Naisujaki Lekangai
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 1,340
- 1,377
Naandika hii baada ya habari ya kijana mmoja jirani yetu anayefanya kazi Tanga kutangaza kwamba baba yake kamloga ndio maana maisha yake hayaendi vizuri.
Niliwaza na kushangaa sana niliposikia habari hii maana kijana mwenyewe na baba yake nawafahamu vya kutosha.
Kijana anafanya kazi bandarini Tanga ana mshahara mzuri.Pamoja na kuwa na kazi maisha ya huyu kijana ni ovyo: ni mlevi wa kupindukia haondoki baa mpaka ifungwe, kila akiishi na mwanamke mwanamke huyo humkimbia baada ya muda mfupi, na vurugu nyingine nyingi za maisha kama kushindwa kulipa kodi ya chumba anachoishi na kufukuzwa kisha kuomba kuishi kwa marafiki.
Nilikutana na huyu kijana mjini Moshi akiwa njiani kwenda kwao Arusha.Alikuwa amechakaa sana kiafya, kijana wa miaka 34 utafikiri mzee wa miaka 55, amevaa ovyoovyo, ikabidi nimwulize nini cha mno."Wacha tu dada Nai", alianza,"Baba ananifanyia mambo mabaya sana"
Nilipomwuliza zaidi akanieleza kwamba baba yake anamloga na maisha yake si mazuri hata kidogo kwa sababu ya kulogwa na baba.
Nilistuka kusikia hivyo nami nikamchunguza zaidi. "Wee Lazaro wee acha kumsema baba yako namna hiyo. Tangu lini mzee Menyooki akawa mchawi?"
Ndipo aliponifafanulia. Eti kwa kuwa baba yake ana maboma matatu ya ng'ombe huko Oldonyosambu kwa nini baba anataka Lazaro amtumie hela? Kwani hizo ng'ombe hazimtoshi?Na akaendelea kunieleza kwamba hajawahi kumtumia baba yake hata senti moja, na kwa ajili hiyo baba yake amemloga ndio maana maisha hayamwendei vizuri.
Lazaro aliniaga kwa harakaharaka na kupanda costa kuelekea Arusha.
Msomaji, hebu nisaidie kuwaza. Je ni kweli mzee Menyooki aweza kuwa mchawi wa maisha ya Lazaro?