Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chase Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo

Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chase Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo

Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chaser Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo.

Sasa ni karibia mwezi wa saba huu tangia nianze biashara hii ya kuendesha Taxi bubu. Nilianza mwezi wa tano (May) mwaka huu wa 2020. Biashara imekuwa ngumu sana kwa maana siku hizi kuna Bajaj.

Mtu anaona bora akodishe Bajaj kwa bei nafuu ndio ampeleke mgonjwa hospital au kwenda mjini. Sisi Taxi Drivers tupo hoi biashara imeshuka. Kabla ya Bajaj kuja huko mambo yalikuwa shwari sana mwaka jana 2019, ila sasa hivi ni balaa tupu.

CHASER AVANTE NUMBER "A"

View attachment 1652148

Kabla ya kuja Bajaj kulikuwa na hawa bodaboda ambao wao hawakuwa kikwazo kwetu kwa maana mtu hawezi kukodi bodaboda akabeba maharusi au akampeleka mama mjamzito kujifungua hospitali ya mbali.

Niliwahi kuwaza niendeshe gari hii kama Uber ila kutokana na ukubwa wake wa engine nisingeweza kupata faida yoyote. Ninaombeni msaada wenu wa mawazo.

Nilifungua kibar kidogo Sana wateja wakasuasua , sasa nimeweka banana walau napata 5000 toka kreti mbili kwa siku.

Mitano Tena.
 
Bajaj ni bei ya gar mkuu inakaribia 8M kama una passo ukikutana na bajaj pak pemben apite maana anaendesha chombo ya gharama kuliko yako[emoji3]
Waaaaaaaaaaahhhhhhh[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
maisha yamekuwa mepesi na rahisi kuliko zama zote, kila unacho kitaka kwa kipindi hiki unakipata tena kwa bei nafuu kabisa, bei ya mazao safi kabisa, pembejeo bei ya punguzo,
kilimo kinalipa.
ukikaa bila kujishughulisha kweli utakufa kwa njaa lkn ukijishughulisha maisha rahisi kabisa kama unakunywa maji.
wanao lia hali ngumu ni wavivu wa kazi na watu wa madili
 
Da pole ndugu yangu, tax now days zinachangamoto sana. Utandawazi umerahisisha viusafiri vya haraka, tax inaonekana old school pia tax ni gharama ukilinganisha na bajaji na boda kwa sababu ya mafuta inayo consume.
Ina-consume mafuta mengi lakini zamani nilikuwa ninapata faida kwa kiasi fulani tofauti na sasa...
 
yani ununue babaji milioni 7 ili dereva akuletee sijui 20,000 kwa siku mpaka upate faida cjui lini hapo una-assume haijaharibika ,haijakamtwa,hujaibia spare,haijapata ajali ,mwendo wa presure tu
Asa Milioni saba si bora anunue Vitz..[emoji853]
 
Kwasababu unaamini Bajaj ndio mchawi wako subiri ziishe au na wewe nunua Bajaj.
Siku moja nilipanda Taxi na jirani kulikuwa na Bajaj na bodaboda. Nikamuuliza Yule dereva wa taxi biashara vipi naona hapa mna ushindani na Bajaj na bodaboda.
Akaniambia kuna abiria wa Bajaj,wa bodaboda na wa taxi. Akaniuliza mbona wewe umeacha bajaj na bodaboda umekuja kuchukua taxi?
Kila mtu na abiria wake, jipange mdogo wangu shida inaweza kuwa wewe tukianza na gari unayotumia kufanya taxi.
Ni kweli mkuu mfano bodaboda wateja wao wakubwa ni wadada ,,Bajaj ni mchanganyiko hasa wamama wa sokoni,wanaume kama hana gari au pikipiki yake binafsi ni aidha atakuwa na baiskeli hasa wa mjini kufanya shanting za hapa na pale ila kupanda Bajaj ni kwa shingo upande
 
Back
Top Bottom