu acha watu watumie mitishamba kwa ajili ya afya zao! Serikali hiyo hiyo inasema haiamini mambo ya uchawi lakini nyakati za uchaguzi kama tutakavyoona mwaka huu, magari kibao ya serikali yatakuwa yanakwenda Bagamoyo kunani?

Serikali kupiga marufuku matumizi ya bhangi si kwamba inawaonea wivu au kwa sababu nyingine yoyote...,ni kutokana na madhara ambayo yamethibitishwa kisayansi kwamba bhangi ni kama madawa ya kulevya mengine- Heroin, Mandrax, etc, hata kama in the short-run yanaweza kuonekana kama yanakusaidia..in the long-run yana athari kwenye ubongo wako.

Kuhusu hilo la uchawi ni swala lingine tofauti kabisa ambalo nawaachia wengine wachangie...
 
Nilipokwenda kwa mjomba,
Nilikutana na binamu yangu,
Na kwa kweli tulipendana,
Wazazi wangu walinikatalia tusioane,
Eti kwa sababu
Yeye ni mtoto wa mjomba,
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoaaa

Wazaziiiiii ninasema (WASEMAAAA)
nasononeka
Kwa vileeeeee msichana,
Nilimpenda.......

Utapata wako mwingine, naye utampenda,
Mtoto wa mjomba kufunga ndoa si vizuriiii!

Laligeni nahitaji na Senksi nyingine hapa kwa hii yuziful post! Hahaha!


Mkuu Crispin, hapa kidogo umechanganya somo. Hili Goma la 'Mtoto wa Mjomba' la miaka ya mwishoni ya Sabini lilipigwa na Urafiki Jazz Band wana Chakachua Ngoma wakiongozwa na 'Ngulimba wa Ngulimba' Mrisho huku mwimbaji mmojawapo kama sijakosea sana akiwa Cosmas Chidumule.
 
Labda nikupoze kidogo kwa hili kipande cha 1982 cha Gurumo na wana Sikinde 🙂:

'mapenzi hayana kificho,
yaingiapo Moyoni mwangu,
mwenye mapenzi haonii ingawa macho aanayo,

Mtu chake apendacho,
hakina ila machoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani,
 
Mkuu Crispin, hapa kidogo umechanganya somo. Hili Goma la 'Mtoto wa Mjomba' la miaka ya mwishoni ya Sabini lilipigwa na Urafiki Jazz Band wana Chakachua Ngoma wakiongozwa na 'Ngulimba wa Ngulimba' Mrisho huku mwimbaji mmojawapo kama sijakosea sana akiwa Cosmas Chidumule.

Hivi Gurumo hakuwepo humo? Kuna jisauti lake hapo, hebu vuta memori kiaina!
 
Hivi Gurumo hakuwepo humo? Kuna jisauti lake hapo, hebu vuta memori kiaina!

ha ha haa, hakuwemo mkuu na hakupata kuimbia Urafiki Jazz! Kipindi hicho Gurumo alikuwa Juwata akitamba na Super Sterio Bitchuka na na vitu kama:


'kijana una umbo la kupendeza,
mrefu mnene, na mwanya wa wastani,
hakika uzuri si shani,
utu wa mtu ni tabia njema...



Inakukumbusha mbali eh?
 
Nilipokwenda kwa mjomba,
Nilikutana na binamu yangu,
Na kwa kweli tulipendana,
Wazazi wangu walinikatalia tusioane,
Eti kwa sababu
Yeye ni mtoto wa mjomba,
Ndivyo ilivyokuwa vigumu kwetu kufunga ndoaaa

Wazaziiiiii ninasema (WASEMAAAA)
nasononeka
Kwa vileeeeee msichana,
Nilimpenda.......

Utapata wako mwingine, naye utampenda,
Mtoto wa mjomba kufunga ndoa si vizuriiii!

Laligeni nahitaji na Senksi nyingine hapa kwa hii yuziful post! Hahaha!

Saafi sana kwa kumkumbuka Ngulimba wa Ngulimba Juma Mrisho na Chaka Chua (Urafiki Jazz)
 
Lwikunulo: Bangi ni kitu cha kawaida sana ili mradi usiinuizie kwa mabaya. Wengi waliofanikiwa katika dunia hii wamevuta majani, mfano: George na Laura bush, Barak na Michel Obama, Bill Clinton, n.k. Ufisadi ni mmbaya zaidi kuliko bangi hasa ule unaofanywa na watu wakiwa macho makavu kama RA...
 
Back
Top Bottom