Maisha yaanza kumnyokea Idris Sultan

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amesema ameanza kuingiza faida kutokana na uwekezaji aliyoufanya baada ya kutoka kwenye shindano la hilo ambalo lilimpatia zaidi ya Sh500 milioni.

Akizungumza na Bongo5, Idris alisema tayari ameanza kuona faida ya pesa ambazo aliwekeza kwenye biashara zake.

“Kwa sasa hivi matunda nimeanza yaona, kuna kipindi fulani nilikuwa sitoki sana, watu wakasema Idris amepotea kwa muda mrefu, hicho ndo kipindi ambacho nilikuwa busy kuweka mambo sawa, unajaribu kufanya hichi, unajaribu hichi ilimradi kuweka mambo sawa,” alisema Idris.




“Kwa hiyo sasa hivi ndiyo naona inshallah mambo yameanza kunyooka. Kazi zinaanza kutoa malipo ambayo yalitakiwa yatoke tangu zamani, lakini biashara zimechukua muda mrefu kidogo kutoa yale malipo ambayo yalikuwa yanastahili,”

Pia Idris amesema kwa sasa anafurahia kazi yake mpya ya utangazaji ambayo anafanya Choice FM.

Chanzo: Bongo 5
 
Alafu kiredio chenyewe kile kimeanza kukosa mvuto, hata wasikilizaji wamepungua
Choice FM ni zamani... Sasa hivi full kiswahili. Itaanza kushindana na clouds sasa
 
Choice FM ni zamani... Sasa hivi full kiswahili. Itaanza kushindana na clouds sasa
Sijui nani aliowashauri iwe hivo,imekua mbaya,wanapiga ngoma kama za clouds tu..niw nimehamia tbc international na kiss fm mchana naskiliza magic..choice wanaiharibu wenyewe
 
Sijui nani aliowashauri iwe hivo,imekua mbaya,wanapiga ngoma kama za clouds tu..niw nimehamia tbc international na kiss fm mchana naskiliza magic..choice wanaiharibu wenyewe
Hata sijui niende wapi.. East Africa walibadilika, Choice nao ndo hivyo... Yani majanga tuu... Wamepoteza mwelekeo.
 
CEO Wa kampuni yenye faida anahamka SAA kumi kwenda kwenye ajira akitoka SAA nne Na hizi foleni uchofu masaa zaidi ya Saba atakuwa anamtumikia mwajiri wake kama kampuni Yake inafaida kwa nini asisimamie kampuni Yake awe anaenda huo muda Wa kazini ofisini kwake si angekuwa Na mafanikio Mara mbili maisha aya aya tusidanganyane
 
Kuna wadada wa bongo huwa ni wazee wa kuwai frusa. Hiv wamemuachia hata kaa vists kwel? Maana madam alikuwa anamfungia ndan tu kila kitu anamletea Ata biashara atakuwa amewekeza kw a madam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…