Maisha yamekupiga? Jiite Mtume, Kuhani au Nabii ndani ya miaka 3 una gari lako

Maisha yamekupiga? Jiite Mtume, Kuhani au Nabii ndani ya miaka 3 una gari lako

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Binafsi nilikuwa miongoni mwa watu ambao ukiwasema vibaya hao niliowataja juu naona kabisa kuwa unakwenda kulaaniwa na hutasamehewa.

Yaani niliona ni heri uue unaweza kusamehewa lakini si kuwasema hao wanaoitwa watumishi wa Mungu.
Sasa niko huru, naweza kujadili na kumsema au kumkemea mpuuzi au tapeli yeyote anayewatapeli watu kwa kutumia jina la Mungu.

Kwa kweli wengi au wote waliojipa vyeo vya Unabii, Utume na Ukuhani ni matapeli. Wengine wana vyeo vya Uchungaji, Walimu na Uinjilist ni matapeli wakubwa.

Wengi wameingia huko kwasababu ya kukosa kazi, kwa jina jingine ni umaskini ndio uliwasukumia huko.
Kwakuwa IQ zetu Afrika ni bellow standard basi wewe ukijiita tu Nabii au Mtume umeshamaliza, mbinu zingine utajifunza hukohuko kwa wenzako.

Hakuna Nabii hapa Tanzania au Afrika mwenye jina kubwa unaweza kuonana naye bila ada. Kwa siku ukionana na wateja 20 tu njaa inapotea automatically. Ada zao zinatokana na umaarufu wao.

Wanapoanza huduma mpaka buku wanachukua. Wakipata umaarufu kuwaona inaanza laki 2 mpaka laki 5.

Afrika umaskini ni kujitakia.
 
Sio rahisi ki hivyo. Mtu asijaribu kama hana wito wa kumtumikia Mungu ataumbuka. Mungu hajaribiwi
Mbona kuhani Musa haumbuki na anawapanga vijana kutoa ushuhuda kwa elfu 20?
Angekuwa na wito wa Kimungu ile ada ya kumwona kwa haraka laki 2 almaarufu FAST TRACK asingeiweka.
Ni ujinga tu umekushika.
 
Fanya utapeli kama Mtume, au Mchungaji, mwaka una gari lako, ila laiti wangekuwa wana fursa ya kukuelezea mwisho wao ukoje usingeongea ujinga. Ulaghai kwenye dini ni mbaya sana.
 
Fanya utapeli kama Mtume, au Mchungaji, mwaka una gari lako, ila laiti wangekuwa wana fursa ya kukuelezea mwisho wao ukoje usingeongea ujinga. Ulaghai kwenye dini ni mbaya sana.
Sasa si wanakuletea pesa wenyewe?
Uliwatuma wawe wajinga?
 
Mbona kuhani Musa haumbuki na anawapanga vijana kutoa ushuhuda kwa elfu 20?
Angekuwa na wito wa Kimungu ile ada ya kumwona kwa haraka laki 2 almaarufu FAST TRACK asingeiweka.
Ni ujinga tu umekushika.
Kuna wenye wito na vipawa ila huuza kwa pesa kama Nabii Balaam Kwenye Biblia ila mwisho wao huwa mbaya

Lakini Mweupe kabisa unajaribu kuiga yatakukuta ya Wana wa Skewa kwenye kitabu cha Matendo ya mitume waliraruriwa na wenye majini

Inaitwa iga ufe
 
Mtoa mada unapaswa ujue haya kwanza sio rahis kama unavyosema na ukitaka iwe rahisi, fanya yafuatayo tafuta kanisa lolote la kilokole uwe muhumin mtihifu soma sana biblia yaan soma, ukiweza hapo tafuta pesa nenda kwa mkali mganga haswa mwambie akubusti toka hapo tafuta eneo jenga banda lako hatua inayofuata jipigie promo kupitia kile ulichokipata kwa mganga mazingaoubwe yawe mengi badili karatas kuwa pesa nk ukiweza hayo we kula hela sasa hayo yote yanaitaji miaka miwili, ukishindwa hayo tafuta mganga ujifunze uganga ukiweza rudi ufungue kanisa mkoa tofaut
 
Mbona kuhani Musa haumbuki na anawapanga vijana kutoa ushuhuda kwa elfu 20?
Angekuwa na wito wa Kimungu ile ada ya kumwona kwa haraka laki 2 almaarufu FAST TRACK asingeiweka.
Ni ujinga tu umekushika.
ni suala la muda tu, kama ni kazi ya Mungu itadumu, kama ni usanii tu itafika muda hiyo huduma Mungu ataifunua ukweli ujulikane
 
Kama ni miaka mitatu hadi nipate gari, afadhali niingie mtaani tu kufanya kazi maana in just 1 year naweza nikatoka na hio gari with right plan and determination.
 
Umenena kweli tupu mimi mwenyewe natafuta kiwanja sehemu nzuri yenye makazi ya watu najenga kanisa naajiri watumishi naanza kukusanya sadaka na zaka
 
Kama unajua Kuna hukumu au maisha baada ya kufa yatayokuchagulia uishije baada ya kuishi hapa duniani basi Hilo kanisa la kutapelia usifungue.

Kuwa nabii au mchungaji unayemtegemea Mungu inawezekana kabisa na Kuna faida kumtegemea Mungu, tatizo lililofanya wachungaji au manabii wawe matapeli kama matapeli wengine ni kwamba hawajui kuishi kiroho Wala Mungu wanayemtangaza hawajui anavyofanya kazi, na Wala hawazijui nguvu za kiroho za Mungu wa kweli zilipo na watu wao wanawafundisha usanii hivyo hivyo.

Haya makanisa kuwepo yanafaida katika jamii yalitakiwa yafanye kazi za jamii yakiwa na kiongozi mkuu, yaani hata kama Yana matawi au bila matawi lakini yawe kwaajili ya kujenga jamii na mazingira Bora ya jamii, dini zote maana yake ni jamii safi ikiwa inamaanisha dini zinapaswa kufanya kazi kuelimisha jamii kutenda mema na kusaidiana na iwe kwa vitendo, na hizo kazi zinazofanywa na wabunge kwenye jamii ndo kazi za dini au makanisa na pale wanapoona jamii Yao imezidiwa au kuwa kizamani bila barabara au huduma za kijamii na wao wameshindwa kufanya basi wanaomba msaada wa serikali ndo dini zilivyopaswa kuwa na zilitakiwa kutambulika kikatiba kama vyama vya siasa vilivyo, na wanapokusanyika popote kwaajili ya huduma njema za jamii Mungu anakuwa pamoja nao, mfano misiba, harusi au jambo lolote na ndo maana wanaojua huwa wanafungisha harusi popote hata iwe hospital maana kusanyiko lao nikwaajili ya matendo mema ya kijamii na kuwa na kiongozi mkuu siyo vibaya ila asiwe kajichagua mwenyewe akasingizia Mungu kamchagua inatakiwa achaguliwe na watu Tena kwa kura ndo maana kuanzisha dini inaweza kuanzishwa kama kikundi baadaye kiongozi anayeonekana atawatumikia vyema ndo mnamchagua.

Haya basi utasema Mungu ataabudiwa wapi, Mungu ataabudiwa popote huku watu wakiwa na vikundi vyao vya kutenda mema na kufundishana kutenda mema na hayo majengo yakukutania kufanya mipango, ila Sasa siyo rahisi kujenga nyumba inayoitwa nyumba ya Mungu hivyo nyumba za Mungu zinajengwa chache au hata Moja nchi nzima na inaweza kuwa inahudumiwa hata na serikali nasema hivyo maana wanaopaswa kukaa huko ni wanadhili wa Mungu yaani watu waliojitenga na dhambi au uasi hao watu wengine wanapelekwa tangu watoto wanawekwa kwa Mungu na wachache wanaenda wakubwa kwasababu maalumu, hizo temple za Mungu ndo zinatoa hata dila ya nchi iendeje maana zinafunuliwa mafunuo kiroho mchana na usiku, muda wote mafunuo yanakuja, mtu wa temple akipata usingizi akiamka anaamka na maono na hawalali vitandani ni chini zaidi godoro, hawaoi Wala kuolewa maana hawaruhusiwi kuishi nje ya temple na temple nisehemu takatifu, malaika wanakuja kutoa muongozo wa nchi, na muda wote nikuomba kwaajili ya watu wote waliokatika nchi.
 
Back
Top Bottom