Maisha Yanaenda Kasi sana.. kwa Ninayoyaona!

Maisha Yanaenda Kasi sana.. kwa Ninayoyaona!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Ndio Maisha yanaenda Kasi sana, Baada ya kupata Chakula cha jioni niliona ni vema kwenda club moja apa kitaa..

Mpaka kufika mida ya saa sita usiku huu nilikuwa nimelewa kispoti..
Kidogo mbele ya Macho yangu Niliona vibinti vitatu.. Vikicheza na kujirusha kwa staili tamanishi..

Kwa uzoefu wangu wa mambo ya club nilivumbua dhahiri kwamba vibinti hivi tayari ni vizoefu kwenye michezo ya club..

Kama vile siamini Masikio yangu nikasikia kibinti kimoja kikimwambia Mshikaji mmoja kwamba "Kama mtu hataki kucheza na wewe si umuache..akaongeza kwamba isitoshe nimekuja na bwana wangu hapa"

Hapa Mzee mkubwa Khan nikahamasika kukatazama haka kabinti usoni.. ni kama vile siamini macho yangu.. Binti alikuwa mdogo kiumri akizidi saana ana miaka 13..Kidogo nikamuuliza bidada mmoja karibu yangu kakajibu ndo kamemaliza darasa la 7 na hao wenzake..!

Badala ya furaha nilijikuta nikiingia katika wimbi zito la masikitiko.. Nikijiuliza taifa la kesho litakuwa na vijana wa aina gani?.. Vita dhidhi ya UKIMWI itafanikiwa kweli? ukizingatia vibinti vidogo kama hivi havina source ya hela lazima viliwe ndo vipate japo pesa ya kula!

Wazazi wa watoto hawa wako wapi? Tatizo limekuwa wazazi au watoto wenyewe?

Kwa Ninayoyaona Maisha Yanaenda Kasi sana!

Divine Khan
 
Bro unaenda vipi club wanazoruhusu underage kuingia! Raise your game bro.
Mkuu Huku Kijijini kwetu Club ndio zinaingia.,btw hata Nikiwa Dar es salaam Niishaona Mabinti Kibao Underage Next door hata Maisha!
 
dah,ina maana hivyo vitoto havina wazazi?
Au wazazi ndo wakina amber ruty
 
Ni Hatari Mkuu Kabinti Miaka 13 Kanacheza dunia ya Saba.. mtoto anavunjika vunjika mithili ya samaki asiye na Mfupa!

Hivi vitoto vipo vingi sana, nakumbuka kuna tulivyovikuta club moja usiku wa sa 7 nje vinatetemeka baridi. Nilisikitika sana. Tulivichukua tukavihoji vikatuambia vimetumwa na shangazi yao.

Kuwahoji vizuri zaidi na kitisho kidogo tukagundua hata huyo shangazi si shangazi bali ni mama muuza watoto makahaba. Na lazima wapeleke pesa 60,000-100,000 siku za kazi na 120,000-200,000 wik end. Hiyo ni lazima wala si ombi na lazima wahakikishe wanaipata.

Huwezi amini wale watoto walikataa kabisa kutuambia wanapoishi, hawaogopi hata mambo ya kupelekwa polisi na wazi wakatuambia wanafahamiana na baadhi yao.

Tuliwafuatilia wale watoto wiki nzima ila tulifanikiwa kumuokoa mmoja tu kati ya 6, 5 walikuwa washakolea mchezoni
 
dah,ina maana hivyo vitoto havina wazazi?
Au wazazi ndo wakina amber ruty

Wengi wanaletwa mjini kama bidhaa mkuu, yaani ni hivi biashara haramj ya kuuza watu bongo ni kubwa sana. Kwa haraka haraka kwenye ma club na madanguro mengine hukosi watoto wadogo 8-13 walioingia kwenye biashara ya ngono.
 
Tuliwafuatilia wale watoto wiki nzima ila tulifanikiwa kumuokoa mmoja tu kati ya 6, 5 walikuwa washakolea mchezoni
Mkuu Huu mchezo ukikolea kwa mtoto wa kike ni ngumu mno kumuokoa, Bora hata wa kiume!
 
Mkuu kuna Mengi ya kujiuliza.. Na vizee vinadandia kama kawaida!
leo kuna RTO mstaafu kakamatwa na kitoto cha darasa la tano ambacho huwa anakila mzigo.
Dunia ina mengi aisee
 
Back
Top Bottom