Maisha ya shule na matukio yake yenye kufurahisha

Nfumu

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2016
Posts
610
Reaction score
698
Kama hukuwahi kusomea shule zetu zileee basi kwa namna moja au nyingine utakuwa hufahamu mambo mengi sana

maisha ya shule(msingi na upili) yalikuwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kupewa adhabu za kuchimba visiki,kushika masikio, kichurachura ,kuzoa taka ,kwenda na chelewa shule lakini haikuondoa makundi ya watu wafuatao

1.watoro sugu mashuleni
2.wambea
3.watukutu walioshindikana
4.bakibencha kupunguza utukutu
5.makomedi wa darasa hata kama mwalimu yupo darasani
6.watoro wa rejareja kila siku kisingozio kikiwa nilikuwa naumwa

Binafsi nilkuwa nafasi ya 4 na ya 5

Lakini pamoja na hayo wanafunzi hawakufeli na waliendelea na masomo yao zaidi
na kufikia malengo yao walioyatarajia

Je wewe ulikuwa kundi gani katika maisha ya shule kuanzia primary hadi high level
 
Bana weeee umenkumbusha mbali Sanaaaa mara sec
Sku1 parade walkua wanakagua soks af nlkua sina bas nkapiga zangu mfuko ile meusi mguuni mara s condmaster huyuapa em pandisha suruale... Kucheki c akaona kitu kinan'gaa alnipiga bakora stasahau
always tulkua tunachit ivo ila ule mfuko ulkua na mafuta ya mandaxi so ulkua unangara ataree
 
Daaah! yaani nimekumbuka jamaa yangu anaitwa mgaya aliiba kiti cha shule nyakati za jion walinzi walipo muona walimkimbiza mpaka kwao na kumkamata ..Ilikua gumzo sana.
 
Daaah! yaani nimekumbuka jamaa yangu anaitwa mgaya aliiba kiti cha shule nyakati za jion walinzi walipo muona walimkimbiza mpaka kwao na kumkamata ..Ilikua gumzo sana.
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nikiwa form 4 kwenye mitihani ya mwezi wa tatu aiseee. Basi ijumapili usiku nikajifungia ndani toka saa 3 nikapiga pindi la Biology tulikua bado tumesoma Growth tu aisee nikameza kila kitu. Nikajua kesho naenda kuua saa nane nikalala sasa nimepiga pindi la masaa 5.
Asubuhi nimefika shule tukaingia ndani tukapewa na paper. Ile namalizia kuandika jina second master akaingia nikasikia "Ray van Boy toka nje" daah nikaumia, kumbe ijumaa kunaadhabu alinipa sikumaliza halafu nilikua nimesahau. Akasema ananipimia futi tano za eneo nilime nikimaliza ndio niingie darasanii. Weeeee nililia kama litoto nikifikilia muda niliotumia kusoma ndio nachoka kabisa. Ikabid anipe mboko 4 kwanza kuniweka makalio vzr then tukaenda kupima sehem ya kulima tena mlimani pakavuuuu ukipiga jembe panadunda. Basi akaniruhusu niende drsn bado dk 20 . Kuingia class nakuta maswali yote nayaweza wacha nihangaike sijui nijibu lipi. Mara najibu true and false kidogo nimelukia multiple choice mara Eseay nkachoka. Jasho lingi sana viganjani. Mtihani ukaisha nikaambulia 30%
 
Umesahau
7. Ulevi na kula wida
8. Wale wa kutupia guso/ugoro
9. Wizi stoo ya shule.
10. Mapenzi

Aseeh acha tu.
11.wapole/wakimya
Yani hawa mwaanzo hadi mwisho wa vipindi yeye ni kimyaaaa,hawanaga marafiki/makundi
 
ha hahaa
 
Kuna mdau mmoja alikuwa anatokea Mtwara , sasa bhana kulikuwa kuna madam mmoja wa kichaga alikuwa anatufundisha BAM na alikuwa mnaa sana kila siku alikuwa anaalika staff nzima kuja kutushushia bakora kwa kutusingizia tumemdharau,
Yule jamaa wa mtwara akahamia siti za mbele ikawa kila madam akiingia tu kufundisha jamaa anajamba kila baada ya dakika tano , madam ilibidi ahamie PCM kufundisha,
Watu wa mtwara sio wa mchezo mchezo.
 
kufuta ice cream au pipi kijiti kwa kutumia nywele kisha unaanza kuila bila kujali ilikuwa mdomoni mwa mwenzako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…