Tulizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 848
- 664
...are you the victim of your own success? are you living your dream or are you living a nighmare?
Yes, you could be a victim of your own success if your heart open up to absorb the pain from others.
Je? Unawezaje kuwa na furaha wakati ndugu zako bado ni fukara na wenye umasikini kupindukia? Je? Utajitahidi kuwasaidia au utawaacha na baadaye kukosa usingizi wakati roho yako inakusuta kwani hata wewe umetoka huko?
una usongo wa mawazo unaotokana na majukumu ya kazi, familia, ie---ndugu, jamaa na marafiki? huna muda wa kufurahia mafanikio yako kielimu, kazi/biashara?... kipato hakikutoshi majukumu ya jamii inayokuzunguka?
Unaweza kuepuka hali hii kama utaweza kujua limits zako na kukubali yale yaliyo ndani ya uwezo wako.
...njia gani muafaka za kuutua mzigo huu wa kuwa tegemeo la familia ili angalau upate kufurahia mafanikio ya kisomo chako, ndoa, familia na maisha kwa ujumla? ...kwani ni lazima uilee familia na ukoo mzima kwakuwa tu una kazi inayokulipa vizuri?
Muda muafaka wa kuutua mzigo huu ni leo, lakini sio kuutupa mzigo ila ni kuutua taratibu ukijaribu kusaidia kadri ya uwezo wako na ndani ya malengo yako. Wema usizidi uwezo na malengo.