mtoto wa mchungaji
JF-Expert Member
- Oct 24, 2020
- 279
- 480
Juzi juzi kila mtu alishuhudia Mwenyekiti wa Chadema akiwa ameshuswa kutoka angani na muda wake mwingi alikuwa akiumalizia Segerea akitumia ndoo kwa matumizi ya msingi. Mfalme huyu wa anga ambaye alikuwa na uwezo wa kubadirisha gia angani hata malaika walikuwa wanashangaa. Wote tulishuudia akikalishwa chini na hata kushindwa kuzibadilisha tena gia akiwa mchangani.
Maisha yanaenda kasi sana leo Mbowe tayari ameshatangaza kuwasamehe waliorudi kuunga juhudi na kuwaambia kuwa milango ipo wazi tena na msamaha juu. Hivyo Mzee Lowasa, Mzee Sumaye, Masha, Nasari na wengine wameambiwa milango ipo wazi mfalme wa anga anapaa kidigitali sasa hivi.