Maisha yanabadilika haraka sana, eti kuvaa barakoa kwa sasa ni ushamba

Maisha yanabadilika haraka sana, eti kuvaa barakoa kwa sasa ni ushamba

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Binafsi nashauri wizara iache kuendelea na matangazo ya kunawa mikono na kuvaa barakoa.

Kwani kufanya hivyo ni kupingana na maoni ya raisi sasa hivi wanaovaa barakoa ni wachache sana kiasi kwamba mnaonekana kama tofauti na wengine.

Ukitembea mitaani utashuhudia na hata bila kuambiwa unaona aibu mwenyewe.

Sasa tumeshaanza kurudia maisha yetu yale ya zamani, mikusanyiko, kushikana mikono madiskoni kama kawaida.

IMG_20200606_101824.JPG

Walimu jana Dodoma

My take:
Kila mtu anawajibika na uzima wa afya yake,kwahio uzima wako unategemea jisni unavyojilinda na sio kutokana na muongozo wa Serikali.
 
Hata mimi nimeliona hili, kwa sisi tunaotumia usafiri wa umma mnaweza kujikuta mko wawili au watatu mliovaa barakoa. Sasa sijui Rais anaposema ugonjwa umepungua ila tuendelee kuchukua tahadhari hua wananchi wanamuelewa vp.
 
Ugonjwa umesha isha, tusonge mbele achana na hofu zisizo za lazima.
 
Huyu mzee bado sijaelewa anachokitafuta..
 
Wacha tuu nionekane mshamba. Hapa nipo kwenye daladala (Tena sio kifodi ni coaster) lakini Ni Mimi peke yangu ndo nimevaa na it's ouky kujilinda ni muhimu.
Nipo kwenye Coaster ya Temeke - Stesheni muda huu. Ni wawili tu tumevaa barakoa.
 
Ugonjwa umesha isha, tusonge mbele achana na hofu zisizo za lazima.
Tanzania si kisiwa kumbuka Kama kwa wengine bado upo Hali still muingiliano ni mkubwa,muhimu kuendelea kuchukua taadhari binafsi kuliko kuwasikiliza wanasiasa wenye malengo ya kisiasa
 
Wengi hawaelewi kabsa,hata raisi hataki uvaaji wa barakoa kabisa ndio mana anaponda kila wakati
Hata mimi nimeliona hili,kwa sisi tunaotumia usafiri wa umma mnaweza kujikuta mko wawili au watatu mliovaa barakoa. Sasa sijui Rais anaposema ugonjwa umepungua ila tuendelee kuchukua tahadhari hua wananchi wanamuelewa vp.
 
Wacha tuu nionekane mshamba.... Hapa nipo kwenye daladala (Tena sio kifodi Ni coaster) lakini Ni Mimi peke yangu ndo nimevaa na it's ouky kujilinda Ni muhimu
Thats why I love you. Take care
 
Pigo lilianza China
Ikaja Iran
Ikahamia Italy
Ikawatandika Spain
Ikavamia England gafla
Ikalipua USA sasa iko Brazil inachakaza tu sasa inatuchora tu,mataifa yote yako vizuri kimfumo wa afya sisi ni kina nani?
Kwa hiyo hujaamini kama ngoma imedunda Tz!
 
Ajabu sana kwamba Tz tuna discourage watu kuvaa barakoa. Tuna serikali ya kienyeji zaidi duniani.
 
Huku kwetu Bondeni kama huna Barakoa basi hupati huduma yotote.
 
Ajabu sana kwamba Tz tuna discourage watu kuvaa barakoa. Tuna serikali ya kienyeji zaidi duniani.
Kabisa. Alafu unaweza kuta ayo ni mashariti wa waganga wake wamempa. Wanataka damu za Watz.
 
Back
Top Bottom