---maisha ya "njozi za kutisha"--

...are you the victim of your own success? are you living your dream or are you living a nighmare?

Yes, you could be a victim of your own success if your heart open up to absorb the pain from others.
Je? Unawezaje kuwa na furaha wakati ndugu zako bado ni fukara na wenye umasikini kupindukia? Je? Utajitahidi kuwasaidia au utawaacha na baadaye kukosa usingizi wakati roho yako inakusuta kwani hata wewe umetoka huko?

una usongo wa mawazo unaotokana na majukumu ya kazi, familia, ie---ndugu, jamaa na marafiki? huna muda wa kufurahia mafanikio yako kielimu, kazi/biashara?... kipato hakikutoshi majukumu ya jamii inayokuzunguka?

Unaweza kuepuka hali hii kama utaweza kujua limits zako na kukubali yale yaliyo ndani ya uwezo wako.

...njia gani muafaka za kuutua mzigo huu wa kuwa tegemeo la familia ili angalau upate kufurahia mafanikio ya kisomo chako, ndoa, familia na maisha kwa ujumla? ...kwani ni lazima uilee familia na ukoo mzima kwakuwa tu una kazi inayokulipa vizuri?

Muda muafaka wa kuutua mzigo huu ni leo, lakini sio kuutupa mzigo ila ni kuutua taratibu ukijaribu kusaidia kadri ya uwezo wako na ndani ya malengo yako. Wema usizidi uwezo na malengo.
 
Hahaha...haya bana.

Tulizo nimekusoma, nitarudi kujibu hoja zako..pamoja na
Maswali ya nyongeza..
Wakati unakuja kujibu usome na hiki kisa......

Ayabau alikuwa rafiki yangu (RIP)
Huyu bwana aliamua na kuapa kabisa kuwa hatakunywa pombe wala kufanya starehe yoyote ile mpaka atakapojenga kibanda chake na kununua kibajaji chake cha kutembelea.........ndani ya miaka mitatu lengo likatimia. Akakamilisha kakibanda kake maeneo ya Bunju na kumiliki ka-Raum kake ka mtumba toka Japan......... Siku anahamia kwake aliangushwa ng'ombe wanaume tukakesha na mabia ya moto na ya baridi......

Wiki ya pili tangu ahamie Ayabau na baadhi ya marafikize wakawa wameketi Bar moja iliyo pembeni mwa barabara ya Bagamoyo maeneo ya Boko. Lori lililokuwa linatokea Bunju kuelekea Tegeta likachomoka tairi ghafla...... Ile tairi ilitumwa na Ziraili imfuate Ayabau pale alipoketi na marafiki. Ayabau aliliona tairi likimjia akanyanyuka ili alikwepe..........maskini tairi likagonga gogo na kumrukia kichwani........ Akakimbizwa hospitalini na marafiki zake kabla marafiki hao hawajapewa habari kuwa Ayabau alikwisha fariki kitambo.........Inauma sana. Marehemu akimuacha mkewe na ujauzito na binti mmoja....

Balaa sasa....huyu shem yetu hii nyumba aliyoachiwa na marehemu mumewe imekuwa danguro hata miaka mitano haijapita tangu mmewe ashindiliwe na dongo la takribani tani saba.......Imagine jamaa alivyojitesa kwa miaka mitatu mfululizo akitembelea mashati yaliyobabuka na kuchanika kwenye ukosi, akishinda mchana bila kula, akisaidiana na vibarua kupandisha matofali ili mafundi wamjengee nyumba yake.......

FUNZO: Maadamu hujampigia Mungu simu akueleze utakufa lini....... Maisha yako ni Leo! Enjoy!!!

RIP Ayabau! Msamehe mkeo, si kosa lake!
 

Bwana apewe sifa ndugu Asprin
 
Babu umeongea point ya muhimu sana, ishi maisha yako leo. Believe me kila mtu anatamani hilo lakini sometimes unajikuta 'sumaku' ya majukumu inakung'ang'ania tu ng'ang'ana, ng'ang'ana!

Mbu hili lisredi lako hata sijui kwa nini umelileta damn !!!
 
MBu.... i am a very ambitious person... everyday i lay a new foundation and platform that is killing me, but you know why?? Its because our life is a program; we are just the windows or processes or at least processors to the program.

whatever we do, is just another system upgrade, adn if one wants to live happily then he/she has to choose obsolete role, which in some cases could be a screw, knob (touched only twice per cycle etc).

with increased demand from loved once, we push ourselves to the limit ... expecting a happy and super reward!!! I wont stop now, i see all the rewards, i wont stop now coz the more nightmares i have the more power and choices come thereafter

The only think i need to balance now is the targets vs. family and friends so that my equilibrium returns to normal, as for now it is shifted towards success.... and somehow affecting my loved ones

nice thread bro

MTM
 
...kwanza nawapa pole wale watumiaji wa blackberry leo...simu zenu leo zime myuti internet ee? msijali, baada ya nusu saa tatizo litakuwa sorted
source; BlackBerry data services suffer massive outage | Business of IT | ZDNet UK


Babu umeongea point ya muhimu sana, ishi maisha yako leo. Believe me kila mtu anatamani hilo lakini sometimes unajikuta 'sumaku' ya majukumu inakung'ang'ania tu ng'ang'ana, ng'ang'ana!

Mbu hili lisredi lako hata sijui kwa nini umelileta damn !!!

...e bana tulizo naelewa bana...hebu fikiria mdada kamaliza chuo, kapata ajira....anajitahidi maskini kukabiliana na maisha yake na kazi inayomlipa vizuri tu...ila tatizo linakuja kwakuwa yeye ni wa kwanza kuzaliwa, inambidi awasomeshe wadogo zake...wakati huo, jukumu la kuishi nalo mjini ni lake pia...---ina maana anawahudumia kuanzia malazi, chakula, school fees, transport & pocket money...na mazaga zaga mengine mengi...

kama hiyo haitoshi, inambidi pia apeleke kamchango kukarabati kibanda cha biashara cha mstaafu...
shukuru mungu iwapo atakuwa na mume mwelewa, lakini hapa tunaweza kuta mume naye keshaweka biti huo mzigo atajielewa yeye na wazazi wake....

mdada huyo atautua vipi taratibu mzigo kama huo bana? acheni tu....msiwaone watu na mabonge ya ma smile usoni...wengine wanaugulia!
 

Mbu we umeamua kuchokoza machungu ya watu wewe, ukipigwa mie sitokusaidia ujue.


Bwana ni kweli kabisa tena kuna kitu umezungumzia .......laana.....mtu mwenye majukumu ya kusomesha ndugu zake hata kama wazazi/mzazi wake anao uwezo huo huwa mara nyingi wanahofia laana. Yaani zile za ...........mimi nimekusomesha wewe ili uwasaidie wadogo zako. Mbaya zaidi ni kuwa wazazi wengi husahau kuwa kama wanauwezo bado ni jukumu lao kutekeleza malezi ya walio wadogo but huchukulia tu kuwa wewe ni wa kwanza na nilikusomesha (hata kama alikusomesha kwa manyanyaso) bado tunajikuta tu unalazimika.

Sasa kama ulivyouliza hapa Mbu, hebu imagine maisha yote unamuishia/waishia wengine!! Say ndo umemaliza chuo ukapata kaajira kako! Hijamalizia kulipia jiko la mchina (Stove) ujipangie kachumba kako, hao unaletewa ndugu, mmoja au wawili uwasomeshe kwa hako kamshahara kako. Unasomesha........na si school fees tu, bali malazi, chakula, pocket money e.t.c na bahati mbaya pengine ndo mmepishana umri wazazi walitumia nyota ya blue ndio unaanza kusomesha tangu high school, chuo (kama walinahatika kufaulu vema other wise ndo unaanzia na Certificates, Diploma mpaka degree - hakuna cha mkopo wa serikali wala mdogo wake Fince!

Umri unasonga nawe unahitaji kuoa/olewa uwe na familia! Hapo sasa unazidi kuufanyia makato mshahara.......ah...Hii hadithi Mbu mi ctaki.

Hivi kuna namna unayowezapunguza haya makali ya ukata kweli?
 
mimi nimeweza siku hizi kuzima simu kwa siku nzima......inaondoa stress zote.....trust me...
Siku nzima the boss utakuwa selfish, kuna watu wanahitaji wakati mwingine msaada wako kama wewe utakavohitaji wakati mwingne, unless upo mbali au uko holiday maybe au imekaaje hii
 
Reactions: Mbu
Babu umenikumbusha mbali, RIP marehemu
 
Mkuu nakubaliana na wewe….

Lakini ukiacha wale ambao wanaona majukumu ya kusaidia ni moja ya kulipa fadhila.. Pia kuna wale ambao majukumu hayo ni moja ya sehemu ya maisha yao mfano wale ambao tumetokea kwenye familia zilizopitia misukosuko ya ndoa.. Mkuu, mimi binafsi nikiwa kiumbe wa kwanza, nilisha-crash na kutaka ku-surrender kwa Mola baada ya majukumu kufika shingoni, ila namshukuru sana rafiki yangu wa Kike ambaye alibaini njama zangu na kunipiga stop..Anyway, huyu bint siwezi kumsahau na ndio maana nilikataa kumwoa na kuwa mke kwani niliogopa majaribu ya kuvunja Moyo wake hapo baadaye. Naamini huyu bint alishachukua nafasi ya Mama kunirudisha duniani kwa mara ya pili… Anyway…




Kama nilivyosema hapo juu.. Ukiacha fadhila ambayo unaweza kuipumzisha kwa muda kama Wazazi wana uwezo. Kuna historia ya maisha ya nyuma ambayo inafanya majukumu kuwa automatically part n' parcel ya maisha.. Si unakumbuka hata Baba wa Taifa alisema Tanzania haitakuwa huru hadi Afrika yote iwe huru.. Lakini hapa yataka uangalifu kwani unaweza kumaliza rasilimali kuwasadia wengine wawe huru nawe binafsi kurudi kwenye umasikini kama ilivyotokea kwa Tanzania.. Ndiyo maana nilisema wema usizidi uwezo…

kama hiyo haitoshi, inambidi pia apeleke kamchango kukarabati kibanda cha biashara cha mstaafu...


Fadhila hizo Mkuu..lakini angalia pia na utamaduni wetu.. Kwani huko nyumbani Jamii haina sehemu za kutunza wastaafu (Wazee) kama ilivyo kule ulaya ambako Wastaafu wao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatunzwa kwenye viota maalumu ambavyo vinatusaidia sisi wengine kupata vibarua.. Lakini mkuu Je? Utawezaje kupata usingizi wakati umepata ajira ya kubadilisha mboga na unajiandaa kuama chumba kimoja lakini yule mstaafu ambaye alikubali kutukanwa na baniani ili mimi nipate ugali na mlenda anaangaika kuomba ulanzi na Komoni kule Ileje nyanda za juu.. Nadhani utajitahidi kumfungulia ka- baa ka ulanzi na komoni ili kiasi fulani anywe na kingine apate hela ya kutambia wenzake wakati wanakunywa ulanzi..

shukuru mungu iwapo atakuwa na mume mwelewa, lakini hapa tunaweza kuta mume naye keshaweka biti huo mzigo atajielewa yeye na wazazi wake....


Ni kweli yataka moyo..hasa ikiwa kati yenu mmoja ameishi maisha ya Magharibi na mwingine ameishi maisha ya Mashariki… Lakini Pia..kuna asilimia chache ya wapenzi ambao wanahisi machungu ya wapenzi wao..

mdada huyo atautua vipi taratibu mzigo kama huo bana? acheni tu....msiwaone watu na mabonge ya ma smile usoni...wengine wanaugulia!


Tutamsaidia kumwambia wengi tumeishi hayo maisha.. Tulishataka kutafuta Shortcut..Lakini tukarudi njiani na kuendelea kupigika na kumwomba Mola aepushe kikombe chake na Majaribu… Mola ametusikiliza lakini sometime Yes..usione tuna smile usoni..Lakini bado tunaugulia moyoni.. Misekule ya dhiki inaendelea kutuandama wakati tunafikiri wenzetu wengi wanaendelea kuteseka na majukumu ambayo hawawezi kuyatua!
 
Nimejifunza mengi katika thread hii. Asante Mbu!
 
Reactions: Mbu
Babu umeongea point ya muhimu sana, ishi maisha yako leo. Believe me kila mtu anatamani hilo lakini sometimes unajikuta 'sumaku' ya majukumu inakung'ang'ania tu ng'ang'ana, ng'ang'ana!

Mbu hili lisredi lako hata sijui kwa nini umelileta damn !!!

Utajua baadae!
 

If you live within your means , you lack imagination

It is easy to get comfortable in life, and tick all the boxes for example I have a job, a wife and a family. But life is not about comfort it is about growing, and growing beyond yourself. So if you are living within yourself, you are not challenging yourself, are you making a contribution to our planet. If you are not challenging yourself you are not growing, if you are not growing... what are you doing. Can you use your imagination and challenge yourself and live beyond yourself? It is the people like Nelson Mandela, Gandhi, Albert Einstein who were ordinary but used their imagination to challenge themselves... and look at what they have done by using their imagination.

( nimejaribu ku explain huo usemi , ntarudi baadaye kuonganisha na topic )

sante Mbu..
 
Reactions: Mbu

...tulizo umeijibu vizuri....hakuna njozi mbaya hapa...
tunaishi kwa matumaini ipo siku mungu atatulipia, au nimekuelewa vibaya?

maana waswahili tuna misemo mingi ya kutishana...utasikia "damu nzito,....!"
ukishajitolea unaambiwa "tenda wema wende zako,.......!"

wakati unashangaa shangaa unajikuta na msemo "mtumai cha ndugu,....!"
 



...are you the victim of your own success?
are you living your dream or are you living a nighmare?






Nimeipenda saana ya huyu mzee na hayo maneno... So touching and so true...

Mbu tukizungumzia jamii yetu nafikiri na level ya maisha yetu pia huchangia saana... Mtu toka anakua yaana mambo yalomzunguka yoote yaonesha hali ya kutegemeana. Katika jamii yetu ukiwa masikini ni shida; hapo hata raha hufikirii na the way maisha yamepanda... Ukiwa na uwezo shida pia maana ujue wee ndo utalea familia yenu yoote kama sio ukoo...

Hata hivo nieme observes saana kua nikitolea mfano jamii zetu hapa; Watu wengi hutumia pesa nyingi saana bila wao kujua kua hufanya hivo... acha kwa yalo muhimu na basic kwa maisha yake... yale ya ziada.... kama un-neccessary mahitaji... nguo, viatu, kofia, accessories bila mpangilia... acha michango mtaani, kazini, kundini kwenye clubs... yaani you name it! Pesa ambazo angeweza hata weka akiba ya badae kupunguza the inevitable stresses za badae.... (sijui nimeenda off point hapa??)
 
yaleyale! unakufa afu pensheni yako mume anatumia kulipia mahari mwenzie (bora isiwe ile small house yake,mweh)
 

Nimekupata Mkuu..sometime hiyo misemo inachanganya sana..Kikubwa naamini kuwa chochote unachofanya kama unaamini uko sahihi basi uko sahihi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…