Maisha ya urafiki na jambazi la kike chuoni

Maisha ya urafiki na jambazi la kike chuoni

Kuna siku katoka likizo Arusha kuja chuoni, siku hiyo aliingia mida kama saa saba usiku akiwa na ngeu, michubuko nikamuuliza Vip akasema amekutana na majambazi kama watano hivi usiku huo walitaka kumpora simu na hela ikabidi apambane nao kama lisaa hivi hadi majambazi yakakimbia. Kweli jamani tangu hapo nikaona huyu mtu hafai kuwa rafiki yangu maana kuna siku atanichenjia
 
Kamwenee bee, miaka hiyo natoka advance nikaomba course ya law chuo flan cha serikali. Nashukuru Mungu sana nikipata. Time ile tuliripoti chuo kama sikosei mwezi wa kumi hivi, basi kufika chuoni rasta nilikuwa mwenyewe tu, enzi hizo marasi hatukuwa wengi. Ila tulikuwa wale marasta by nature sio hawa Wa siku hizi wa fashion.

Basi ile wiki ya pili chuoni akaingia mwana chuo kutokea kaskazini (akitoka kazini) huyo ni mwanamke wote Tupo class moja, akavutiwa nami vile alijua sio mtu wa mambo mengi na wala sio sista duu,

Akanambia Vip Ras vyombo unapiga wap nikamwambia aah mi sio wa vyomboo saana, akasema fresh basi Jion tuonane pub flani nikamjibu fresh.

Kweli jioni nikaingizana maeneo alioniambia nikamkuta anatandika vyombo sio vya nchi hii, value +konyagi anachanganyia humo humo nikasema dah, fresh nikapiga japo kwa kujikaza sana.

Baada ya muda urafiki ukakolea sana, kuna siku Tupo na wana class wenzetu tumekaa tunamimina vyombo ghafla mtaa huo huo tukasikia kelele kumbe za wizi bana, mdada akachomoka kama mshale hapo keshapiga zile value za chupa Saizi ya kati zaidi ya nne hivi akaelekekea eneo la tukio. Kilichotuacha hoi ni Vip yule dada kupigana na majambazi manne tena ya kiume hadi hao majambazi kukimbia wote tulimuogopa kwa kweli.

Mi sikutaka urafiki nae hata japo alikuwa akinilizamisha tu hasa ile wikiendi tutoke wote, mi nilimuogopa vile sijawahi kumuona akiwa emevaa gauni wala sketi wala kwenda kanisani kwa muda wote huo tuliokuwa nae pale chuoni.

Pili mawasiliano yake, alikuwa akipigiwa simu nyingi kutoka kwa wanaume na alikuwa akiongea mikato mikato ili mtu wa pembeni usielewe.

Kilichofanya nikakata urafiki nae kabisa kuna wizi ulitokeaga bank fulani hivi na hiyo wiki alikuja hosteli kwangu tule maisha lakini akaniambia anaweza safiri kama siku mbili tatu hivi, na katika hizo siku akiwa kwangu alikuwa anatamka maneno maneno yanayohusiana na benki na ujambazi akiwa anaongea na simu na kweli baada ya muda ndo huo aliosafiri wizi ukatokea katika bank hiyo.

Niliuchuna kama sio mimi na nikamfungia vioo baada ya kugundua ni jambazi Sugu la kike tena linalokunywa mapombe yote makali hata bia hawezi kunywa anasema hizo ni soda, Huku linasoma sheria.

Tuweni makini sana na marafiki tunaowapata jamani bila kuwa makini angeniingiza kwenye ujambazi na mimi
Nimejikuta nacheka sana hata sijui kwa nini
 
Kuna siku katoka likizo Arusha kuja chuoni, siku hiyo aliingia mida kama saa saba usiku akiwa na ngeu, michubuko nikamuuliza Vip akasema amekutana na majambazi kama watano hivi usiku huo walitaka kumpora simu na hela ikabidi apambane nao kama lisaa hivi hadi majambazi yakakimbia. Kweli jamani tangu hapo nikaona huyu mtu hafai kuwa rafiki yangu maana kuna siku atanichenjia
Mapolisi wengi huwa wanashiriki mishe za ujambazi ili wawapate vyema wahusika.
Mengine siwezi ongea hapa, kuna watu tuna fahamiana.
 
Ungefanyiwa recruitment kwenye chama lao,aliona sura yako imekaa kijambazi akaona unawafaa
 
Ila huu uzi unafurahisha😂😂😂😂😂
 
Umenikumbusha demu mmoja wa kujiita mkush naye anasoma sheria ni kama lijambazi alina kiuno
 
Hivi kwa nn arusha kuna majambakuzi yaliyoshindikana embu tupeni kinaga ubaga wajuzi
 
Back
Top Bottom